Kwa hakika hii nchi ni ngumu sana. Mambo yote hata yasiyopaswa yamegeuzwa kuwa siasa siasa tu.
Hili la law school nalo kwa hakika ni shida.
Examination Results
Hiyo ni "site' yenye matokeo yaliyotoka tangia jumatano 5/10 lakini hayafunguki.
Waliofeli, watatakiwa kwenye supplementary zitakazoanza jumatatu 10/10.
"Watajua vipi wanafunzi waliofeli kuwa wamefeli na kujiandaa tokea kokote waliko Tanzania, kufika kwenye mtihani Dar kwa wakati?"
Hayupo anayejali ila kukusanya pesa za ada tu.
Mass failures ni jambo la kawaida kwenye chuo hiki. Takwimu zinaonyesha si nadra wanafunzi 30 tu kufaulu baina ya wanafunzi 400. Kwa uhalali upi?
Wanafunzi hawa huwa ni wahitimu wa shahada za kwanza, wengine wakiwa na shahada za uzamili na hata za uzamivu. Walimu Law School ni hawa hawa wanaofundisha UDSM na vyuo vingine.
"Iweje wanafunzi hao kufeli law school wanapokuja kusoma kwa mwaka mmoja tu, kwa walimu hao hao?"
Mazingira wezeshi kabisa kwenye zile rushwa zetu pendwa za ngono na mauzo batili ya notes.
"Iweje kitabu 'original' kilichoandikwa na mwalimu husika kuruhisiwa kuingia nacho kwenye mtihani, lakini siyo photocopy ya kitabu hicho hicho?"
Kwa hakika kuna mengi ya kuangaliwa kwenye vyuo hivi vinavyoendeshwa na walimu miungu watu.