Mbunge wa Viti Maalum mkoani Njombe kupitia chama cha CHAUMMA, Sigrada Wilhem Mligo, amefunguka kuhusu changamoto zinazovikabili vyama vya upinzani nchini, akidai kuwa kuna njama za makusudi zinazofanywa na serikali ili kuvigawa na kuvidhoofisha vyama hivyo.
Amesema hayo katika mahojiano yaliyorushwa Julai 5, 2026 na Nijuze, akijibu swali kuhusu yanayoendelea ndani ya CHAUMMA ambapo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu kuondolewa kwenye nyadhifa hiyo kwa tuhuma za kujichukulia mamlaka ya Mwenyekiti wa chama hicho.