Sijawahi kuielewa timu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan

Sijawahi kuielewa timu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Hili jambo nimeliwaza muda mrefu sana ila sijawahi kupata nafasi ya kulisema.

Hii timu ya Al Hilal ya Sudan sijawahi kuielewa style yake ya uchezaji. NI timu ambayo ki-rank unaweza kusema ni moja ya timu bora Afrika na pia huko Sudan na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki unaweza kusema ni moja ya timu kubwa ila sijawahi kuwaelewa kabisa, hasa katika miaka ya hivi karibuni.

Ni timu ambayo ukiwa unaitazama inapocheza hauoni ni jinsi gani watapata goli wakati huo huo nao hawafungiki kirahisi sana ingawa siyo kwamba wana defense nzuri kihiiivyo. Unaweza kuwalinganisha na uchezaji wa Taifa Stars kwa sasa.

Wangapi wanakubaliana na mimi katika hili?

Soma Pia: CAFCL & CAFCC Group Stage Draw 2024
 
Baadae wakipigwa utayakataa maneno yako,tushawazoea na sababu wanacheza na Yanga.Uzuri JF wanatunza risiti.
Kama nilivyosema katika bandiko langu, nimewaza hivi muda mrefu sana, sikuwahi tu kupata msukumo wala nafasi ya kulisema hili. Hata misimu miwili iliyopita walipoitoa Yanga sikuwa nawaelewa.
 
Kwa hii miaka miwili ambayo sudan haikaliki sijui wakoje. Juzi walicheza na simba wakatoa sare. Sikuona timu ya kuogofya. Ile waliyoitoa yanga mwaka juzi ilikuwa nzuri
Kiwango na uchezaji wao wa sasa hatuna tofauti sana na ule waliokuwa nao walipoitoa Yanga mwaka juzi. Ni timu fulani ya ajabu, usije shangaa wakafika hata nusu fainali.
 
Hili jambo nimeliwaza muda mrefu sana ila sijawahi kupata nafasi ya kulisema.

Hii timu ya Al Hilal ya Sudan sijawahi kuielewa style yake ya uchezaji. NI timu ambayo ki-rank unaweza kusema ni moja ya timu bora Afrika na pia huko Sudan...
Upo sahii... Unapigwa goli haujui lilipotokea, ndio limelala hivyo.
 
Back
Top Bottom