Sielewi Kigwangalla anataka kuonesha nini kati ya Tanzania ya Magufuli VS Tanzania ya Nyerere!

Kigwa ameomba zama za Magufuli zisifananishwe na za Nyerere sababu Nyerere hawezi fanana na mtu mwingine kama alivyo Magufuli.... na tunayemuombolezea sasa ni Magufuli na sio Nyerere

Kila mtu ni unique ndio maana hata sasa mtu akitaka Samia afanane na Magufuli haitakua rahisi. Tunaangalia malengo na jinsi yanavyofikiwa
Impressive!

Lakini Kigwa, kama walivyo watu wengi, sio pekee amefanya hivi, hupenda kulinganisha watu.
Nina hakika hili sio geni kwako, na kampeni ilishaanza hapa hapa nyumbani siku za nyuma kidogo za kufananisha.

Kwa hiyo. Kigwa sio mvumbuzi wa hili.

Ni wazi watu hawawezi wakafanana kwa mengi, lakini kuna mambo muhimu wanayoyasimamia yanaweza yakafanana ila kiutekelezaji kukawa tofauti.

Mfano: Kiujumla, mimi nadhani Magufuli kwa kweli alikuwa anaitakia mema sana Tanzania, bila shaka yoyote kama alivyoitakia mema Mwalimu Nyerere.

Katika kutekeleza mambo mbalimbali ya kuifanya Tanzania iwe ya neema, hapo bila shaka yoyote kuna tofauti kubwa kati yao kutokana na utofauti wao kama binaadam wawili wasioweza kuwa sawasawa kwa kila kitu, hata wakiwa mapacha (identical twins).

Huu ni mfano mmoja kati ya mingi ya kuzielezea tofauti zao; tena zinazowatofautisha sana sana.
 
Kama hana uwezo wa kuunda na kuunganisha maneno yakaleta maana anayoitarajia ndio hajui hivyo!!
Hapana mkuu.

Simtetei, najua ni mmoja kati ya 'opportunists' wengi ndani ya chama, lakini siamini kuwa kutoweza kujieleza ipasavyo kwa sababu tu za kuvuruga (confuse) watu ili kulinda maslahi ni "kutojua".
 
Impressive!

Lakini Kigwa, kama walivyo watu wengi, sio pekee amefanya hivi, hupenda kulinganisha watu.
Nina hakika hili sio geni kwako, na kampeni ilishaanza hapa hapa nyumbani siku za nyuma kidogo za kufananisha.

Kwa hiyo. Kigwa sio mvumbuzi wa hili.

Ni wazi watu hawawezi wakafanana kwa mengi, lakini kuna mambo muhimu wanayoyasimamia yanaweza yakafanana ila kiutekelezaji kukawa tofauti.

Mfano: Kiujumla, mimi nadhani Magufuli kwa kweli alikuwa anaitakia mema sana Tanzania, bila shaka yoyote kama alivyoitakia mema Mwalimu Nyerere.

Katika kutekeleza mambo mbalimbali ya kuifanya Tanzania iwe ya neema, hapo bila shaka yoyote kuna tofauti kubwa kati yao kutokana na utofauti wao kama binaadam wawili wasioweza kuwa sawasawa kwa kila kitu, hata wakiwa mapacha (identical twins).

Huu ni mfano mmoja kati ya mingi ya kuzielezea tofauti zao; tena zinazowatofautisha sana sana.
Nashukuru sana Mkuu!

Kile ulichojaribu kukielezea wewe kipo tofauti nahisi na kile Kigwa amejaribu kukiwakilisha yeye dhahiri kweupe inaonyesha anaamin Magufuli alikua Bora than Nyerere
Ila nikushukuru umejaribu kuleta ufafanuzi mzuri wako kama wewe
 
Back
Top Bottom