sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Disemba 10, 2015 Magufuli wakati akitangaza Baraza lake la Mawaziri alimteua Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Katiba na Sheria nafasi aliyoishikilia mpaka 23 Machi 2017 alipobadilishiwa wizara na kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akijaza nafasi ya Bwana Nape Nnauye. Shule ya Sheria Tanzania (LST) ipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Malalamiko juu ya usahishaji wa mitihani na utoaji matokeo wa LST kuwa mbovu hayajaanza jana, ni ya muda mrefu toka tu shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 2008. Pindi alipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mwakyembe alikuwa akiisimamia shule hiyo na hata kufanya mazungumzo na watendaji wake hata hivyo hakuwahi kutoa uamuzi wowote juu ya mamalamiko hayo, tafsiri inayoweza kusemwa ni kuwa aliyapuuza. Mfano tarehe 22 Februari 2017 alitembelewa na makamu mkuu wa Chuo, Lukumay na viongozi wengine na kufanya mazungumzo wayajuayo wao ama labda walijitetea juu ya mamalamiko ya wanafunzi na akayaamini na kutochukua hatua, angalia hapa Law schoool wamtembelea dkt Mwakyembe ofisini kwake mjini Dodoma
Kumteua Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati itayochunguza malalamiko ambayo hakuyachukulia hatua ama ambayo aliyapuuza wakati wa uongozi wake wa Wizara sio jambo sawa. Kwanza tayari mtu huyu ana mgongano wa maslahi, maana anachunguza kitu ambacho anakijua tayari kwa kuwa malalamiko juu ya LST sio jambo jipya. Mheshimiwa Waziri Ndumbaro, tafadhali mteue mtu mwingine asiye na mgongano wa kimaslahi awe kiongozi wa kamati hiyo, Mwakyembe hastahili sio tu kuwa Mwenyekiti bali hata kuwa mjumbe wa kawaida wa Kamati hiyo.
Pichani ni Mwakyembe akiwa pamoja na Kina Lukumay ambao kimsingi ndio
wanaotuhumiwa kuonea