Sifa za makabila mbalimbali hapa Tanzania

Uliowataja sio machifu wa Kizaramo
 
Makabila ya kusini yale yote ni wakarimu na wapole.. hawabaguani hata kidogo.. hufurahi muda wote na hao ndio huchangamsha jiji la Dar..
 
Wapare ni wabahili pia wana roho mbaya, kuna siku nlikutana na mdada kwenye bus, akawa ananipa story ya shoga ake anamfanyia visa, anafanya mambo kwa binafsi n.k n.k nikamuuliza rafiki ako ni mpare? Akajibu ndio... Nilicheka, Wapare wana roho mbaya
big up Evelyn Salt umeutendea haki huu uzi. inasemekana asilimia kubwa ya wapare wanaume kwa wanawake utulivu kwenye mahusiano ni sifuri, hili lina ukweli?
 
Wagogo- ni wakarimu sana, wapole, wachapa kazi, hawapendi makuu, ni wazalendo karibuni Dodoma.

Kwa sasa nipo kijijini Chilonwa.
 
Bashite kweli anawakilisha wa Misungwi, kwa kina Bashite ni kijiji cha Kolomije.
 
Haya ndio Makabila 125 ya TANZANIA

Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani.

Waalagwa, (Wasi)
Waakiek,Waarusha,Waassa,Wabarabaig ( Wamang'ati)
Wabembe,Wabena,WabendeWabondei,Wabungu (Wawungu),Waburunge,Wachagga,Wadatoga,Wadhaiso,WadigoWadoe,Wafipa,Wagogo,Wagorowa (Wafiome)
Wagweno,Waha,Wahadzabe (Wahadza) na Watindiga,Wahangaza,WahayaWahehe,Waikizu,Waikoma, Wairaqw( Wambulu),
Waisanzu,Wajiji,Wajita,Wakabwa,Wakaguru,Wakahe,Wakami,Wakara(Waregi)Wakerewe,
Wakimbu,Wakinga,Wakisankasa,Wakisi,Wakonongo Wakuria,Wakutu,Wakw'adza,WakwaviWakwaya,Wakwere ( Wanghwele)Wakwifa,
Walambya,Waluguru,Waluo,Wamaasai,WamachingaWamagoma,Wamakonde,Wamakua (Wamakhuwa) Wamakwe ( Wamaraba) Wamalila,Wamambwe,Wamanda Wamatengo,Wamatumbi,
Wamaviha Wambugwe,Wambunga,WamosiroWampoto,Wamwanga,Wamwera Wandali,Wandamba,Wandendeule,Wandengereko,Wandonde,Wangasa,Wangindo,Wangoni, Wangulu,Wangurimi ( Wangoreme),Wanilamba,(Wanyiramba)
Wanindi,Wanyakyusa, Wanyambo,Wanyamwanga, Wanyamwezi,
Wanyanyembe,Wanyaturu ( Warimi) Wanyiha,Wapangwa,Wapare ( Wasu),Wapimbwe,Wapogolo,Warangi (Walangi) Warufiji,Warungi,Warungu (Walungu),Warungwa,Warwa, Wasafwa,Wasagara,Wasandawe,Wasangu,Wasegeju, Washambaa, Washubi Wasizaki,Wasuba,Wasukuma Wasumbwa,Waswahili,Watemi Wasonjo,Watongwe,Watubuka,Wavidunda,Wavinza,Wawanda,Wawanji,Waware,Wayao,Wazanaki,WazaramoWazigula Wazinza, Wazyoba.

Je, kabila gani halija tajwa hapo ?
 
Huo uchapakazi wameanza lini??? Wagogo ni wavivu wa kutupa si wanaume si wanawake ni wavivu mnooo
Akutukanaye hakuchagulii tusi.

Wagogo ni wachapa kazi sana hasa kilimo na ufugaji. Changamoto tuliyonayo ni uhaba wa mvua mara kadhaa. Tunaomba serikali iongeze fungu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…