Nimekusoma naona ni kama vile unataka kuaminisha kwa hisia zako washindani wa Precision wanahusika kwenye hii ajali, jambo ambalo siliafiki, ajali mara nyingi huwa haichagui pakutokea.
Masuala mengine kama muda wa uokoaji kuwa mrefu, na kufungia uwanja hapo nakubaliana nawe, naona kama Majaliwa alikurupuka jambo litakalosababishia usumbufu abiria na watumiaji wengine wa uwanja wa Bukoba.
Kuhusu machozi ya mtendaji/bosi wa Precision yanaweza kuwa ni hisia za kibinadamu tu, wala sio sababu za kibiashara kama unavyodhani, uhai wa mwanadamu una thamani zaidi ya ushindani wa kibiashara, usiusemee moyo wa mtu.