Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

inatakiwa ufahamu mzee dingi anaishi kwa mchongo, km kwenda kwake anafanya mzunguko kiasi hiko na kubadili dala dala hizo ndio arudi kwake hivi anaweza kuweka hela ac moja kweli??

au unasoma story kutafuta makosa sio kujifunza mkuu,.
shida ujuaji mwingi watu, soma enjoy kula kona...yaani mtu anasoma hadithi utafikiri anaenda jibu pepa ya necta...

Yaani Mtendaji Apostle alitakiwa awapotezee tu.
 
Kwa madawa hayo najua kabisa siwezi ni kakwepa kutapeliwa, kama mzee DINGI kubwa la utapeli alienda kutoa hela ATM na vidawa vyake . Je, kwa mti mkavu itakuwaje?
 
16th Portion:


... Usiku huo nilitafakari mambo mengi sana. Ila jambo kubwa ni kitendo cha wale washirika wangu wote kunipa false direction ya sehemu wanazo ishi. Tokea nilivyoamua kujiunga nao rasmi, Mzee Dingi nilidhani amehamia Mbagala au maeneo ya huko, ila kumbe sivyo. Tafsiri iliyonijia, hata wale wengine nao nikaanza kuwa na mashaka na makazi yao. Kwa ufupi, wote walijua Mimi napatikana Tabata, ila wao sijui wanapokaa. Na kibaya zaidi, Mzee Dingi anapajua ninapokaa. Ule mshtuko alioupata baada ya kuniona mitaa ya kwake, ulinipa tafsiri ya hatari. Hii kwangu haikuwa nzuri, nikaadhimia kuhama. Nikampigia dalali anifanyie mpango kesho nipate chumba.

******* ****** ****** *****

Palivyokucha, nikaanza pilika pilika na dalali wangu. Baada ya kuzunguka nyumba kadhaa, hatimae nikapata chumba maeneo ya Tabata Segerea, kwa Bibi pale (kwa wale waliosoma story ya fumanizi la mama mwenye nyumba, nyumba yenyewe ni hii). Nilidhamiria kukaa pale kwa miezi michache, alaf ndio niende eneo jingine nje ya Tabata nitakalokaa kwa kutulia.

Nilitafuta usafiri wa kunihamisha siku hiyo hiyo. Mama mwenye nyumba hakuwepo, nilifanya kumpigia na kumtaarifu kwa njia ya simu. Alisikitika kuhama ghafla, akataka kujua kama kuna tatizo, ila nikamtoa wasi wasi nimepata kazi sehemu, hivyo nataka nihamie karibu na nitakapofanya kazi, ili kupunguza gharama za usafiri. Huyu mama nilishakaa kwenye nyumba zake mbili. Ile ya kwanza tulikuwa wapangaji tupu, hii ya pili ambayo nahama, yeye ndio alikuwa anaishi hapo.

Akaniuliza vipi kuhusu kodi yangu iliyobaki, maana ilikuwa imebaki miezi mingi. Nikamwambia asiwe na wasi, maana nimehama kwa hiari yangu, basi kodi nasamehe.Tukamalizana hivyo. Nikahamisha vitu vyangu.

Nilivyoingiza vitu vyote ndani ya makazi yangu mapya, sikutaka hata kuvipanga vizuri. Nilifunga Kitanda tu.

Baada ya hapo, nikaona niende bank kuweka ile hela iliyobaki, toka kwenye hela niliyochukua kwa Mzee Dingi, sikutaka kuendelea kukaa nayo ndani.

Nikajiandaa kama kawaida ili nitoke. Unajua ngozi ya uso wangu ni ya mafuta, nikipaka lotion, walau kuna unafuu. Ila Sasa kile kitendo cha kuwa naongezea na mafuta ya nazi juu yake, kikawa kinaleta changamoto, nikipigwa na jua kidogo, uso unang'aa kama kitumbua, Yani nikiwa kwambali unajua kabisa Analyse yule anakuja. Hiyo hali ikawa inaniboa, ikabidi nibadili namna ya kupaka yale mafuta ya nazi. Nakumbuka mtaalam aliniambia natakiwa kuyapaka kidogo tu maeneo ya usoni na viganjani. Nikaanza kuwa nayapaka kidogo chini ya mdomo wa chini, alaf na sehemu ya ndani ya masikio. Yani mtu ningekutana nae, kwa haraka haraka angeweza kuhisi nimekosea tu kwenye kujipaka, au pengine hata asing'amue, maana nilikuwa nayapaka kidogo sana.

Tokea niwe na yale mafuta na kile kihirizi, route za mjini hakuna siku niliyowahi toa hela yangu kumpa konda. Tena wale ndio wepesi kinoma, ukimgusa bega kidogo, mtapiga story hadi mwisho wa safari. Alaf nikishuka wananiaga kama vile tunajuana miaka mingi sana.

Leo hii nikisikia mtu katapeliwa kimazingara, siwezi mlaumu kabisa. Akili inakuwa sio yake muda ule. Baadae sana ndio ufahamu unamrudia.

***** ****** ***** ** **

Nilitoka mpaka bank, NMB tawi la Mandela. Pale pale alipowithdraw hela Mzee Dingi. Nilichagua tawi lile, maana ndio lilikuwa karibu na Mimi.

Baada ya pale, sikutaka kulala kule kwangu siku ile. Niliadhimia kwenda kulala kwa Shani. Hivyo nilirudi gheto kwangu na kuchukua kibegi changu cha kazi, na nguo nitakazo vaa hiyo kesho siku ya dili, pia nikapitia sehemu na kumnunulia vitu kadhaa vya kupika ambavyo najua angehitaji. Kisha nikaelekea kwake.

Nilivyokuwa mazingira ya pale kwake, walau mawazo ya kazi ya kesho yalipungua. Naweza sema, niliyasahau kwa muda, au tuseme alinisaahulisha kila kitu.


** ** ***** *****

Asubuhi niliamshwa na simu toka kwa Mzee Dingi, akaniambia niwahi kusogea meeting point, ili niweze kuondoka na wale wazee wengine.

Nikajiandaa kama kawaida, Kisha nikapaka yale mafuta. Sikutaka hata kusubiria chai, japo Shani alisisitiza sana.

Ilitakiwa nikutane nao pale mataa ya ubungo. Nilichelewa kidogo, nikawakuta tayari wamefika, wananisubiria Mimi tu. Nikajitosa kwenye gari ya yule Mzee KY, safari ikaanza.

Kila nikiwa na wale wazee, nilikuwa napatwa na mawazo ya kujilaumu sana. Nilimpotezea Mzee wa maana ambae angeweza kubadili maisha yangu, ila nimejikuta naangukia kwenye himaya ya wazee wa ajabu. Nilipata funzo kwa njia ngumu sana, kwamba usiharibu maisha yako kwasababu ya watu wengine. Maana utaacha mambo yako, kwa ajili yao, ila ikifika wakati wa wao kufanya yao, hawatojiuliza hata mara mbili, watakupotezea bila kujali ulijitoa vipi kwao au ulikuwa na mchango gani.

Safari nzima ilitawaliwa na ukimya. Na ungetuona tulivyokuwa serious na tumependeza, ungeweza hisi ni wana familia tunaenda ukweni kutoa mahari. Maana kijana nilikuwa peke yangu, nimezungukwa na wazee tu.

Ndani ya ile gari tulikuwa watu wanne. Mimi, Mzee KY, mwanasheria feki na Mzee Kidevu. Mzee Dingi yeye alitakiwa kuja na yule mlengwa wetu.

Tulisogea hadi eneo la tukio. Gari ikaenda kupack mbele zaidi, kwenye nyumba fulani kuu kuu isiyokuwa na uzio. Mzee KY akasalimiana na majirani pale, kisha akatukaribisha ndani, na kutwambia kuwa pale ni kwake.

Yani jamaa alitafuta na nyumba kabisa, na hata majirani wanamjua na wamemzoea. Kiufupi alikuwa kajipanga. Nilistaajabu sana, huyu Mzee ni mtu wa aina gani?

Wote kwa pamoja tukatulia, huku tukisubiria signal ya Mzee Dingi.

Mzee KY akatukumbushia tena umuhimu wa kila mmoja kuplay part yake bila kutetereka.

Katika zile siku kadhaa nilizokuwa nakutana nao kupanga hii plan, niligundua kuwa Mzee wa KY ndiye aliyekuwa kiongozi wa kile kikosi. Na hata dili nyingi kubwa, yeye ndio alikuwa anatengeneza plan nzima, namna gani iwe, na yupi achukue nafasi ipi.

Tukiwa pale kwenye makazi feki ya Mzee KY, Mzee Dingi akatuma msg ; "Get Ready"

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
 
Aliyeanzisha swali kuhusu hiyo amount iliyotolewa, sikuwa na plan ya kumjibu, maana kuna some details ni irrelevant ktk simulizi, na hata ukiziweka zinaweza leta tafsiri tofauti.

Sitaki kuingia in details, naomba nikuulize swali "Katika bank unayotumia wewe, una account ngapi?". Ukielewa mantiki ya swali langu, basi hutokuwa na haja ya kunijibu mkuu. Tukutane after iftar [emoji28][emoji28]

Mbona tushafuturu jamani hujashusha
 
7th Portion:

... Mzee Dingi akaniambia "Hela ikishafika mkononi mwako, alaf ukairudisha ilipotoka, utasumbuka sana kupata hela tena. Hela hairudishwi apostle"

Ilo jina apostle lilishaanza kunikera. Japo wanasema jina ukilikataa ndio linakua, ila sikuwa na namna, nikajikuta namjibu kwa hasira "Yule anafamilia inamtegemea, sio haki kumdhurumu, alafu na ilo jina la apostle sitaki kulisikia tena, umesikia we Mzee?". Mzee Dingi akabaki ameniangalia tu, alaf nae akawaka "Sikia apostle, nani ambae hana familia hapa?, Mimi mwenyewe napambania familia yangu vile vile". Akaendelea "Nyumbani hawajali hela naipataje, wao wanachohitaji ni matunzo, hata kama siipati kwa njia halali, ila nyumbani ikifika, inatatua shida zao, na wananishukuru kama Baba"

Nikamkatisha "Utajisikiaje unampa mkeo hela kwa ajili ya ada ya watoto, alaf anatokea mtu anamtapeli?". Wote wawili wakacheka, alaf Mzee Dingi akaniambia "Hiyo ndio itakuwa tiketi ya kurudi kwao, maana siwezi kuwa na mke mwenye tamaa. Huwezi kutapeliwa kama huna tamaa". Nikataka kuongea kitu, yule mwanasheria feki akaingilia "Apostle, kama unamuonea huruma, kamrudishie walau hiyo laki, haya shuka kwenye gari". Sikutaka kuendelea kuongea nao, nikashuka.

Nilivyoshuka kwenye ile gari yao, wao wakaondoka bila kuniambia wanaelekea wapi. Ila Mimi niliendelea kubakia eneo lile lile, nikiwa natafakari nini cha kufanya. Yule jamaa wa mkaa nilikuwa namuonea huruma, ila hapo hapo upande wangu nilikuwa nimefulia sana, kiasi kwamba nafsi ikawa inagoma kurudisha ile hela, jobless upate laki alafu urudishe? Labda Ulaya. Lakini upande mwingine nikajifikiria, endapo nitamrudishia ile laki, basi hapo nitakuwa nimejiingiza matatizoni. Potelea pote, nikaamua kurudi zangu gheto.

Ila nikawa nimepitisha uhamuzi wa kuwapotezea kina Mzee Dingi, maana kampani yao niliiona ni kama ticket ya jela.

Kesho yake mida saa sita, Mzee Dingi akanipigia simu, sikupokea, akapiga tena, sikupokea. Akaamua kutuma msg "Apostle, njoo mtaa wa Msimbazi na Lindi, kuna Kijiwe wanauza kahawa, fanya haraka". Nikaisoma, alaf nikaipotezea, nae akakausha. Ilivyofika wik end, siku ya jumapili, akaniita tuongee. Ila hakutaka tuongelee pale nyumbani, tukaenda kwenye kipub fulani hivi.

Kufika pale, ndio akaanza kuniambia "Sikiliza mdogo wangu, haya maisha yanahitaji kupambana, najua umesoma na unaelimu nzuri, lakini hiyo sio njia pekee ya ww kuingiza hela. Kama kuna kitu hujui ni kwamba, unakismart cha kuaminiwa, nyota yako inang'aa Apostle. Ni rahisi sana mtu kukuamini wewe, alaf na ulivyo muongeaji, na unavyojua kupangilia maneno, wewe ni mtu sahihi kabisa ambaye ofisi yetu ilikuwa inamkosa"

Nikamwangalia yule Mzee wee, sikusema chochote. Mzee aliongea vyote anavyojua ila kwa upande wangu nilishadhamiria siingii kwenye kazi zao. Nikaamua kuondoka eneo lile. Wakati naondoka, akawa ananisindikiza na maneno, "Ulivyokuja kuniomba nikuunganishie michongo, ulitegemea ufanye kazi ikulu? Au ulitaka ofisi yenye A.C? Mshamba sana we mtoto"

Sikumjibu kitu, nikamuacha kwenye ile pub, nikaelekea zangu betting center kupoteza muda.

Siku zilisogea, niliendelea na harakati zangu za kuunga unga kama kawaida, ila Mzee Dingi aliendelea kunishawishi nijiunge na timu yao. Ilifikia hatua ikawa kero sasa, hadi nikaanza kujutia kwanini nilimfataga kumwambia aniunganishie mchongo.

Nilivyoona usumbufu umezidi, nikaamua kuhama eneo lile. Nikahamia sehemu moja Tabata chang'ombe, karibia na hospital ya Kundy. Mimi na yeye tukawa tunaonana mara chache chache sana, hasa kwenye vituo vya dalala au njiani.

Kiuhalisia, baada ya kuhama, hata yeye akaamua kunipotezea kabisa. Ila miezi kama minne tokea nihame pale nilipokuwa nakaa mwanzo, Mzee Dingi akanipigia simu, mpaka kufikia pale, niliamini alishakubaliana na msimamo wangu, so sikuona tabu kupokea simu yake.

Nilivyoipokea, after salamu akaniambia "Apostle, fanya mpango tuonane wik end hii, kuna kitu nataka tujadiliane". Nikamuuliza "Kitu gani?". Akajibu "Usiwe na wasi, sio zile dili za kipindi kile, hii ni issue nyingine, wik end fanya unitafute". Nikamwambia fresh.

Ilivyofika jumapili tukakutana bar. Story mbili tatu, ndio akaniambia alichoniitia. "Sikia apostle, kuna kiasi fulani cha hela ninacho, nataka nianze kufanya biashara halali, sitaki tena dhuluma". Nikamjibu "Ni jambo zuri, ila sijaelewa Mimi nahusika vipi hapa?". Akasema " Sikia apostle, nahitaji mawazo ya biashara na mtu ambae naweza kufanya nae. Nahitaji tushirikiane"

Baada ya blah blah hapa na pale, kuna wazo nikalitoa, ambalo nililifikiriaga muda mrefu, ila mtaji ikawa ndio shida

Na ilo wazo lilikuwa kutoa mkaa vijijini, kisha unakuja kusambaza mjini, kama jinsi alivyokuwa anafanya yule jamaa aliyetapeliwa na kina Mzee Dingi. Nilipomuelezea, akafikiria kwa muda kidogo, Kisha akaniuliza vitu kadhaa kuona uelewa wangu kwenye hiyo biashara. Alivyoona maelezo yangu yapo clear, akasema ngoja atafakari zaidi, huku akiwa anaangalia uwezekano wa kupata madalali hapa mjini, ili mzigo ukifika, tusisumbuke kupata soko.

Tukaagana, nikaondoka eneo lile.

Baada ya kama siku tatu, akanipigia tena. Akaomba tuonane, ila safari hii akaja mpaka nilipohamia. Baada ya maongezi ya hapa na pale, tukawa tumekubaliana kufanya biashara. Kwavile sikuwa na mishe ya kueleweka, hii niliichukulia kama nafasi pekee ya kunitoa kwenye ukata. Nikadhamiria kuifanya kwa moyo na uaminifu, ili kujitengenezea kipato, lakini pia kumuonesha Mzee Dingi kuwa inawezekana kuingiza hela kwa njia halali.

Nilijidanganya. Nilichokuwa nawaza Mimi, sicho alichokuwa akiwaza Mzee Dingi.....


Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Apostle kama apostle[emoji28]
 
Sorry guys portion ya leo imekuwa fupi, kutokana na mazingira niliyopo. Nimejitahidi tu walau kuandika ili nisipitishe siku bila kupost, kama nilivyoahidi. Next portion nitafidia.

Nipo mazingira tight. [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Usjali shukrani sana
 
Back
Top Bottom