Pigania katiba mpya itakayokupa fursa ya kuchagua mkuu wako wa mkoa kwa kura yako mwenyewe badala ya kuteuliwa Bashite au Sabaya.
Mkuu 'Yoda', kukwambia ukweli bila kukuficha lolote, uamini wangu umekwishapita hatua hiyo ya kuitegemea Katiba kuwa mwarobaini wa matatizo yetu.
Hapana, sisemi hapa kwamba Katiba mpya ni muhimu, tena sana, lakini katiba hiyo haiwezi kuondoa matatizo chungu nzima tunayoyapata sasa hivi katika kutafuta njia za kutuondoa kwenye umaskini huu. Si unaona pale kwa majirani zetu, hapo kaskazini wanavyohangaika hata baada ya kupata katiba wanayojigamba nayo kwamba ni nzuri sana, pamoja na kwamba wamenakiri tu sehemu mbalimbali. Wanao maseneta na magavana, lakini mikoroganyo yao ipo palepale, kama ndiyo haikukorea kabisa!
Magufuli alikuwa na masinema sinema mengi mno yaliyovuruga utawala wake kwa kiasi kikubwa, lakini angesimamia yale ya ujenzi wa nchi bila ya mizengwe hiyo ya pembeni, sina shaka hata pamoja na uwepo wa katiba hii mbovu, hali ya nchi yetu ingebadilika.
Huo ni mfano mmoja.
Hizi nchi tunazopewa kama mifano ya nchi zilizoweza kujitoa kwenye umaskini katika muda mfupi, nchi kama Malaysia, Singapore, na kwingineko, hivi katiba zao ndizo zilizoleta mabadiliko makubwa kiasi kile kwa muda mfupi? Hili ni swali, kwa sababu sijui jibu lake.
Tulipopata uhuru hapo 1961, Tanganyika ilikuwa chini sana. Hatukuwa hata na watumishi wa kuendesha serikali yetu kikamilifu. Pamoja na matatizo mengi, baadhi yake yakiwa nje ya uwezo wa nchi mojamoja (matatizo ya dunia), lakini tuliweza kujikongoja; watu wetu wakasoma, tukawa na watu wetu wa kutosha katika maeneo mengi ya mahitaji yetu. Wengi hawataki kusema, lakini ukweli ni kwamba tulipiga hatua sana kwenda mbele pamoja na kuwepo kwa changamoto zote zile.
Sasa basi, hatuwa tuliyoifikia sasa hivi ndiyo muhimu kabisa (threshold, critical point) ya kutunyanyua ili ionekane wazi kwamba tunaendelea.
Kinachotakiwa ni kuwepo kwa viongozi, hasa huyo mkuu kabisa mwenye kuona dira ya mwenendo wa taifa hili na kuifuata dira hiyo ili tunyanyuke.
Lakini badala yake, haya yanayoonekana sasa hivi ni kama tunazungukia tu humohumo bila ya kujuwa tunataka kwenda wapi!
Katiba mpya haiwezi kuleta kiongozi mwenye maono sahihi.
Haya ni mawazo yangu. Nimeona niyamwage kwako, kwa sababu nakuheshimu.