Siitazami ajali ya ndege kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake

Siitazami ajali ya ndege kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake

Unadhani wataiacha, wanaweza kusingizia hata imeliwa na mamba 😂😂😂 kama ile engine ya Scania pale mto Wami.
Sasa kwa yaliyotokea kuhusu Precision hii ni doa tosha kwenye Royal Tour. Naamini watalii wakija nchini wengine wanaenda sehemu mbalimbali za Tz, na Precision wana mchango mkubwa kwenye usafiri wa anga na utalii nchini😭
 
Hivi hizo ndege za kampuni ya Prescion Air hazina kisanduku cheusi. Black box? Inaonyesha Kila mtu anatoa maoni yake chanzo Cha ajali. Tuziachie mamlaka zitupe taarifa rasmi badala ya kutulisha matango pori.

Mamlaka hizi hizi ambazo sehemu yake imeshindwa kwenda kutoa msaada kwa wakati lilipotokea tukio?
Taarifa Rasmi Ni nini/ipi kwa mtazamo wako?
 
Hebu tushirikiane kuwaza mambo kadha wa kadha hapa na ya msingi;

Mara zote kwenye mambo ya msingi nakuwa firm Kabisa utani pembeni hata Kama kuna nyuki wa mama wananikaba Kwa kusema labda sikutakiwa kusema watakuwa wanakosea sana maana nilipumzika kuandika Makala ndefu ndefu nikaishia kuwa naona kama nishaandika kila kitu Kwa wakati sahihi linapotokea ndo nafufua uzi husika wa mada husika !

Swala la ajali hii ya ndege linafikirisha mengi sana nimekuta mtu sehemu anauliza mambo ya msingi Kabisa nikashirikiana naye kuwaza haya

1. Nikiwa nawaamini sana Marubani wa Precision air pengine kuliko wa mashirika mengine, pasi shaka hata chembe najiuliza kwa nini ndege hii imeelekea kwenye uelekeo tofauti wa runway? Katika hili najiuliza Control Tower ilikuwa na ofisa? Na kama ndio alikuwa anafanya kazi gani? Au kwa nini hakutoa vzr/alitoa maelekezo tofauti ya jinsi ya kutua? (Hili linakuja kaa kuwa Rubani yeyote anaweza kutua kiwanja chochote kipya kwa maelekezo kutoka chumba cha waongoza ndege akiwa 5-30miles) juu ya jinsi ya kutua, speed, distance ya kugusia runway, hali ya hewa etc).

Hapa najiuliza sipati majibu na inanipa maswali juu ya chanzo cha ajali hii.

2. Ndege inasema ilikuwa na abiria 43 lakini idadi ya majeruhi 26 na marehemu 19 inafanya maswali mengi. Sitaki kulaumu sana kwa kuwa ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 48 ila TAA ichunguze hii ATC ilitolewaje? Nani walihusika.

3. Ndege imezama, yaan iko sehemu salama kimfumo wa ajali za ndege, tena mita 100+ tu kutoka kiwanja ila uokoaji umechukua masaa zaidi ya manne, RPC anasema watu watulie kila kitu kiko under control, control ipi?...HII NI AIBU KUBWA KWA SERIKALI YETU.

4. Waziri Mkuu ameagiza uwanja ufungwe... Je kuna siri gani hapa nyuma ya pazia? Uwanja una shida gani kama kila kitu kilikuwa sawa? Kama kila kitu kilikuwa sawa ina maana watu wasisafiri tena kwenda Bukoba sababu ya ajali hii? KUNA NINI CHA KUFUNGIA UWANJA?

5. Nimemuangalia Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Airways(Patrick Mwanri) akiomba watu tusipotoshe Umma juu ya ajali hii, amebeba uchungu mzito sana akizungumza akiwa analia machozi mbele ya waandishi... It is not normal, hata kama jamaa anaumia kibiashara ila anajua kabisa Bima watamlipa ila swali la chanzo cha ajali hii na matokeo yake yanawagusa sana Precision kuliko sisi wote.

Binafsi siitazami ajali hii kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake.

Tuwe sometimes na Uwezo wa kuchunguza yanayoendelea chini ya carpet bila kusubiria kulishwa kila taarifa

Kwako Pascal Mayalla


Britanicca
Hapo no 2 labda waliwajumhisha marubani na wahudumu wa ndani ya ndege
 
Kwani awali ndege ilitaka kutua Mwanza ikashindikana ndo ikaelekea Bukoba? Make Kuna abiria waliopoteza maisha kwenye ajali walikua washukie Mwanza.

Je, ni kweli kuwa hali ya hewa ya Mwanza ndo chanzo za kuilazimu Rubani kuelekea Bukoba? Na pia kwa uzoefu wa Hali ya hewa ya Mwanza na Bukoba wapi panakuwa na angalau? Mamlaka ya Hali ya hewa kwenye viwanja vyetu hawawasikiani kutoa ushauri ni wapi angalau Kati ya Mwanza na Bukoba? Ili Rubani afanye maamuzi sahihi Kati ya Arusha au Chato Kama kweli alishindwa kutua Mwanza.
Ndege imetoka dar, inatua mwanza na bukoba, so inategemea na abiria wa mwanza bukoba au bukoba mwanza ndio wataamua ndege ianzie kutua wapi? The route can either be dar bukiba mwanza dar au dar mwanza bukoba dar
 
Anasema eti alitumia kasia kuvunja mlango wa ndege seriously mlango wa ndege sio kitu rahisi kuvunja hata vioo vilivyowekwa sio vya kawaida vyuma vigumu mchanganyiko wa madini,tena anasema alifunga mlango kwa kamba kwa nature ya milango ya ndege inafungwa kwa ndani yeye kamba alifunga kwa wapi hakuna hata sehemu ya kufunga kamba,tena anasema alionana na rubani ukichunguza ndege ilianguka kwenye kina kifupi abiria waliokufa ilisababishwa na mshtuko mkubwa ndio maana ukiangalia kwa mbele ndege imepondeka sana kama ingekuwa imeanguka kwenye kina kirefu hoja ingekuwa na mashiko mshtuko usingekuwa mkubwa waliopona niwale waliokuwa nyuma ya ndege, This is bull shitt msitengeneze stori kushika akili za watu kuficha uzembe na upumbavu uliofanyika.
 
Ndege imetoka dar, inatua mwanza na bukoba, so inategemea na abiria wa mwanza bukoba au bukoba mwanza ndio wataamua ndege ianzie kutua wapi? The route can either be dar bukiba mwanza dar au dar mwanza bukoba dar
No inafuata taratibu Zote ,ndege haijawai anzia Bukoba ikaenda mwanza Mara zoote zinaanza Mwanza then bukoba, pili ndege ikianzia Bukoba Jua mwanza hali ya hewa mbaya sana na haijatikea siku za karibu
 
Pengine swali la msingi hapa ni je why haipiti miaka mitano lazima ziwa victoria liondoke na watu?kuna Siri gani?...kuna matambiko ya damu tunafanya? Sisi si ndo nchi ambayo albino wanauwawa kutafuta Utajiri?..
Nimeona leo
 
Back
Top Bottom