Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Ondoa hiyo kila ....mmoja wetu
Mkuu, mpaka Watanzania wasio CCM wala NCCR watazipata neema. Watanzania wa wilaya ya Hai sasa watapata neema kwa kufanya biashara zao bila bughudha.

Hii ni kwa sababu Mama ni kiongozi msikivu na mwenye upendo kwa anaowaongoza. Malalamiko juu ya DC yule yalianza kitambo sana. Leo umeona hatua za kijasiri alizozichkua Mama???

Neema zitamfikia kila mmoja wetu kwa wakati.
 
Defence ikizidi tutaanza mgeuka hata tunaomsupport.
Aachwe kivipi? Challenge ni lazima.
Mlisema jiwe aachwe - yaliyotokea wote tunayajua. Hii kuachwa,,, hapana,, akitoka kwenye mstari lazima akumbushwe. La sivyo tutatengeneza dikteta mwingine soon.
Mimi sikuwahi kusema jiwe aachwe. Jiwe tulimjua na kashfa zake za wizara ya ujenzi na mifumo yake ya uendeshaji wa ofisi anazozisimamia.

Mama mpaka anaingia madarakani hakuwa na kashfa kabisa.

Nakubaliana nawe mkuu, challenges ni lazima na zinatakiwa ziwepo ili uweze ku-perform vizuri zaidi. Tunachokisema tu ni kwamba Mheshimiwa rais awe challenged kwa staha na heshima.

Ni kweli akitoka kwenye mstari ni lazima akumbushwe.

Tatizo unalikuta jitu linasema Mama tangu aingie madarakani hakuna alilolifanya, sasa huoni kama watu aina hii inabidi tuwasaidie kuwaonyesha mama alilolifanya???
 
Hilo lilikuwa ni kosa kubwa la JPM maskini! Hakumjua RA vyema maskini ya mungu. Bye
See????

Yaani JPM aliekuwa kwenye system for more than 20 years before he became a president asimjue Rostam vizuri ila wewe mchimba chumvi ndio umjue Rostam vizuri???

You are a very small mind. You know nothing about administration. You know nothing about "giving in" in administration.

Tuachie kelele zako na kutuletea hoja zako za kiwehuwehu
 
Defence ikizidi tutaanza mgeuka hata tunaomsupport.
Aachwe kivipi? Challenge ni lazima.
Mlisema jiwe aachwe - yaliyotokea wote tunayajua. Hii kuachwa,,, hapana,, akitoka kwenye mstari lazima akumbushwe. La sivyo tutatengeneza dikteta mwingine soon.
Mungu hawezi kuumba watu wawili wendawazimu watutawale kwa kupokezana. Mwendazake ilikuwa ni ajali. Mungu bado anaipenda nchi yetu Tanzania ametupatia Rais msikivu, mwenye hekima na mwenye upeo/ uelewa, SSH.

Tmuombe tu atuachie Katiba ya Rasimu ya Warioba
 
kiasi kwamba watu wale wale, tena walio na rekodi mbaya katika utumishi wao ndio waendelee kuteuliwa?
Ukosefu wa demokrasia miaka 5 ya muovu dikteta jiwe haikutoa fursa kwa wanasiasa wapya kuonesha vipaji vyao. Ndiyo maana watu wanaojulikana vipaji vyao ni wale wa enzi ya Kikwete.

Madhara ya kuongozwa na mwendazake ndiyo tunayaona
 
Hivi sisi waswahili tuna tatizo gani lakini? kwa nini tunaona kwamba kuna watu fulani wanastahili kupewa fursa za uongozi hata wafanye madhambi ya ajabu kiasi gani? Ina maana hapa nchini suala la uongozi kuna watu wanaostahili na wengine wasiostahili?

Mtu anafanya makosa makubwa katika nafasi fulani, anaondolewa, anapumzishwa na baada ya muda fulani anateuliwa tena katika nafasi nyingine ya uongozi. Au utakuta mtu anaharibu sana katika sehemu moja, badala ya kuwajibishwa anahamishiwa sehemu nyingine.

Imekuwa kawaida sasa kusikia Raisi, au Waziri Mkuu au Waziri wakisema kwamba mtu fulani ameharibu sana hapa. Arudishwe wizarani akapangiwe kazi nyingine. Au Raisi kamtumbua mtu fulani, atapangiwa kazi nyingine. Ina maana apewe nafasi ya kuharibu sehemu nyingine? Hivi ina maana kuna watu ambao wanapewa hati miliki za uongozi? Na wengine hawastahili?

Kwa mfano, watu walilalamika kuhusu tabia za baadhi ya wakuu wa mikoa, kuhusu dharau zao, lugha zao, pamoja na Chalamila, lakini hawakusikilizwa. Kweli ilibidi Raisi Samia asubiri hadi na yeye awe mhanga wa lugha zisizofaa ndio achukue hatua? Kwa nini alipoambiwa hakutaka kusikiliza?

Kuna mkuu wa mkoa mwingine ambae alichakachua msaada wa seikali, Jakaya Kikwete akakasirika na kumwondoa kwenye nafasi yake. Leo Raisi Samia anaamua kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa. Hatuna watu wengine Tanzania wanaoweza kuwa wakuu wa mkoa bali yeye tu?
Wewe ni mmbea. Taja jina wacha majungu
 
Mungu hawezi kuumba watu wawili wendawazimu watutawale kwa kupokezana. Mwendazake ilikuwa ni ajali. Mungu bado anaipenda nchi yetu Tanzania ametupatia Rais msikivu, mwenye hekima na mwenye upeo/ uelewa, SSH.

Tmuombe tu atuachie Katiba ya Rasimu ya Warioba
Na haya ndiyo maombi yetu.

Na mama ameshatuskia na analifanyia kazi hili.

Nawasihi Watanzania wenzangu, hili jambo la katiba utekelezaji wake unachkua muda kidogo. Maandalizi na umakini wa hali ya juu.

Nawaomba sana kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Hivi kwa nini haitwi Balozi Batilda Buriani?Au unaweza kuwa umewahi kuwa Balozi nchi fulani na bado ukawa huna hiyo salutation ya ubalozi?
Kiranga
 
Hii ndio kawaida mnapokosa hoja. Whenever you see people speculating about others, just know they are small minds. Haihitaji kuambiwa, wewe jua tu kwamba you are a loser!

How can you start discussing people?? You are talking about Batilda na boys to men as if you know them. Discuss idea, stop discussing people as haisaidii. Mama Batilda is now RC Tabora na wewe na kumjadili kwako haitomfanya now asiwe RC. Mheshimiwa Rais kamteua kamuamini na atafanya kazi aliotumwa. Nyinyi endeleeni kuuliza maswali.

Mmekaa kwa wivu na fitna na majungu mnaombea watu mabaya. Eti Mungu yupo, ni lini Mungu alikuwa hayupo?? Halafu mnafanya kama Mungu ni wenu peke yenu. Losers! Mungu ni wa Mama Samia na Madam Batilda pia.

Na just so you know, kazi inaendelea wewe endelea kulalama.
Mambo ya Dr Batilda yameingiaje? Kubali hujui hii nchi inaendaje
 
See????

Yaani JPM aliekuwa kwenye system for more than 20 years before he became a president asimjue Rostam vizuri ila wewe mchimba chumvi ndio umjue Rostam vizuri???

You are a very small mind. You know nothing about administration. You know nothing about "giving in" in administration.

Tuachie kelele zako na kutuletea hoja zako za kiwehuwehu
Hujui kitu ndo maana unaingiza masuala ambayo sijawahi na siwezi kumsema Dr Batilda. Masuala ya kuwa mkuu wa mkoa ni small issue to me. Mie naongelea masuala ya uendeshaji nchi. Kama humjui RA basi wewe ni amateur au ni mahaba ya watu fulani fulani.
 
Umesema kweli na mifano iko mingi, si ya kutafuta wala kutajiwa. Wanasiasa wa kitanzania wote wanaunganishwa na kitu kimoja: maslahi binafsi. Haya mengine ya kusema sijui kutumikia wananchi ni bla bla tu. Ni sahihi kusema kabisa kuwa ni kama kikundi cha matapeli au wahalifu. Hawatupani.
Wanasiasa wa tz hasa ccm ni kama walikulia familia moja au walisoma shule moja. Ni waarabu wa pemba hutambuana kwa vilemba vyao.
Wanabebana tu. Raisi akisema hebu nipeni watu wanaofaa udc au afisa wa tawala wanaompa majina yao wanarudi mle kwenye kundi lao.
Ndege wa aina moja huruka pamoja. Kwa kila kitu watapeana; tenda, teuzi, kazi, vyeo, ulaji nk.
Hata kama raisi hajui wanasema wanapeana 'pande' kwa hiyo wakati mwingine rais huweza kuingia mkenge.
Uzalendo mdomoni kushiba tumboni vitambi si mwaviona? vitambi si matumbo tu haaa na hizo mali pia, ndio huitwa uboss.
 
Team JK imerudi kwa kasi, lakini matumaini ni kwamba hao wanaorudishwa hawatarudi na madudu ya awamu ile.

Matumaini ni Rais Samia kuwa na sauti, maana inakuwa haina faida kwa taifa kama wanarudishwa wanamtandao halafu wakarudi na akili zile zile za wakati ule.
Ki ukweli sio timu JK bali timu ulaji
 
Nimekumbuka uandishi wa gwiji wa kiswahili Seif Khatibu(RIP). "Walaji hupendwa sana na tuhuma zikizidi huamishiwa kwa Jana na akale kwa juhudi"
hii ndiyo desturi ya viongozi wengi kutoka chama like.
 
Pigania katiba mpya itakayokupa fursa ya kuchagua mkuu wako wa mkoa kwa kura yako mwenyewe badala ya kuteuliwa Bashite au Sabaya.
Mkuu 'Yoda', kukwambia ukweli bila kukuficha lolote, uamini wangu umekwishapita hatua hiyo ya kuitegemea Katiba kuwa mwarobaini wa matatizo yetu.
Hapana, sisemi hapa kwamba Katiba mpya ni muhimu, tena sana, lakini katiba hiyo haiwezi kuondoa matatizo chungu nzima tunayoyapata sasa hivi katika kutafuta njia za kutuondoa kwenye umaskini huu. Si unaona pale kwa majirani zetu, hapo kaskazini wanavyohangaika hata baada ya kupata katiba wanayojigamba nayo kwamba ni nzuri sana, pamoja na kwamba wamenakiri tu sehemu mbalimbali. Wanao maseneta na magavana, lakini mikoroganyo yao ipo palepale, kama ndiyo haikukorea kabisa!

Magufuli alikuwa na masinema sinema mengi mno yaliyovuruga utawala wake kwa kiasi kikubwa, lakini angesimamia yale ya ujenzi wa nchi bila ya mizengwe hiyo ya pembeni, sina shaka hata pamoja na uwepo wa katiba hii mbovu, hali ya nchi yetu ingebadilika.

Huo ni mfano mmoja.

Hizi nchi tunazopewa kama mifano ya nchi zilizoweza kujitoa kwenye umaskini katika muda mfupi, nchi kama Malaysia, Singapore, na kwingineko, hivi katiba zao ndizo zilizoleta mabadiliko makubwa kiasi kile kwa muda mfupi? Hili ni swali, kwa sababu sijui jibu lake.

Tulipopata uhuru hapo 1961, Tanganyika ilikuwa chini sana. Hatukuwa hata na watumishi wa kuendesha serikali yetu kikamilifu. Pamoja na matatizo mengi, baadhi yake yakiwa nje ya uwezo wa nchi mojamoja (matatizo ya dunia), lakini tuliweza kujikongoja; watu wetu wakasoma, tukawa na watu wetu wa kutosha katika maeneo mengi ya mahitaji yetu. Wengi hawataki kusema, lakini ukweli ni kwamba tulipiga hatua sana kwenda mbele pamoja na kuwepo kwa changamoto zote zile.

Sasa basi, hatuwa tuliyoifikia sasa hivi ndiyo muhimu kabisa (threshold, critical point) ya kutunyanyua ili ionekane wazi kwamba tunaendelea.
Kinachotakiwa ni kuwepo kwa viongozi, hasa huyo mkuu kabisa mwenye kuona dira ya mwenendo wa taifa hili na kuifuata dira hiyo ili tunyanyuke.

Lakini badala yake, haya yanayoonekana sasa hivi ni kama tunazungukia tu humohumo bila ya kujuwa tunataka kwenda wapi!

Katiba mpya haiwezi kuleta kiongozi mwenye maono sahihi.

Haya ni mawazo yangu. Nimeona niyamwage kwako, kwa sababu nakuheshimu.
 
Kama unashindwa kuona mpaka Leo kwa macho yako mwenyewe ni lipi haswa sisi tunaweza kukuonyesha??

Umesikia huko Kwamba vyombo vya habari vilivyofungiwa vyote vimefunguliwa?

Nchi hii ilikuwa inaliwa kimya kimya na genge flani la watu waliokuwa wakijifanya ndio wazalendo, unazo habari kwamba mama amewatimua wote ikulu mmoja baada ya mwengine. Au unadhani kulitoa lile genge ikulu ni kazi rahisi?? Hilo genge ndio lilikuwa linaenda kuandaa mtu wao wa kuchukua madaraka 2025 mpaka 2035. Kufikia 2035 wewe ungekuwa na miaka 55 au 60 na habari yako ingekuwa imekwisha. Mshukuru sana Mama mkuu.
Wewe unaeleweka toka ulipoweka lile bango lako hapa.
Kwa hiyo huwezi kuona kingine mbali ya u'sycophant' unaokusukuma.
 
Ni kama tunajidanganya kuwa nchi hii ni yetu (watanzania) wote. Ukiangalia kwa kina utaona sisi wengine (achana na wanaostahili teuzi na kuhamahama nafasi) ni kama wahamiaji ila tu hatuitwi haramu. Hatustahili kupata nafasi yoyote ya kimaamuzi zaidi ya kupangiwa utaratibu wa maisha na tabaka lilelile la miaka na miaka. Keki ya Taifa si ya wote, ni sisi tu ndio tunaoambiwa kuwa tujiulize tumeifanyia nini nchi yetu, sasa hili swali linastahili kusomwa kimasikitiko, hivi tumeifanyia nini nchi yetu mpaka tunapuuzwa hivi?
Sajo, nimekusoma mkuu.

Haya uliyoandika hapa ndicho kitendawili kikuu cha nchi yetu. Nchi imekuwa ya watawala, sisi wengine tumekuwa wasindikizaji tusiokuwa na sauti yoyote katika mambo yanayotuhusu!

Kwa nini iwe hivyo?

Kwa nini tunakosa uwezo wa kuibadilisha hali hiyo?
 
Back
Top Bottom