Sidhani kama bado kuna watu wanaamini tena eti kufanya kazi kwa bidii pekee huleta maisha bora

Sidhani kama bado kuna watu wanaamini tena eti kufanya kazi kwa bidii pekee huleta maisha bora

Ukiacha Mafisadi, Hakuna Mwenye mafanikio asie kua na bidii, HAYUPO.

Angalia Field zote za Maisha Utakuata watu wote walio fanikiwa kwenye field zao wana bidii sana ya wanacho kifanya.

Mimi nakutajia Baadhi ya wanotembea/Walio tembea na bidii
1.Millard ayo
2.Diamond
3.Lissu
4.Mo dewji
5.JPM
 
Inategemea ni kwenye jambo gani, sasa wewe jichanganye
 
Dhana ya bidii kuwa ndio huleta mafanikio ni sawa na shuhuda za miujiza makanisani au shuhuda za wale washindi wa michezo ya bahati.
Hakika mkuu

Au kuwepo na majini wazuri😜
 
Kwa Tanzania na nchi nyingi Afrika hu msemo unawafaa zaidi watu waliojiajiri.

Kama umeajiriwa unajisumbua tu, mshahara utabaki kuwa pale pale, ndio maana watu makazini wanapiga stori na wanazurura sana huwakuti ofisini. wanaopandishwa vyeo wengi ni machawa, wanaotoa rushwa, ndugu na wale wenye msaada kwenye kupiga dili.
 
Ni msemo unaowafaa zaidi watu waliojiajiri

Kama umeajiriwa unajisumbua tu, mshahara utabaki kuwa pale pale, ndio maana watu makazini wanapiga stori na wanazurura sana huwakuti ofisini. wanaopandishwa vyeo wengi ni machawa, wanaotoa rushwa, ndugu na wale wenye msaada kwenye kupiga dili.
☹️☹️
 
Kuna wakati bidii iliheshimika, ilikuwa valued katika level ya dhahabu na almasi.

Kuna wakati bidii ilikuletea tumaini la kubadirisha maisha na hakika baada ya muda fulani bidii ilikufanya ufurahie kile maisha ilicho ki-offer.

Baada ya dunia kupitia recession, rasilimali muhimu kuwekwa chini ya vikundi vichache maalum, baada ya soko la ajira kuwa siasa-fied, umuhimu wa mtu kuwa substitute ya teknolojia, uchawa kuwa glorified, makalio makubwa kuzidi akili etc imepelekea juhudi kuwa kituko duniani.

Maisha bora tena hayako guaranteed na ubidii au unyenyekevu wako ila pale utakapobahatika kula samahani moja na waendesha usukani.

++JASUSI COHEN++
kwa mm siamini mtu anaefurahia ajira
 
Huwezi kusema utasukuma mkokoteni kwa bidii ufanikiwe, kuna kazi ukifanya kwa bidii utafanikiwa kuna nyingine hata ufanye kwa bidii jinsi gani mafanikio utayasikia tu kwenye bomba. Lakini inategemea na nchi na nyakati pia, nchi kama Marekani, Israel, za Ulaya, China, Canada, Japan, Korea Kusini na nyingine za aina hiyo zinazoegemea merits zaidi bidii ni muhimu katika mafanikio.
 
Back
Top Bottom