Sijawahi kuielewa timu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan

Sijawahi kuielewa timu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan

Kwa hii miaka miwili ambayo sudan haikaliki sijui wakoje. Juzi walicheza na simba wakatoa sare. Sikuona timu ya kuogofya. Ile waliyoitoa yanga mwaka juzi ilikuwa nzuri
Huko kwao kuna ligi kweli na machafuko yale? Wanapataje nafasi ya kushiriki mashindano ya caf?
 
Kiwango na uchezaji wao wa sasa hatuna tofauti sana na ule waliokuwa nao walipoitoa Yanga mwaka juzi. Ni timu fulani ya ajabu, usije shangaa wakafika hata nusu fainali.
Mwaka gani walifika nusu fainal hii mipira mnaongea mkiwa wapi yaani wafike nusu fainal kwa kupita makundi tu au ushazichukua na hizo Raja na ndugu zake kuwa watafungwa na Al Hilal.
 
Hili jambo nimeliwaza muda mrefu sana ila sijawahi kupata nafasi ya kulisema.

Hii timu ya Al Hilal ya Sudan sijawahi kuielewa style yake ya uchezaji. NI timu ambayo ki-rank unaweza kusema ni moja ya timu bora Afrika na pia huko Sudan na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki unaweza kusema ni moja ya timu kubwa ila sijawahi kuwaelewa kabisa, hasa katika miaka ya hivi karibuni.

Ni timu ambayo ukiwa unaitazama inapocheza hauoni ni jinsi gani watapata goli wakati huo huo nao hawafungiki kirahisi sana ingawa siyo kwamba wana defense nzuri kihiiivyo. Unaweza kuwalinganisha na uchezaji wa Taifa Stars kwa sasa.

Wangapi wanakubaliana na mimi katika hili?

Soma Pia: CAFCL & CAFCC Group Stage Draw 2024
Mkuu kuna watu watawaelewa tu..muda sio mrefu.
 
Ni kweli mkuu yaani hii timu ukiona inavyo cheza waweza dhani ni Jkt ruvu lakini kimbembe kinakuja kwenye kuwafunga hawafungiki kirahisi kabisa.
Hata mamelody na Al Ahaly huwa wana mwaga jasho ya kutosha kupata matokeo wanapo kutana na timu hiyo.
 
1. Ni timu ya Sudani iliyolazimika kuhamia nchini Mauritania kama uwanja wa nyumbani.

2. Kabla ya Uamuzi wa kuhamia Mauritania, Al hilal waliwahi kuwasilisha maombi TFF kuja kucheza ligi ya NBC wakawekewa zengwe.

3. Ni timu yenye ukwasi mkubwa kuliko timu zetu.

4. Yapo madai kwamba mmiliki wa timu hii ndiyo mwenye share nyingi Newcastle United..Anamiliki timu tatu...Newcastle, Al hilal na timu fulani huko Asia..ni mwarabu.

4. Al hilal ina wachezaji mseto wa mataifa kama ilivyo Yanga au Simba....pale wapo wakongo, ivory coast, Ghana, Senegal, Mali, wazawa wengi (Wasudan) wanasugua benchi.

5. Uwanja wa mkapa ni wenyeji sana tu.
Wamekuwa wakiutumia kwny baadhi ya michezo yao kama home ground.

6...Al hilal ni timu iliyozoea maisha ya ugenini..inaishi ugenini, ina train ugenini, inashiriki ligi ugenini, wamezoea maisha ya ugenini..ugenini ni kama kwao.

Unlike, timu zetu zina home sickness.
Namna Simba au Yanga inavyo-react ikiwa ugenini ni tofauti na Al hilal
 
Back
Top Bottom