Wyatt Mathewson,
assuming everything is controlled and hence constant, GPA inge'suggest' hiyo reasoning capacity sijui unayojaribu kuitajata, lakini uhalisia hauko hivyo ndugu yangu, huyu kasoma chuo X katoka na misonge na GPA ya 4.0 huyu mwingine kasomea chuo Y amerudi na makalayi mengi na vi'B' vichache. Ukija waweka katika interview ya analytical na reasoning capacity huyu mwenye GPA ya sisimizi ya shule Y anakuja fanya vizuri kuliko huyu mwenye GPA mlima ya chuo X. Hapo sijui unasemaje sijui. Huu ndio kwa bahati mbaya sana umekuwa uhalisia ktk kutafuta wakufunzi wa vyuo vya udaktari.
Labda kama ww haupo kwenye fani ya udaktari, umetoka na GPA ya 4.0 ya Siasa/ Historia ndio huwezi elewa nachokiongelea. Lakini kama hata umeshawahi fanya 'observation' kidogo tu ktk vyuo vyetu vinavyoandaa madaktari, utaelewa magumu vinavyopitia. Kwenye political sciences nyie endeleeni tu na GPA za 5.0
Msingi wa hoja yangu ni kuweka vigezo vinavyoakisi uhalisia ili kuepuka kuathiri vibaya mafunzo ya fani ya udaktari na ambata zake!.