Siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi mkuu 2025

Wamekosea kumfanya Silo kuwa katibu mwenezi wa chama.

Sasa hapo kete pekee iliyobaki na msajili na tume ya uchaguz
 
But viongozi wote wa Upinzani wa Kenya kwa sasa walikuwa ni makada waandamizi wa KANU, tunarudi kule kule kwa Nyerere, Upinzani wa kweli utatoka CCM
Sio kila wazo la Nyerere ni sahihi
 
Nchi sio chama nchi ni watu
Na hao watu lazima wapate mtu wa kuwaongoza, au unataka nchi iwe kama Sudan or Congo? Kila mtu afanye vile anataka yeye? Upinzani wetu umeonesha udhaifu sana since 2015, hawafai kupewa nchi
 
Ccm hawajawahi kushinda uchaguzi wowote na hiki alithibitisha Mzee Diallo Mwenyekiti wa CCM Mkoa! Akm
 
Upinzani mnasubiri hadi CCM iwaandalie mtu aje kuwavuruga ndipo mtie akili. Hamkujifunza kwa Lowassa, Sumaye, Membe sasa mnamsubiri Diallo.
 
Una mawazo ya ajabu si mchezo.
 
Tatizo la viongozi wa upinzani wanaendesha siasa kama zima moto /utakuja kuona imebaki week moja before uchaguzi ndo wanataka kuingiza barabarani watu kudai tume huru ya uchaguzi,hapo ndo wananichoshaga sana wakati wakati sahihi ni huu
Kwani sasa hivi hawadai hiyo tume?

Hivi hitaji la tume huru ya uchaguzi ni la wapinzani tu ili waweze kushinda uchaguzi au ni la wananchi wote wapate kuchagua viongozi wanaowataka?

Tusijitoe ufahamu kwa kiwango hicho.
 
Kila mtu sasa mnamwita kada wa ccm. Nyie hamuoni tu wananchi hawawakubali? Kama nia yenu pekee ni kushika dola wenzenu ccm wanaleta maendeleo kwa wananchi.
 

Mkuu Nani atapewa Sasa madaraka na kuifanya Tanzania iwe tajiri ghafla. Unadhani tatizo Ni chama. Wewe mfano chama gani. Je umeshawahi toa au kupokea rushwa. Umeshawahi kula hela usiyostahili. Je kipato chako Ni halali. Wazazi wako. Mkeo. Mumeo. Je wala rushwa Tz Ni wanachama tu wa CCM. Wavivu. Wapiga Dili nk. Chama gani kina sera huko Tz. Mmekalia majungu na kudandia hoja.

Toka atoke Slaa CHadema. Hakuna la maana. Mna watu watukanaji na wqnaharakati. Kuweni wastaarabu ili watu wawatofautishe. Ona wewe unakukazana kusema kuhusu uchaguzi wa 2025.

Hiyo hali mbaya lini ilikuwa nzuri. Watz wanafiki sana. Wanaendesha maisha na kula Bata na kuhongana sana. Nilikuja mwaka huu na kukuta bata tu. Sijui wewe unajua kuwa watz hawajawahi kusema wanazo. Na corona hii sijui unashangaa Nini.

Mama anajitajidi katika nafasi yake. Akijenga shule. Barabara. Hospital nk ndo kazi ya Serikali. Sio kukupa wewe hela mfukoni.
 
Kw
Kwani ccm inashinda kwa uchaguzi?
 
Ccm hawajawahi kushinda uchaguzi tangu viruhusiwe vyama vingi Tanzania!!!
 
Sema ,wapinzani hawajajipanga vizuri.Mbona Zambia wapinzani wameshinda kwa katiba mbovu?Huku kwetu ,hatuna wapinzani tishio.Uchaguzi ukifika,lowassa njoo ugombee.Uchaguzi ukifika Lissu acha kuosha vyombo vya wazungu ,njoo ugombee.Kuna kushinda hapo?
 
Hata kwa hayati watu walilia vyuma vimekaza na akaondoka na 84%. Mama itakuwa mafuriko 2025
Haahaa kwa tume hii hata mie nikigombea kupitia ccm natoka na ushindi wa zaidi ya Jpm yaani hata 95+%
 
Sema ,wapinzani hawajajipanga vizuri.Mbona Zambia wapinzani wameshinda kwa katiba mbovu?Huku kwetu ,hatuna wapinzani tishio.Uchaguzi ukifika,lowassa njoo ugombee.Uchaguzi ukifika Lissu acha kuosha vyombo vya wazungu ,njoo ugombee.Kuna kushinda hapo?
Kwa ukanda wetu katiba yetu hakuna mfano ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…