Siheshimiwi mtaani kwa sababu sijaoa

Siheshimiwi mtaani kwa sababu sijaoa

Jamani najikuta nawaza sana hivi nitatoa lini? Mbona mda unazidi kusonga? Shauku ya kuoa unakuja mara inapotea, ukimpata unaempenda changamoto inakuwa kiuchumi unakuwa hauko vizuri, ukiwa vizuri kiuchumi wakimuona humuoni jamani mpaka inafikia hatua nawaza nini kinanisibu au kuna mkono wa mtu katika hili rika langu kwenye mtaa ninakoishi karibu wote washaoa mpaka na vijana ambao wamezaliwa nawaona imenishushia heshima katika jamii nadharaulika na kila mtu mpaka home ushauri wenu tafadhali nahisi imeniaffect kisaikolojia.
Mshirikishe Mungu utaoa .
Maana hata waganga wanamshirikisha Mungu .
Utaoa tu ukimshirikisha Yeye atutiae nguvu .
Kuna huyu mtu Mshana Jr nilimueleza shida zangu akanipa ushauri .
Mshirikishe Mungu .

Ndiye anayesikia na anayekupa hitaji la moyo wako.

Auoa mzunguu
 
Hapo tatizo huyu haeshimiwi sababu hayuko vizuri kiuchumi, hiyo ndio sababu... Mkuu tafuta hela hamna atakaejali umeoa au haujaoa!

Hao hao wanaokudharau watakuita boss/mkubwa etc
 
Jamani najikuta nawaza sana hivi nitatoa lini? Mbona mda unazidi kusonga? Shauku ya kuoa unakuja mara inapotea, ukimpata unaempenda changamoto inakuwa kiuchumi unakuwa hauko vizuri, ukiwa vizuri kiuchumi wakimuona humuoni jamani mpaka inafikia hatua nawaza nini kinanisibu au kuna mkono wa mtu katika hili rika langu kwenye mtaa ninakoishi karibu wote washaoa mpaka na vijana ambao wamezaliwa nawaona imenishushia heshima katika jamii nadharaulika na kila mtu mpaka home ushauri wenu tafadhali nahisi imeniaffect kisaikolojia.
Wewe Hujazisoma Nyakati? Hao wanaokudharau hususan Ke wanataka uwaoe wao. Wanajipitisha-pitisha kwako halafu wanaona ziii. Wewe kaza uso kama gumegume na utafika muda utaoa tuu. Usioe kwa kutaka kuridhisha mtaa. Hao hao ndo watakuja kukucheka, Watakuja kukuzomea na kukukejeli wakati mambo yatakapokuendea mrama kwenye ndoa yako na itakuwa ni wakati ndoa ishakuwa Ndoana.
Je, Hao wanaokudharau na hata vijana walio oa (kwa shinikizo kama la kwako) unazionaje ndoa zao? Suala kwamba Muda unazidi kusonga (Umri)- asikudanganye mtu.Hakuna cha kuwahi au kuchelewa. Jipange vizuri na ujiimarishe kiuchumi halafu ndio ufikirie habari ya kuoa ukizingatia kwamba unaanzisha Familia ya kwako ambayo utawajibika kwayo. Nakuonya kwamba zingatia sana ndugu yangu kwamba, Kuoa sio suala la kulala na mwanamke tu, bali ni kuongezea majukumu mazito katika maisha yako. Hivi huwa husomi/huoni wenzio wanavyo lia-lia humu jamvini kuomba msaada wa Ushauri?
Jamaa mmoja alisema " Laiti Mungu angelisema anabatilisha ndoa zote na kutoa ruksa kwa kila mwanaume aoe upya - Ni wanaume wachache sana wangeliwarudia wanawake ambao ni wake zao walio nao kwa sasa"
NB: Kama una masikio nadhani Umesikia. Kazi iendelee
 
Back
Top Bottom