Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
Nimesema sana nimebezwa.

Lazima tuwe na viongozi wenye hekima, busara na wenyekujali utu. Mwl Julius Nyerere pamoja na udogo wake hakuipuuza wala kuidharau Zanzibar, aliipa heshima kamili. hakuwapuuza wala kuwabaguwa majirani zake, tumepata watawala wasionaaibu wala hawaoni mbele, kwao lazima visasi na uwongo ndiyo sera.

Tutawapuuza wanyarwanda lakini kuna baadhi ya watanzania watapoteza mali na hata kufilisika kwa sababu za kijinga kabisa wala hazina mashiko kwa mtu yoyote mwenyekufikiri vema.

Lazima tuzingatie mahusiano bora na majirani zetu kwa matokeo bora ya tanzania ya kesho
Wakati wa Mwalimu, serikali ya Habyarimana (ingawa simfagilii) na serikali ya Kaunda ... baadae of course Samora. Wengine wote wanaotuzunguka walikuwa wamepigwa ban.

Hujui historia ya nchi yako, kwa hiyo nenda uani.
 
Watakaoumia ni wanyarwanda wenyewe,kwani ninachojua hakuna mfanyabiashara anayepata hasara hata siku moja! hivyo kama bidhaa kama zinapelekwa Rwanda bei ya bidhaa zitapanda tu!

Kagame ana gundu. Sijui anajua athari ya hatua hiyo ktk uchumi wa mwananchi? Ongezeko la kodi litamwathiri zaidi mlaji wa mwisho. Ajue kwamba nchi yake haina bandari. Najua an hasira. Lakini hatuwezi.
 
Tumia akili, hapo maana yake ni kuwalazimisha wafanyabiashara wa Rwanda wapite Mombasa.
sasa akiwalazimisha watumie mombasa hujui ni sawa na kuwalazimisha watumie kitu cha GHARAMA KUBWA na waache NAFUU?changamsha akili wewe,KAGAME amechanganyikiwa.
 
daa inaonesha ni hasira za rwanda kwa sababu ya wakimbizi wao kuwarudisha kwao, na kwa mtazamo wangu swala hili litaleta madhara makubwa hapo badaye,
 
Mr Slim hajitambui hivi hajui kuwa atawaumiza wananchi wake mwenyewe...!!!??au ndo analazimisha wafanyabiashara watumie bandari ya Mombasa...???/atajijua na utahaira wake ......may be damu za watu wasio na hatia zinavuruga mfumo wake wa kufikiri

Hasa anapohusishwa na damu za marais wawili wa nchi mbili tofauti tena kwa mpigo!
 
mkuu, kagame na wafuasi wake wanajidanganya sana.

Kwa hiyo kupoteza kiasi hicho unaona siyo tatizo? Kumbuka tunatakiwa kukuza uchumi wetu haitakiwi tuwe pale tulipokuwa jana inauma sana kama uchumi haupandi je inaumaje unaposhuka?
 
Wakati wa Mwalimu, serikali ya Habyarimana (ingawa simfagilii) na serikali ya Kaunda ... baadae of course Samora. Wengine wote wanaotuzunguka walikuwa wamepigwa ban.

Hujui historia ya nchi yako, kwa hiyo nenda uani.

Unaongelea historiagani kobelo au do hizi hadith za kubumba?

Kenyata hakuelewana na Nyerere nataka uniambie kama ulisikia mwl kuwafukuza wakenya

Kamuzu banda wa malawi pia hakuelewana na mwalimu uniambie kama mwl aliwafukuza wanyasa

hiyo nii mifano miwili tu, nataka ulieleze jukwaa kwa mifano japo miwili ni lini na majiranigani mwalimu aliwafukuza.
 
Kagame ana gundu. Sijui anajua athari ya hatua hiyo ktk uchumi wa mwananchi? Ongezeko la kodi litamwathiri zaidi mlaji wa mwisho. Ajue kwamba nchi yake haina bandari. Najua an hasira. Lakini hatuwezi.
Anatamani hata apewe mita za mraba 10000 tu kwe ufuki wa Bahari ya Hindi ili apate bandari! Kuna wakati alisema anatamani apewe bandari ya Dar aiendeshe, watu tukashangilia kwamba sisi hatufanyi kazi kumbe jamaa ana usongo kwa kuwa land locked. Wacha acheze na mfanyabiashara wa Kenya ataingizwa mikataba ya Mangungo na hatatoka. Ngoja siku wakgombea tena madini na rafiki yake Museven sijui atapitishia wapi hayo malori. Anajichongea tu uchochoro wa matatizo. Tumuache tu tujifanye kama hatufahamu diplomasia kuna siku atakuja mwenyewe akiwa ameinama na kusujudu.
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

Kutoka Rwanda bidhaa gani tena? Kwan kuna bidhaa tz yahitaji from Rwanda
 
Afadhali wambie Kamanda, unajua Watanzania ni kama tumelogwa. Tunashabikia mambo bila kufikiria, watakao umia ni haohao wanaomiliki biashara za malori. Na hii maana ya haraka haraka ni kuanza ku discourage mizigokushushiwa Dar sasa watalazimika kwenda Bandari ya Mombasa.

Mambo mengine adghabu zake ni hapa hapa tu hakuna kungojea,

TAFAKARI
Tusiwe na papara juu ya ongezeko ilo,ngoja tuone itakuwaje baada ya mwezi,tutapata mrejesho kamili
 
Hasa anapohusishwa na damu za marais wawili wa nchi mbili tofauti tena kwa mpigo!

Naungana na wewe kama nikweli na kunaushahidi, lakini tunaposikitikia marais wa nchi jirani inakuwa vipi pale

Kolimba anapotezewa uhai wake kwa utata

Mwangosi anapotezewa uhai wake kwa utata

Imran kombe anapotezewa uhai wake kwa utata

Watanzania tunaishi kwa kutazama sana ya wenzetu bila kujitazama sisi kwanza kamatunatimiza yale tunayowalalamikia wenzetu. Tuanze kuihoji serikali yetu kwanza kwa watanzania wenzetu tena wengi tu ndipo tupate ujasiri wa kuhoji ya majirani zetu.
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

Duh mkuu upo na huku? Ninyi watu mna mshkamano kweli kweli. Wote ambao mpo dar mnafahamiana na sehemu mnayoishi kila mmoja wenu. Wa mwanza wote wanafahamiana. Nakumbuka mwaka 1990 jinsi ambavyo mlikuwa mki recruit vijana wa kujiunga na RPF pale Mwanza! kwa hiyo Kagame naye ameamua kupuuza makubaliano ya EAC kama Tanzania? Magari ya wanachama wengine wa EAC yanatozwa kiasi gani hapo Rusumo ama kwenye mipaka mingine? M23 inaanza kuvurga taratibu
 
Malipo ya ubaguzi, ukijiona wewe mbabe, wenzako nao watakuonesha jeuri yao, tulipofanya unyanyapaa kwa wanyarwanda mlidhani wao watatulia tu kama kondoo!

Majuto ni mjukuu.

hajuti mtu hapa! kodi ikipanda mlaji ndio atajuta kwa bei ya bidhaa husika kupanda (pia na kuadimika kwa bidhaa hizo) na ktk mazingira haya yule yule mhamiaji-haramu mwenye stress aliyetoka tz juzi ndio last consumer ; sasa hapa hamuoni kwamba mh. Kagame si anazidi kujitengenezea bomu!
 
Atacompansate na mapato ya madin kutoka drc anaakili ya hesabu kuliko yako, unadhani kwanini hakuna nyumba za nyasi kule tafuta majibu.

unajua kinachoendelea congo au unaota....congo haingii tena. Framework ya UN ni kupokonya silaha vikundi vyote vya waasi. Baada ya hapo akitia mguu huko ni agression to full scale war against rwanda. Kuweweseka kwake ni kwa sababu ya mkong'oto wanaoupata vibaraka wake M23 kutoka kwa majeshi ya drc na UN chini ya Brig General Mwaki wa TZ.
 
hajuti mtu hapa! kodi ikipanda mlaji ndio atajuta kwa bei ya bidhaa husika kupanda (pia na kuadimika kwa bidhaa hizo) na ktk mazingira haya yule yule mhamiaji-haramu mwenye stress aliyetoka tz juzi ndio last consumer ; sasa hapa hamuoni kwamba mh. Kagame si anazidi kujitengenezea bomu!

Ni mtazamo tu mkuu kila mtu anatathimini anavyoona, lakini ile mikutano yao ya kigali, nairobi na kampala inamalengo yake.

Na hivyo hivyo wanautashi n akili kama sisi nk tunatofautiana katika kudhibiti mapato na utekelezaji wa mipango-mikakati.

pamoja na udogo wa nchi yao mapato yao sidhani kama yanavuja kama ya kwetu na hapo ndipo gharama za uendeshaji zinapoanzia.
 
Umenena vyema! Watakaoumia na Wanyarwanda!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Gharama ya kusafirisha mzigo toka Mombasa hadi Rwanda kisha ukalipia dola 152 tu ni Ghari sana kuliko Dsm hadi Rwanda kisha unalipia dola 500 Hilo ni janga kwa wafanyabiashara wa Mombasa ambao wanadhani wanaikomoa Tz kumbe wanajikomoa wenyewe hasa ukizingatia kwamba Rwanda ni kataifa kadogo sana lakini kenye Jeshi kubwa kuliko maelezo huku wakiligharamia kwa kuiba
 
Umenena vyema! Watakaoumia na Wanyarwanda!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Gharama ya kusafirisha mzigo toka Mombasa hadi Rwanda kisha ukalipia dola 152 tu ni Ghari sana kuliko Dsm hadi Rwanda kisha unalipia dola 500 Hilo ni janga kwa wafanyabiashara wa Mombasa ambao wanadhani wanaikomoa Tz kumbe wanajikomoa wenyewe hasa ukizingatia kwamba Rwanda ni kataifa kadogo sana lakini kenye Jeshi kubwa kuliko maelezo huku wakiligharamia kwa kuiba Mali za Congo sasa Wanaoma kimenuka wanachachawa ile mbaya
 
unajua kinachoendelea congo au unaota....congo haingii tena. Framework ya UN ni kupokonya silaha vikundi vyote vya waasi. Baada ya hapo akitia mguu huko ni agression to full scale war against rwanda. Kuweweseka kwake ni kwa sababu ya mkong'oto wanaoupata vibaraka wake M23 kutoka kwa majeshi ya drc na UN chini ya Brig General Mwaki wa TZ.

Bilashaka uko sahihi kinadharia kivitendo hapana.

Nitakupa mifano

Iraq imetulia?

Somalia imetulia?

Afghanstan imetulia?

Hebu tuambiane ukweli hawa UN hufanya mambo yao kwa malengo na kwa muda maalumu na kwa maana hiyo futa ndoto ya DRC kutulizwa kwa mkakati wa UN.

DRC itatulizwa na kutulia tu pale itakapopata kiongozi makini amabaye atajaaliwa na mungu kuwaunganisha wakongomani kwa ujumla wake basi.
 
Madikteta siku zote historia yao inafanana. Huwa wanasifiwa sana kwenye miaka ya mwanzo ya utawala wao. Mwishoni wanaharibu kila kitu. Wanyarwandwa wataungia katika dhiki kuu kwa sababu ya hasira za kagame.
 
mbona nasikia hata magari ya rwanda yaliyokuwa yanaingia TZ kuingiza mzigo na kutoa bandarini, mchezo ulikuwa ni huo huo labda ni kukomoana . kwenye gazeti la east african walilielezea ni problem ya muda mrefu . lakini rwanda atachemsha tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom