3rd Portion:
... Maelezo ambayo nilikuja kupewa baadae na head prefect, ni kuwa inaonekana mshua alinitafuta sana kwenye simu kabla hajaenda pale shule, ila hakufanikiwa kunipata. Kwavile hatujawasiliana muda mrefu, na akisema arudi kijijini, maana yake utapita muda mrefu mwingine bila kuonana, ndio akaona afunge safari mpaka shule. Kufika pale akajitambulisha kama mzazi wangu, na akaomba kuonana na mimi. Walim wakashangaa, mzazi wake
Analyse?, Wewe ni baba yake mkubwa au mlezi? Dingi akawa hajaelewa. Akawaambia yeye ni Mzee wangu kabisa, Mwalim wa nidham akaona mshua anamletea masihara, ili swala la wanafunzi kuleta wazazi feki inabidi likomeshwe, akamwambia Mzee akae kwenye benchi. Baada ya kushauriana na mkuu wa shule, wakataka kumpeleka Mzee Polisi. Mshua akawakazia, walivyoona yupo serious sana, wakamuomba ID yoyote.
Akawapa voters ID, walivyoona mfanano wa majina, walim wakachoka. Ikabidi waanze kuulizana, kama wewe ndio baba yake, yule aliyekuja nae ni nani? Hapo ndio wakampa picha nzima. Mzee akacheka (Mzee wangu akiwa na hasira sana, kuna kicheko fulani kinakujaga automatically). Mwisho wa siku wakaazimia head prefect awe ananipigia simu mara kwa mara, akinipata, anipe zile taarifa za kuhitajika shule kwa ajili ya usajili. Na ahakikishe ananishawishi niende na mzazi niliyempeleka last time.
Walimu walikuwa na shauku ya kuniona Mimi maana nimecheza na akili zao, ila Mshua target zake ilikuwa ni kumuona yule mzazi niliyempeleka badala yake. Mwamba Sina ili wala lile, kesho yake nikapanda Simba Mtoto, safari ya shule ikaanza. Nilivyofika, nikaunga moja kwa moja mpaka nguvu mali, nikapoa kwa mshikaji wangu pale Galanosi, kesho yake asubuhi, tukabebana Mimi na yule Mchaga hao mpaka shule.
Ile shule ilivyo, ukishaingia kupitia main entrance, unakata upande wa kulia, ndio kuna ofisi za walim pamoja na head master. Upande wa kushoto, kulikuwa na korido inayoelekea madarasani, lakini pia mwanzoni kuna njia ya kwenda vyooni, na ngazi za kuelekea madarasa ya juu. Sasa kwenye hizi ngazi ndio alikuwa kakaa Mshua ananisubiria Mimi na baba yangu tufike. Na sisi tulivyofika, direct tukakata kona kulia, hatukuangalia nyuma. Mzee akatuungia tela mdogo mdogo. Machale ni kama yalinicheza hivi, nikapata hisia zinaniambia geuka nyuma, kugeuka nakutana na Mshua kakaza sura kimtindo, mikono yote miwili kaikutanisha nyuma ya makalio, kama wanavyopendaga kutembea wazee. Alipoona nimegeuka, akasimama kwa muda Nikapatwa na mshtuko, maana sikutarajia kumuona pale, nikajikuta nimeita "Baba?". Yule Mchaga alikuwa bado hajausoma mchezo, akaitikia "Naam jembe langu". Ila alivyogeuka, na kukuta nimeelekeza attention kwa mtu mwingine, akili yake ikaload faster, akajikuta anatukana kichini chini "Ku***na walai".
Mshua akawa anamuangalia tu, huku kaweka tabasam la mamba. Mchaga akapiga hesabu za haraka, akaona hapa akiingia ofisini, basi hatoweza kutoka, anaweza akaishia polisi. Akapitisha wazo la kutoweka eneo lile, ila njia peke rahisi ni kupitia upande aliosimama Mshua, pia japo shule haikuwa na fensi, ila kukimbilia upande waliopo wanafunzi inaweza ikawa msala zaidi, maana wanafunzi hawana dogo. Akaamua kurudi na njia tuliyojia, upande aliosimama Mshua. Kosa alilofanya Mchaga, alim-underestimate Mshua, labda alijiona yeye kijana zaidi akijilinganisha nae, so angemzidi nguvu. Mchaga alitoka speed ghafla, mshua akawahi kumrukia, wakavaana mpaka chini. Kitendo cha kuanguka chini tu, Mshua kama kawaida yake, akamuwahi Mchaga na kabali moja matata. Mchaga kila akirusha ngumi, Mshua hana habari, ndio kwanza anazidi kukaza mikono. Wanafunzi wakajaa madirishani, kelele zikazagaa eneo lile, wengine wakaanza kutoka madarasani kuja kushuhudia kwa ukaribu.
Walim ikabidi waanze zoezi la kuwaachanisha, walipofanikiwa, Mchaga macho yalikuwa mekunduu kama katoka kulala au kulia. Walim wakawa wanafukuza wanafunzi warudi madarasani, Kisha wakawaomba Baba na yule Mchaga waende ofisini kwa mazungumzo, maana kwa umri wao haifai kushikana mashati namna ile. Wakiwa wanakaribia mlango wa ofisi ya walim, yule Mchaga aligeuka, akatoka speed, akaelekea upande zilipo hostels za wanafunzi wa advance, akapita kwenye senyenge, alivyotokea upande wa pili, akaongeza speed, akapotelea kwenye makazi ya watu. Hakuna hata mwalim aliyejisumbua kumkimbiza, wakabaki wanamwangalia tu. Ila wanafunzi ndio wakawa wanamzomea. Jamaa akasepa, msala nikabaki nao peke yangu. Kikao kikafanyikia ofisi ya walimu wote, mwanenu nikapigishwa magoti huku nasemwa..
Ubaya wa ofisi ya walimu, hata yule mwalim ambae hakujui, lazima apate cha kukuongelea. Nilitembezewa fimbo za kufa mtu siku ile, japo mshua hakunipiga, ila alichangia pakubwa sana kuikuza adhabu yangu, maana aliongea mengi sana, kiasi kwamba nikaonekana kituko. Mshua alilipa ile hela ya faini, nikaruhusiwa kwenda darasani. Aliamua kuondoka siku hiyo hiyo, hakujisumbua kuongea na Mimi baada ya kutoka mle ofisini, na hakunipa hata shiling 10 Kwa ajili ya matumizi pale shuleni. Kiufupi aliniacha kikauzu sana. Nimeingia class sina mzuka hata kidogo, mda wote nimelala kwenye dawati. Mida ya mchana baada ya msosi, nikaamsha zangu kuelekea hostel. Nikalala mpaka mida ya jioni.
Wakati natoka kula msosi wa usiku shuleni, yule jamaa yangu wa Galanosi akanipigia simu, anauliza nimemfanya nini Mchaga? Maana kakutana nae ana nundu kwenye kona ya uso, alaf kamuahidi kwamba siku akikutana na Mimi, sitokaa nimsahau maishani mwangu kwa atakachonifanya. Ikabidi nimuelezee kwa ufupi yaliyojili. Jamaa alicheka sana, mwishowe akaniambia nikienda shuleni kwao niende kwa tahadhari, maana Mchaga alimaanisha alichokisema. Tukaishiana hapo, then nikaenda chamber kupiga msuli. Tokea siku ile nikaanza kupiga sana msuli, sikuwa na msala mwingine wowote, japo walimu waliendelea kuwa wananizingua hapa na pale, ila niliamua kuwa mpole.
Mshua hakuwahi kunitafuta tena, sio kwa simu wala msg. Ni kama alinizila. Kipindi tunakaribia kufanya mtihani wa mwisho, nikaanza kumfukuzia demu mmoja wa O level pale pale shuleni, alikuwa mweupe, sauti nyembamba na kishundu fulani cha kuvunjia shingo, maana akikupita lazima ugeuke. Siku moja nimekaa nae maeneo ya garden mida ya jioni, naendelea kuingizia mistari, maana alikuwa bado hajaeleweka. Katika maongezi akaniambia "Wewe hapa Tanga sio kwenu, unasema unanipenda, wakati siku sio nyingi utamaliza shule, utaacha umenitumia alafu utaondoka".
Nikamjibu kuwa mgeni Tanga hainizuii Mimi kumpenda yeye, umbali sio kikwazo kwangu. Akaniuliza "Unamaanisha unachosema? Kuwa utarudi kwa ajili yangu?, Niambie ukweli, sitaki uongo". Nikasita kidogo kutoa jibu, yeye akaendelea "Mimi ninachohitaji kujua ni Nia yako tu, kama kweli utataka kurudi, mimi nitakurudisha". Ile kauli ikanimakinisha kidogo, nikamuuliza "Utanirudisha kivipi? " Akajibu "Wewe ilo niachie Mimi, je ni kweli unanipenda na ungependa kurudi kwa ajili yangu, nikurudishe??
Nikabaki nimeduwaa kwa muda, najiuliza "Huyu anaongelea nini?".....
Endelea hapa
Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu. Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee