Siheshimiwi mtaani kwa sababu sijaoa

Mshirikishe Mungu utaoa .
Maana hata waganga wanamshirikisha Mungu .
Utaoa tu ukimshirikisha Yeye atutiae nguvu .
Kuna huyu mtu Mshana Jr nilimueleza shida zangu akanipa ushauri .
Mshirikishe Mungu .

Ndiye anayesikia na anayekupa hitaji la moyo wako.

Auoa mzunguu
 
Hapo tatizo huyu haeshimiwi sababu hayuko vizuri kiuchumi, hiyo ndio sababu... Mkuu tafuta hela hamna atakaejali umeoa au haujaoa!

Hao hao wanaokudharau watakuita boss/mkubwa etc
 
Wewe Hujazisoma Nyakati? Hao wanaokudharau hususan Ke wanataka uwaoe wao. Wanajipitisha-pitisha kwako halafu wanaona ziii. Wewe kaza uso kama gumegume na utafika muda utaoa tuu. Usioe kwa kutaka kuridhisha mtaa. Hao hao ndo watakuja kukucheka, Watakuja kukuzomea na kukukejeli wakati mambo yatakapokuendea mrama kwenye ndoa yako na itakuwa ni wakati ndoa ishakuwa Ndoana.
Je, Hao wanaokudharau na hata vijana walio oa (kwa shinikizo kama la kwako) unazionaje ndoa zao? Suala kwamba Muda unazidi kusonga (Umri)- asikudanganye mtu.Hakuna cha kuwahi au kuchelewa. Jipange vizuri na ujiimarishe kiuchumi halafu ndio ufikirie habari ya kuoa ukizingatia kwamba unaanzisha Familia ya kwako ambayo utawajibika kwayo. Nakuonya kwamba zingatia sana ndugu yangu kwamba, Kuoa sio suala la kulala na mwanamke tu, bali ni kuongezea majukumu mazito katika maisha yako. Hivi huwa husomi/huoni wenzio wanavyo lia-lia humu jamvini kuomba msaada wa Ushauri?
Jamaa mmoja alisema " Laiti Mungu angelisema anabatilisha ndoa zote na kutoa ruksa kwa kila mwanaume aoe upya - Ni wanaume wachache sana wangeliwarudia wanawake ambao ni wake zao walio nao kwa sasa"
NB: Kama una masikio nadhani Umesikia. Kazi iendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…