Siasa zenye Chuki binafsi ni Sababu ya Vurugu na Vita

Siasa zenye Chuki binafsi ni Sababu ya Vurugu na Vita

EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Joined
Feb 2, 2015
Posts
150
Reaction score
84
Mtu yeyote anaweza kupata fursa nzuri na maendeleo. Zipo familia zilizo bahatika kuishi katika utajiri mkubwa.

Hiyo ni fursa ambayo wamejariwa. Changamoto ni kwamba wapo wanao amini kuwa umaskini walionao umesababishwa na matajiri waliopo.

Ndipo Watu hawa huwa na chuki dhidi ya matajiri. Na hii chuki ukiitazama kiundani utagundua kuwa inachochewa na wivu wa kwa nini awe nacho na mimi nisiwe nacho?

Hili kundi la Watu wenye chuki binafsi linapokuwa kubwa hushawishi wanasiasa kutafuta umaarufu kupitia hoja zenye nia mbaya. Binadamu wengi hawapendi kuona mtu mwingine akifanikiwa kumpita yeye.

Tunapoyalea makundi yenye chuki binafsi na wivu tuna hatarisha amani na usalama wa Watu wengine. Leo utakuta tunawashutumu watoto wa viongozi wa nchi pale wanapo ishi kifahari.

Sasa, kama familia ina mapato mazuri, vitega uchumi n.k Kuna ubaya gani kama wakitumia kilicho chao? Je hiyo nafasi ingekuwa ni yangu au ni yako je usingeitumia kuishi kifahari?

Walio bahatika wamebahatika si vizuri kuwatazama kwa jicho baya. Kama ni yao ni yao tu,chuki zako haziwezi kugeuza yao ikawa yako

Mwenyezi MUNGU akitaka upate nawe utapata. Tuache chuki ,kijicho ,roho mbaya ni chanzo cha migogoro na Vita.

Kama unahisi unaoibiwa na ushahidi unao, nenda mahakamani, chuki haijengi ila inabomoa taifa letu. Si kwamba hawapo matajiri wanyonyaji na mafisadi,wapo ila si wote, na kama unamjua nenda kashtaki tusieneze chuki hili ni taifa la wote, maskini na matajiri.
 
Mbona unalalamika,umekuwa mhanga wa hilo,🤔
 
Back
Top Bottom