Siasa za nchi yetu pamoja na wanasiasa wetu wenye tamaa

Siasa za nchi yetu pamoja na wanasiasa wetu wenye tamaa

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,951
Reaction score
19,766
Habari jamii Africa.

Mmmmh.

Poleni wananchi wa Tanzania,
Poleni raia wa Tanzania.

Lakini poleni zaidi wapenda Mabadiliko wa Tanzania.

Mimi ni mmoja wa wapenda Mabadiliko,ambaye sipo upande wowote wa chama,japo kazi zangu naweza jikuta natekeleza ilani ya CCM ila nachojua Mimi nawajibika kusukuma maendeleo ya taifa basi.

Ndugu zangu Kwa taarifa nazozipata kutoka kwenye vyanzo vyangu,
Pamoja na watu wenye ushawishi nchini,au hata wenye ushawishi mitandaoni,ni kwamba ni ngumu ni vigumu na haitakaa itokee kupata mpinzani wa kweli.

Naweza sema asilimia 97 watu woooote wanaoanzisha vyama vya siasa ,malengo Yao ni kupata maslahi Yao na familia zao Kwanza ndipo watafuata wananchi masikini.

Hakuna mwanasiasa yeyote mwenye upendo wa kweli ambaye anaweza kuwaletea maslahi watanzania zaidi ya kutaka kujineemesha mwenyewe kwanza.

Agustino Lyatonga Mrema ndiye mwanasiasa machachari kabisa kutoka chama cha NCCR_Mageuzi,ambaye alionesha ushawishi Kwa baadhi ya watu.

Ibrahim Lipumba toka Chama cha CUF naye aliwahi kuleta presha fulani kwenye nchi hii kiasi cha ukanda wa pwani kudhani ni suala la muda Lipumba ataingia Ikulu.

Dr.Wilbroad Silaa Naye alionesha nguvu na ushawishi mkubwa toka Chama cha demokrasia na maendeleo kiasi cha wakaskazini kuhisi wana asilimia kiduchu watapeleka watu wao Ikulu.

Ndugu zangu hao ni baadhi ya wanasiasa wachache ambao kabla hujawagundua unaweza sema wapo tayari kuipigania hii nchi kumbe ni Kwa maslahi Yao kutaka kuandika historia kwaniaba yao na familia zao.

Unakumbuka tukio la Edward Ngoyai Lowassa Kukatwa?

Yes ni Kukatwa kutoka CCM alikokuwa anawania urais , kwasababu walizozijua wao,hii ikaamsha hasira Kwa wananchi, kwanini Lowassa akatwe,Mtu ambaye njia ya Ikulu ilikuwa nyeupe,yaani kama ni kula chakula kilikuwa mezani,halafu Lowassa keshanawa kabisa halafu anaambiwa ,hata ukiwa huli,
ENL akaona haiwezekani,Kwanza alikuwa na watu ,pili alikuwa na nguvu na Sera tamu.

Akaamua kuhamia side B akapokelewa Kwa mikono miwili ,akasimamishwa kuwa mgombea uraisi kupitia UKAWA yaaaaaani namaaaaaniiiisha vyama vyote,viliunganisha nguvu vikisimamisha mtu mmoja tu,aliwahi kushika nyadhifa kubwa na muhimu nchi hii,watu walimfurahia,pamoja na kashifa zoooote ikiwemo RICHMOND lakini babu ENL alisafishwa akatakasika akang'aa kama dhahabu kwenye Moto,wangekuwa na uwezo wangemuweka juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro lakini hakukuwa na haja
Neno M4C lilitamkwa hadi na mabubu na viziwi walilisikia vizuri kwani njia ya Ikulu ilikuwa wazi ,huku ENL akisubiri kuapishwa tu 🤣🤣🤣🤣🤣

Lakini Nyokooooo CCM achaneni nayo? Mungu ni mwema alisikia kilio chetu akatuletea Rais ambaye hatukumtarajia.mwanangu Sana , rafiki yangu,Nilizoea kumwita Baba na aliwahi kunichapa kibao tukiwa huko mkoani Lindi hakupenda mtu mzembe.
Nilitamani nimsukumie mikono lakini alikuwa ni Baba, kiongozi na mwenye msimamo wa kweli kwenye kazi zake asiyependa kuyumbishwa.

Turudi huku, CDM
Ebwana eeh Ndoto za uraisi za ENL zilizimika kama kibatari kwenye Upepo mkali,mbaya zaidi kamari waliocheza CDM ikawa mbaya kwani hawakuwa na cha kujitetea Kwa walishachanganya mkeka Kwa kuweka magoli mengi kwenye mechi ya kukamiana.

Kiasi walipoteza mvuto,unajua kwanini, wananchi ni kama makondoo tu,Leo wapo huku kesho huku wanaodanganywa na tishet na kofia.

Wachache wanaahidiwa vyeo.

Wengi ni tamaa ya Pombe za bure na nyama pamoja vijibahasha.ili kunusuru familia zao.

Hakuna Mtu kutoka upinzani atachukua nchi hii,labda mpinzani atoke CCM.

Nisameheni wanabodi huenda nimeamka nazo hapa navuta muda nikawashangilie.

Renaissance Sportive Berkane.
Asubuhi njema
 
Vyeo vinawapa tamaa sana hata wakistaafu bado wanapewa vyeo.
Jiulize kwa nini wanatanguliziwa haadi za vyeo watimize wanacho taka
 
Leo hii mwamba amegeuzwa kitendea kazi cha mboga mboga kukibomoa chama alichoshiriki kukijenga kwa jasho na damu, ni ngumu kuamini lakini ndiyo ukweli wenyewe.
 
Vyeo vinawapa tamaa sana hata wakistaafu bado wanapewa vyeo.
Jiulize kwa nini wanatanguliziwa haadi za vyeo watimize wanacho taka
Ndiyo hapo Tanzania kuwa huru bado Sana
 
Mkuu umeongea kweli kabisa lakini twende mbele turudi nyuma………LISSU na HECHE ndio WAPINZANI wa kweli kuwahi kutokea hapa Nchini

Hii CHADEMA ingekuwa imelegea legea mwaka huu CCM walikuwa wanaizika ila bahati nzuri Mungu akaamua kuwatetea Lissu akashinda………….na kwa baraka zake,siku hiyo Mvua ikapiga Dar nzima

Ila jambo wanalopaswa kufanya kwa sasa ni kutoruhusu kuwataja taja wale wanao hama Chama chao,kwani CCM wametengeneza haya mazingira ili kuwatoa CHADEMA kwenye njia ya kuzungmza maovu ya CCM
 
Back
Top Bottom