Wanabodi,
Kwa vile uchaguzi wa Zanzibar pia umesababisha vidonda na bado ni vibichi, damu bado haijakauka, hivyo naomba kuanza bandiko hili kwa a healing massage ya kuponya vidonda kwa kuungana na Watanzania wengine wote wapenda haki, amani na utulivu, kutoa pole kwa wahanga wa kilichotokea Zanzibar kwenye uchaguzi huu, ukiwemo umwakigaji damu, natoa pole kwa wote, na kama ni kweli kuna dhulma zozote zilizofanyika, then JAJI MKUU WA MAJAJI WOTE DUNIANI KWA KUTUMIA SHERIA KUU YA HAKI DUNIANI, THE LAW OF KARMA, will take care of this.
Sasa uchaguzi umeisha, life has to go on back to normal huku tukiendelea kuponya majeraha ya uchaguzi, pole sana kwa washindwa, na hongera kwa washindi.
Siasa za Zanzibar, natoa hongera kwa Dr. Hussein Mwinyi, kwa ushindi wa kishindo, cha kihistoria, haijapata kutokea toka Zanzibar izaliwe, ushindi wa zaidi ya asilimia 50%, siku zote uchaguzi wa Zanzibar matokeo huwa ni close range, lakini safari hii, ushindi wa 76% ni landslide ya funga kazi, na funga kalomo kwa vitimbakwiri vyenye maneno maneno kuhusu uchaguzi wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar yenye GNU, Maalim Seif Sharrif Hamad atakuwa Makamu wa I, wa rais, namshauri Maalim akubali uteuzi huo, kwa umri wake aliofikia, kipindi hiki kwake ni final finale, kwa uchaguzi wa 2025, kutahitajika damu changa, nashauri Jussa au Hamid apokee mikoba.
Japo kwa maoni yangu baada ya Dr. Mwinyi, mtu wa pili kwa u presidential material ni Prof. Mbarawa,
View attachment 1615747View attachment 1615748View attachment 1615749View attachment 1615750
Wanabodi, Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huwa na swali, na hoja, halafu jibu tulitoa wewe mwenyewe. Moja ya matatizo makubwa ya nchi yetu ni kutokuwa na kitu kinachoitwa succession plan kwenye urais wa nchini, hivyo mwaka wa uchaguzi ukifika, kila mtu...
Na rais Magufuli alimshauri Dr. Mwinyi kuchagua makamu toka Pemba, lakini kwa vile Makamu wa I ni Maalim Seif ni kutoka Pemba, then natoa wito kwa Dr. Mwinyi, amteue, Balozi Amina Salum Ally awe Makamu wa II, ili kutoa sare sare maua na makamu wa huku bara, Mama Samia Suluhu Hassan, tena sare ya Amina Salum Ally na Samia Suluhu Hassan, itakuwa ni sare inayoendana hadi macho!.
Nakuwekea picha 2, moja macho mawili na nyingine macho manne
Pasco
Rejea ya macho
Wana MMU, Salaam. Sisi binaadamu kila mtu ana kitu chake apendacho ndani ya moyo wake, na kila akikiona hicho apendacho, anakuwa roho kwatu!. Nina swali, inapotokea wewe unapenda macho, halafu kukatokea kuna kiongozi fulani mwanamke ana jicho hilo!, wewe unapenda jicho, ukimuona huyo mwenye...