Siasa za Kenya ni za kushangaza sana

Siasa za Kenya ni za kushangaza sana

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
1,907
Reaction score
3,560
Siasa za Kenya kuna wakati zina shangaza sana sasa sijui ni kusalitiana au vipi?

Bunge la Kenya linataka kumkong'oa Naibu wa Rais wa Kenya Rigadhi Gachagua.

Naibu Rais huyo wa Kenya anakabiliwa na tuhuma za kuendeleza ukabila kwa watu wa mlima Kenya pia kutokuelewana na Raisi William Ruto.

Wanaeleza kuwa ni mara kadhaa naibu wa Rais Gachagua hajahudhuria hafla za Rais Ruto.

Siku za hivi karibuni pia Naibu Rais huyo alilalamika kuondolewa kwenye kundi la whatsapp la Raisi Ruto.

Gachagua na wandani wake wamelalamika kuwa pengine washauri wa Rais Ruto wanamshauri vibaya awadharua watu wa mlima Kenya ilihali wao ndio walimpigia kura nyingi.

Nini kinakushangaza kwenye Siasa za Kenya ?
 
Siasa za Kenya kuna wakati zina shangaza sana sasa sijui ni
kusalitiana au vipi?

Bunge la Kenya linataka kumkong'oa Naibu wa Raisi wa Kenya
Rigadhi Gachagua.

Naibu Raisi huyo wa Kenya anakabiliwa na tuhuma za kuendeleza
ukabila ya watu wa mlima Kenya pia kutokuelewana na Raisi William Ruto.
Wanaeleza kuwa ni mara kadhaa naibu wa Raisi Gachagua hajajudhuria hafla
za Raisi Ruto.

Siku za hivi karibuni pia Naibu Raisi huyo alilalamika kuondolewa
kwenye kundi la whatsapp la Raisi Ruto.

Gachagua na wandani wake wamelalamika kuwa pengine
washauri wa Raisi Ruto wana mshauri vibaya awadharua watu
wa mlima Kenya ilihali wao ndio walimpigia kura nyingi.

Nini kinakushangaza kwenye Siasa za Kenya ?
Kwani Tanzania hakuna hayo?
 
Gachagua alitaka kucheza na upepo wa Gen Z, bahati mbaya sana Ruto aliweza kumu outsmart kwa kuachana na uchura kiziwi ikabidi awasikilize Gen Z, na matokeo yake ndiyo tunaona. Ilivyokuwa inaonekana Ruto alikuwa anaambiwa mambo yako poa wakati huo huo akawa hafuatilii na vyombo vya usalama vikawa vinamuambia kila kitu iko poa tutawathibiti kumbe ndiyo hivyo na Gachagua akawa anategemea Ruto akiong’olewa basi yeye awe Rais wa mpito hahaha
 
Kenya kuna misingi imara ya mihimili ndiyo maana yeyote anayekiuka anaweza kuwajibishwa tofauti na tanzania
Ni kweli nimeiona kwa hule naibu kamishna wa polisi ilibidi aende kuiomba

msamaha mahakama.
 
Baptist naona wewe ni mbobezi wa Sayansi ya Siasa umeona nini?
Kura za Gachagua ndio hizo hizo Kura za Ruto, ukimtoa Gachagua anaondoka na Ruto

Gachagua amepata unaibu Rais Kwa kura za Wananchi ingekuwa aliingia kama Mpango sawa hilo la kumuondoa peke yake lingewezekana
 
Gachagua alitaka kucheza na upepo wa Gen Z, bahati mbaya sana Ruto aliweza kumu outsmart kwa kuachana na uchura kiziwi ikabidi awasikilize Gen Z, na matokeo yake ndiyo tunaona. Ilivyokuwa inaonekana Ruto alikuwa anaambiwa mambo yako poa wakati huo huo akawa hafuatilii na vyombo vya usalama vikawa vinamuambia kila kitu iko poa tutawathibiti kumbe ndiyo hivyo na Gachagua akawa anategemea Ruto akiong’olewa basi yeye awe Rais wa mpito hahaha
Ruto aliweza kuruka kiunzi hiko sio, hali ilikuwa tete sana.
 
Kura za Gachagua ndio hizo hizo Kura za Ruto, ukimtoa Gachagua anaondoka na Ruto

Gachagua amepata unaibu Rais Kwa kura za Wananchi ingekuwa aliingia kama Mpango sawa hilo la kumuondoa peke yake lingewezekana
Hapo nimekupata vizuri, na mimi nimeshangaa kuona
wabunge wanao simamia kuondolewa kwa Gachagua ni

wakutoka mlima Kenya nikajiuliza ni lini Kenya wameacha
ukabila kwa kiwango hiko? Kumbe inaweza kuwa ni arrangee 🤣🤣
 
Ahaa haaa ila kuna wasomi pia kule kama Mawakili, kwani ina ongozwa

na mtu mmoja mkuu?
Mkuu chama kinao viongozi wanaotoa mamuzi ya chama ,embu fikiria cdm maauzi yanayotolewa na hawa viongozi walifeli elimu ya sekondari mfano ,Mzee Mbowe,Sugu,Lema na Wenje.Hawa ni vipngozi waandamizi 🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Back
Top Bottom