Siasa si uadui: Dk. Tulia amtembelea mama wa Halima Mdee aliyelazwa hospitali

Siasa si uadui: Dk. Tulia amtembelea mama wa Halima Mdee aliyelazwa hospitali

Siasa haziondoi utu wetu. Hivi karibuni Mbowe aliwaalika wabunge hao maarufu sana katila hafla ya kuchangia ujenzi wa kanisa.
---

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, leo Januari 31, 2024 amemtembelea na kumjulia hali, Theresia Ngowi ambaye ni mama mzazi wa mbunge wa viti maalumu, Halima Mdee.

Dk Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amemtembelea mama huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma kwa matibabu.
Hili la ''siasa siyo uadui'' inabidi umfuate Magufuli kaburini umwelimishe.
 
Mara ya kwanza alitembelewa Wodini na Waziri Mkuu , Jana ametembelewa na Spika wa Bunge , leo ametembelewa na Rais .

Hii ni Bahati kubwa sana !

View attachment 2890779
Nyie chadema ni wa ovyo sana. Itikadi mpaka kwenye ugonjwa wa mtu!
Samia bila kujali itikadi alienda kumsalimia kamanda msaliti wakati amelazwa Nairobi, nyie kumsalimia mama wa Halima mnaona nongwa. Mungu anawaona.
 
Mbunge wa CCM tena Spika kumtembelea mama wa mbunge viti maalum kupitia CHADEMA ni jambo la busara sana. Spika ana upendo hata kwa chama kinachokaribia kufa.
Chunga sana matamanio yako.
Unaweza tangulia wewe kabla ya kuona "kukaribia kufa" kwa CHADEMA.
Mfano hai ni mwendakuzimu.
 
Hivi "mujahedeen" wa JF hawajawahi kuandamana sababu ya upupu unaoandika hapa jukwaani!!??
Maana hiyo ID yako na yale unayoyaandika ni mbingu na ardhi.
Sema alipo halima kuna ester, au alipo mdee kuna bulaya.
Hayo mambo ndo makamu mwenyekiti wao anayapigania kuita ni faragha yasiingiliwe.
 
Kwani sasa hivi si wamoja hao? Kuna uadui gani kati yao?

Ila jamani kila alipo Halima kuna Bulaya, mi nataka BFF kama huyo.
Huu upendo ni wa ajabu!
hiyo ya mdee na bulaya ni sawa na ule msemo wa "chombo ya fundi"
 
Siasa haziondoi utu wetu. Hivi karibuni Mbowe aliwaalika wabunge hao maarufu sana katila hafla ya kuchangia ujenzi wa kanisa.
---

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, leo Januari 31, 2024 amemtembelea na kumjulia hali, Theresia Ngowi ambaye ni mama mzazi wa mbunge wa viti maalumu, Halima Mdee.

Dk Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amemtembelea mama huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma kwa matibabu.
Hakuna jipya ni kawaida tu
 
Back
Top Bottom