BALENSIAGA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2019
- 3,353
- 5,800
-ni kweli tuhuma za rushwa nimezisikia, kama wanavyosikia wengine.Jitihada zako za kuchomoa betri zinaonekana. Umesahau kuwa ni wewe ulisema tuhuma za rushwa huzijui. Kumbe na wewe umekuwa ukizisikia? Hukuwa umeonyesha Hilo awali.
Kwamba kuna mitihani migumu inatungwa kuliko uwezo wa wanafunzi? Hii ni hoja yako mpya kabisa kuwahi kuisikia. Umeipata wapi wewe hoja hii? Kumbuka nimejaribu kuainisha wazi wazi tatizo na hata ufumbuzi wake.
"Pana tatizo la utahini. Ufumbuzi pande tatu ziwe tofauti. Yaani mtahiniwa, mtunga mtihani na msahihishaji. Mtunga mtihani asiwe msahishaji na asiwe mwalimu husika wa somo. Kama ilivyo kwa shule za msingi na secondary ambako masomo na mitihani ni kwa mujibu wa syllabus."
Kwamba takwimu zilipaswa kuwa je?
Haupo mtihani ambao matokeo yake hayafuati formula ya normal distribution na yakawa halali:
View attachment 2381370
Kwa utaratibu huu takwimu zingekuwa hivi:
View attachment 2381372
Ambako idadi ya DISCO ingekuwa takribani sawa na idadi ya walio perform with distinction au first class.
Mfano angalau ingekuwa hivi:
Wenye distinction au first class 3
DISCO 4
supp 26
Pass 600
Ni aibu kuwa malengo mazuri yaliyokuwapo ya kuwa na TLS yamegeuzwa siasa na sasa chuo ni kijiwe cha ndugu waliojiapiza kuwafelisha wahitimu waliofaulu vyuo vikuu kwa starehe zao.
Kwa uhalali upi? Au kwa ugumu upi wa sheria?
-ni kweli kuna mitihani inakuwa migumu kuliko uwezo wa mwanafunzi na hii ndio sababu inayochangia watu kufeli, mfano mdogo wangu alifanya supp ya somo la Ethics anadai waliofaulu hilo somo hawazidi 50 out of 700, inaonekana pale LST kuna baadhi ya mitihani ni migumu kupita kiasi hata hao wenye PhD wanafeli
-huo mfumo unaotaka utumike kama wa secondary kwa kweli utasubiri sana hadi wakubali, cha muhimu mkuu ni kupambana tu, mdogo wangu alikuwa na Supp nyingi tu akapambana hadi akamaliza
-yaani supp 600, disco 4 na fest sitting 3 hiki kitu hakiwezekani, kwa maana nyingine unataka Law School iwe ni Shule ya Kupitisha Watu kirahisi rahisi hapana haikubaliki kabisa, huku ni kushusha Viwango Na heshima ya Uwakili
-halafu usichanganye TLS na LST inaonekana hauko makini
-kuhusu kusema ni kijiwe cha ndugu waliojiapiza kufelisha watu hii hoja ina walakini, kwa sababu Mwezi wa 7 kuna Mawakili 300 wameapishwa, hao 300 wametoka wapi,kama sio kupambana na shule?.