Watu wanahangaika kusomesha wanafunzi miaka 4 ya chuo kikuu LLB na mwaka mmoja huko LST halafu ada zao zinatupwa kwa elimu ya kijana kuishia hapo LST kwa kukwamisha kimakusudi na walimu wa taasisi hiyo, wanaendelea kunyonya ada za wanafunzi kwa kuwadiskosha makusudi, wanaendelea kuneemeka kwa ada za supplementary ambapo kila component hulipiwa Tshs. 30,000/= yaani kwa somo moja tu, LST huweza kuingiza zaidi ya milioni 11 kwa siku moja (masaa 3) tu, sasa kwa masomo karibu 10 wanaingiza kiasi gani? Na hapo ni somo, ukisema uchambue kwa component maana yake somo moja lina component 3, kwa hiyo mtu analipa elfu 90 kwa somo zima, sasa kwa wanafunzi 400 waliosupp hawa LST wanapata kiasi gani? Na hizi ada ndio chanzo chao kikuu cha mapato kwa mujibu wa Fact and Figures report ya 2018/2019 iliyotolewa nao LST, inapatikana hapa
Facts and Figures 2019
Sasa kwa nini isiaminiwe kuwa wanafelisha sana wanafunzi ili LST wapate mapato kupitia ada za masomo na supplementary??
Mkuu, hii taasisi ni ya kifisadi kabisa na kama ulivyoeleza madhara ya ufelishaji wao hovyo wanafunzi ni makubwa kwani sio kwa watu binafsi tu bali kwa Taifa zima, unapozalisha majobless wenye taaluma, hasara ni kwa Taifa, cha ajabu Mkaguzi Mkuu wa Serikali hajawahi kutoa ripoti ya ukaguzi kwa hii taasisi inayojiita ya serikali huku kihalisia ni ya watu binafsi wachache.
Hebu angalia hapa, kwa mujibu wa Fact and Figures yao ya 2019, inaonesha LST walikuwa na watumishi 52, huku walimu wakiwa ni 11 na 41 wakiwa ni wasio walimu (utawala). Sasa hawa watumishi wanalipwa mishahara kwa mwaka kiasi cha Tshs. 1,321,523,820.97 ambapo kwa mwezi ni kiasi cha Tshs. 2,117,826.64 (flat rate) kwa kila mwalimu. Fedha hii haitoki serikalini bali ni katika ada za wanafunzi, hapo fedha za supplementary, statement za matokeo, rufaa nk hazijaoneshwa hesabu yake zinatumika vipi. Na ni kwa nini kama chuo ni cha serikali, mishahara ya walimu itokane na ada za wanafunzi na sio kapu kuu la serikali?? Hamuoni kuwa kufanya ada kama chanzo cha mapato ya kulipa mishahara ni mwanya wa wazi wa kutengeneza 'vipindi' ili mishahara ipatikane?? Ni wazi wanafunzi wanafelishwa ili warudie kusoma na mishahara ipatikane kupitia ada zao. Tunaomba Serikali hii hii ingilie kati, uchunguzi ufanyike kwenye matokeo ya wanafunzi na tuhuma za rushwa. Hali ni mbaya, kweli mwalimu anaharibu future ya mwanafunzi kwa sababu tu apate mshahara?? Kweli
Hiyo fact and figures ni kama inavyojieleza hapa kwenye kielelezo.