Hero
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 3,919
- 2,843
Nachokoza mada tu leo,
Mimi ni mdau katika elimu yetu ya juu ya vyuo vikuu vya Dar es salaam, hasa katika kuandaa madaktari na waambata wao.
Hali ilivyo sasa inatia shaka sana katika utoshelevu wa wakufunzi katika fani za 'biomedical sciences', hasa katika eneo la 'Human Anatomy' (anatomia ya binadamu), 'Human Physiology' (fisiologia ya binadamu), 'Human Pathology' (pathologia ya binadamu), na 'pharmacology'
Wakati wakuu wa vyuo vingi hasa vya udaktari wakikurupuka na kurukia matumizi ya GPA yanayotumiwa hasa na vyuo vya social sciences katika kuajiri wanataaluma, badala ya umahili wa somo husika tu, upatikanaji wa wakufunzi wenye viwango vya GPA husika imekuwa ni ngumu sana. Na hata wale wachache sana wakipatikana wanakuwa hawana utayari wa kufanya kazi katika vitengo husika.
Wakati upatikanaji wa viwango husika vya GPA katika vyuo vya sayansi ya jamii ni 'relatively doable' kwa maana mwanafunzi anasoma katika kipindi cha miaka isiyozidi 3 na kupitia idara zisizozidi tano, kwa masomo ambayo kiuhalisia hayalingani kiuzito na masomo ya udaktari, wanafunzi hawa wengi hupata GPA husika bila kuvuja jasho sana. Na kwa mantiki hii, kuweka vigezo vya GPA husika katika upatikanaji wa wanataaluma katika vyuo hivi haina ukakasi sana.
Ugumu wa madaktari kupata GPA husika hata ukiacha waliosoma 'kipindi cha kukomoana' pale MUCHS (2002 backwards) ni kutokana na ukweli kwamba, mwanafunzi anayesomea udaktari anapitia idara zaidi ya 16 (katika miaka yake mitano) ambazo zote anapaswa kufaulu angalau kwa kiwango cha B+ ili aweze kufikia GPA ya kuweza ajiriwa katika idara husika.
Uhalisia umekuwa mgumu sana ukuzingatia mapungufu na changamoto nyingi ambazo taasisi zetu za elimu ya juu zinazopitia. Ndio maana unakuta Watanzania wanapokwenda kusomea udaktari nje ya nchi kama Urusi, China nk hurudi wakiwa na vyeti vilivyosheheni misonge (A), na kuwaacha wale waliosomea nchini na makalayi (C).
Kitu cha kushangaza ukiwapambanisha ktk 'interview' mara nyingi unakuta waliosomea Tanzania huwa wapo vizuri zaidi katika umahili na kuwaacha wale wenye misonge wakishangaa. Lakini kwa sababu ya viwango duni vya GPA hawa wabongo hubaki kusoma namba na kuwapatia wale waliosomea nje ya Tanzania kufaidika na nafasi husika bila kuzingatia umahili wao katika nafasi husika.
Hapo siku za nyuma, cheti cha udaktari hakikuwa na madaraja kwa maana kuwa hukuna daktari daraja A, B,C, D n.k. Kilichokuwa kikiangaliwa ni kutimiza kiwango cha kutibu mgonjwa kwa usalama. Na inapofikia daktari anataka kubobea au kuwa mwanataaluma, ufaulu wa somo husika kwa kiwango kisichopungua 'B' ulifuatwa. Kwangu mimi hii nafikiri ilikuwa na maana zaidi, maana masomo mengine hayatakuwa na tija sana ukilinganisha na somo husika atakaloajiriwa kulifundisha na kubobea.
Matatizo ya kukosekana kwa wanataaluma hasa katika maeneo hayo juu (Human Anatomy (Anatomia ya Binadamu), Human Physiology (Fisiologia ya Binadamu), Human Pathology (Pathologia ya Binadamu), (Pharmacology) kumeviweka vyuo vingi vya madaktari nchini ktk mazingira magumu pasi kujua cha kufanya ingawaje ki uhalisia cha kufanya kipo wazi. Utakuta wakuu wa vyuo wakilalamika kuwa hawapati wakufunzi wenye viwango vya GPA husika kwa mujibu wa TCU.
Cha kushangaza sana, TCU wenyewe wanawashangaa wanazuoni hao (wakuu wa vyuo) maana wao wakuu wa vyuo ndio waliopeleka mapendekezo ya viwango vya GPA husika, hali wakijua uhalisia katika fani za udaktari, sasa iweje wao wenyewe waanze lalamika!
Kimsingi TCU husimamia maamuzi yaliyopitishwa na wakuu wa vyuo husika ili kuhakikisha viwango hivyo vinafikiwa katika vyuo vyote, sasa kama wanazuoni hawa wanaweka viwango visivyoweza fikika (inatia shaka) uwezo wao wa kufikili.
Katika nyakati tofauti, nimekuwa nikisikia TCU wakiwataka wanzuoni hao wakae na kuleta mapendekezo ya vigezo vyenye uhalisia vitakavyofuatwa na vyuo vetu vya madaktari ktk kuajiri wanataaluma hao badala ya kulalamika katika njia. Nachelea kusema hawa wakuu wa vyuo husika bado kufanyia kazi maelekezo haya yenye tija saana katika muktadha wa vyuo vyetu vya madaktari Tanzania
Niwaombe sana wanazuoni hawa, wakae chini na wapeleke mapendekezo yenye uhalisia TCU juu ya criteria/vigezo vinavyoendana na uhalisia katika kuajiri wanataaluma katika vyuo vikuu vya madaktari Tanzania ili kuvinusuru na madhira vinayopitia vyuo vyetu na wanafunzi husika kwa kukosa utoshelevu wa wanataaluma hawa katika idara mbali mbali katika 'medical schools'.
Kama nilivyoanza hapo awali, leo nimechokoza tu mada.