Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Nyumba ya kwanza ya huyu mama, nilikaa hata kabla sijafahamiana na Mzee Dingi. Na nilivyohama nyumba ya huyo mama, nilihamia nyumba nyingine before sijahamia aalipokuwa anaishi Mzee Dingi. Na hata nilivyokuja kufahamiana na Mzee Dingi na kumfata kumuomba connection, pale nilikuwa nishakaa kwenye ile nyumba long enough...

What are you trying to prove buddy? Hii story hujibii necta. Do what pleases you, whether ni chai or uji 😅😅😅😅
Kama mtu ashazoea kunyw uji wa ulezi ukimpa uji wa Mchele atapata shida😀

walishindw kumuamini Yesu ni masihi watakuamini wewe aposto ? That's how life is brother😀
 
Ni ngumu uchangiwe na watu wanne watu halafu watu waangalie tu halafu ubebwe uwekwe kwenye gari wanakuangalia tu unaondoka tena na hayo maeneo nimeambiwa na mwananchi mmoja kuna polisi na walinzi karibu. Uwe makini dogo usipoteze umakini please. Utanikwaza
Juzi jumamosi maeneo ya buguruni chama, ukilivuka tu daraja la treni, kuna jamaa muokota makopo aligongwa na bodaboda. Alistrugle pale hadi akafa, no one went of help. Nilipita around saa moja nikiwa ndani ya gari, nikakuta ameshakufa, raia walichofanya ni kumfunika tu. Trafk yupo anaita magari tu ili kupunguza foleni.

Raia wapo, askari wapo, wenye magari na usafiri wapo, ila yule jamaa alikufa wanamuangalia. Sembuse kupigana? 😅😅😅
 
Juzi jumamosi maeneo ya buguruni chama, ukilivuka tu daraja la treni, kuna jamaa muokota makopo aligongwa na bodaboda. Alistrugle pale hadi akafa, no one went of help. Nilipita around saa moja nikiwa ndani ya gari, nikakuta ameshakufa, raia walichofanya ni kumfunika tu. Trafk yupo anaita magari tu ili kupunguza foleni.

Raia wapo, askari wapo, wenye magari na usafiri wapo, ila yule jamaa alikufa wanamuangalia. Sembuse kupigana? 😅😅😅
We call it bystander effect. Hakuna anayejali, kila mtu anahisi atatokea wa kuamua. Huo msaada hautofika kamwe...
 
Nisameheni sana wakuu, bahati mbaya dharura haiji na taarifa. Kune emergency ilijitokeza kwa upande wangu, that's why nilikuwa kimya tokea jumamosi jioni.

Twende pamoja, tumalizie 🙏🙏
usijal mkuu, tuendelee kujifunza kutoka kwako
 
15th Portion:


.... Masharti ya zile dawa, ni kwamba, ili mambo yaende kama unavyotaka. Ukikutana na muhusika tu, kabla ya yote, sharti la kwanza lazima umpe mkono wenye ile hirizi. Akiupokea tu, anakuwa chini ya himaya yako.

Na endapo atakuwa katika mazingira ya kushindwa kukupa mkono, mfano amebeba vitu mkononi au hajataka kukupa mkono, basi unachotakiwa kufanya ni kumpiga piga begani mara mbili au tatu na ule mkono wenye hirizi ( in a friendly way, sio kumpiga kwa nguvu).

Ukifanikiwa kufanya kimoja kati ya hivyo (kumpa mkono au kumpiga piga bega), unagain access ya akili yake. Unachomwambia, lazima atekeleze. Kutokana na kutokuwa na uhakika na lile jambo kama ni kweli linawezekana, ndio maana nilichagua kwenda kwa Shani, maana kumshika mkono au kumpiga bega isingekuwa big deal.

Sasa nilivyofika kwa shangazi Shani, alivyoniona, kwanza akashangaa maana sikuwa nimempa taarifa kuwa naenda. Akaniuliza "Mwenzetu vipi, kuja kimya kimya bila taarifa, ndio umekuja kufumania?"

Nikamjibu "Tusalimiane kwanza basi mama". Alaf nikamsogelea na kumshika mabega yote mawili. Kwavile pete ilikuwa kidole cha mkono wa kulia, nikampiga piga kwenye bega lake la kushoto mara mbili, Kisha nikamwambia

Analyse: "Nimekumiss kipenzi"
Shani: "Kwenda huko, hakuna cha kunimiss wala nini, ni lile game ndio linakuzuzua, huishi kuja"
Analyse: "Wala sijaja sababu ya ilo game. Alaf afadhali umeliongelea, naomba basi leo niende nalo, hapa kwako halitumiki, mwishowe lijae kutu"
Shani: "Babu eeh, chukua ilo hapo uende nalo, maana unaweweseka kweli. Kila ukija mawazo yapo kwenye ilo dude tu"

Nikajikuta natabasamu tu.

Tukapiga story za hapa na pale huku tunacheck tamthilia pale. Msosi ulivyokuwa tayari nikala, kisha nikamla na yeye. Mida ya saa tano nikaaga niondoke. Nikapewa PS, nikaamsha nayo.

Wakati nipo njiani naelekea ghetto, uso umechanua kwa tabasam, najiuliza How is this possible?. Sema kuna wazo likaniambia, alishachoka kukaa nayo, ndio maana kakupa, wala sio hayo madawa yako.

Usiku wa siku hiyo hiyo, kabla hata sijafika gheto. Mzee Dingi alinipigia simu na kuniambia kuwa kesho inabidi tukutane wote kwa pamoja, lengo ni kuweka mambo sawa, na kukumbushana majukumu ya kila mmoja. Location ya kukutania, ni pale pale kinondoni. Akili ikaanza kuniambia Ili dili ni must win, jamaa hawataki liende mlama hata kidogo.


. . . ***** ****** ****** ******

Asubuhi na mapema, nikajisogeza eneo la kukutania. Tukakumbushiana umuhimu wa kila mmoja kutekeleza jukumu lake, lakini pia Mzee Dingi akatupa mrejesho wa maongezi yake na yule mstaafu, kwamba kila kitu kipo sawa, na hiyo siku ya kuonana nae ni ile ile.

Timu nzima ikawa inanisisitiza nihakikishe nakuwa mtulivu na mwenye kujiamini, maana nafasi yangu (mwenyekiti), ndio nafasi muhimu ya kumfanya mlengwa asiwe na wasi wasi kabisa.

Kikao kilidumu kama dakika 45 tu. Kisha tukatawanyika.

Binafsi kwa upande wangu sikuwa na amani kabisa. Nilikuwa nikiiangalia timu nzima tunaokutanaga, sikuwa na Imani na mgao utakavyokuwa. Nilikuwa nimeshaanza kutawaliwa na mawazo ya kudhurumiwa tu.

Sasa tulivyotawanyika, wazo likanijia nimfatilie Mzee Dingi hadi anapokaa. Nikishapajua kwake, itakuwa rahisi kudeal nao endapo watataka kunidhurumu, maana familia yake walikuwa hawajui ukweli kuhusu mishe zake kwahiyo ingekuwa rahisi kumtaitisha akiwa kwake. Maana alichowaambia nyumbani, ni tofauti na anachofanya.

Nikadhamiria kumfungia tela. Pale kinondoni Mimi na Mzee Dingi tukapanda wote gari za kwenda kariakoo. Tulivyofika, tukaachana. Nikawa kama naondoka, ila nikajibanza nimuangalie. Akapanda gari ya Mbagala, nikachukua pikipiki na kuanza kumfatilia. Alivyofika mivinjeni, akashuka, akapanda tena gari ya kurudi Kkoo. Nikaanza kujiuliza, huyu Mzee kasahau kununua kitu town au?. Alivyofika kkoo, akapanda gari za gongo la mboto, zikampeleka hadi bungoni, pale pia akashuka, akachukua gari za Tabata. Kumbe jamaa anakaa Matumbi pale. Inaonekana ndio mtindo wake kila akitaka kurudi kwake. Siku zote nilikuwa najua amehamia Mbagala, maana kila tukiachana lazima apande gari za kwenda kule.

Kutokea pale Matumbi aliposhukia, kuna kibao kinaonesha Matumbi Street, kipo upande ule ule alioshukia. Akaingia na kibao kilipokuwa kinaelekeza. nilimfatilia mdogo mdogo, akikata kona nipo, akavuka reli nipo. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, ni kama vile machale yalimcheza. Tulikuwa kwenye kichochoro kirefu, ambacho sikutaka kumpa distance kubwa, maana nilihisi akikimaliza naweza nikampoteza, njia ni vichochoro mno. Alivyokimaliza tu kichochoro, anageuka nyuma anakutana uso kwa uso na Mimi.

Alishtuka kinoma, akabana kibegi chake kwapani, nakuanza kukimbia. Sikulaza damu, nikaanza kumkimbiza, baada ya kile kichochoro, kulikuwa na nyumba mbili zimefatana. Akazipita akiwa speed kali, Mimi nilivyoipita ile nyumba ya pili, nasikia kitoto kinaitwa "Baba, baba". Kile kitoto kikaendelea "Mama, njoo umuone Baba kapapita nyumbani anakimbia". Akili ikaniambia kumbe hapa ndipo anapoishi, basi sina haja ya kuendelea kumkimbiza, atarudi tu.

Nilivyoisogelea ile nyumba kwa ukaribu, kale katoto kakanikimbilia "Anko, anko umekuja kwetu". Mama ake nae akatoka nje, tukasalimiana pale, akanikaribisha ndani, ila sikutaka kuingia, nikaomba kistuli nikae nje. Baada ya kama robo saa hivi, namuona Mzee Dingi anakuja kinyoonge. Alivyofika akanikata jicho tu, kisha akaingia ndani bila hata ya kunisemesha. Nikamsubiria atoke huku nikiwa natafakari na kupangilia maneno yangu kichwani.

Alivyotoka tu, nikasimama na kumpa mkono, akashindwa kuukataa japo alikuwa kafura, akaupokea. Alaf akaniambia tutoke nje ya lile eneo, kama vile hataki mtu mwingine aliyepo ndani au karibu na pale atusikie. Nikampiga piga piga begani na kumwambia kwamba asiwe na wasi wasi. Kiukweli, sikuwa na nia yoyote ovu na Mzee Dingi. Nilikuwa najua Mimi na yeye wote tuko sawa, maana mganga wetu ni mmoja. Hata ile kumpa mkono, na kumpiga bega, ni vitu ambavyo vilitokea naturally tu, siku tegemea chochote, na wala sikuwa na wazo lolote. Ila cha ajabu, baada ya kufanya vile, Mzee Dingi ghafla akawa submissive sana kwangu. Ule ukali aliokuwa nao machoni, na sura aliyokuwa kaikunja, vyote vikapotea. Nikabaki najiuliza, how come? Inamaana dawa zangu Mimi ziko strong kuliko zake au ni vipi?

Nakumbuka tulivyotoka nje ya eneo lake, aliniuliza "Unashida gani Apostle, mbona tunafatana mpaka nyumbani?".

Unajua kama nilivyosema hapo awali katika kile kikundi, hakuna aliyekuwa anajua wengine wanakaa wapi, au hata kuyajua majina yao halisi. Ni Mimi tu ndio nilikuwa namfahamu Mzee Dingi kwa jina la mtoto wake, na hii ni kwasababu tulishawahi kuishi nyumba moja. Yani hata ungetokea msala, atakayeshikwa ni ngumu kuwakamatisha wengine.

Nikajaribu kumwambia Mzee Dingi, "Nina matatizo ya kifamilia, nataka nimrudishe wife kijijini, akajifungulie kule, ila sina hata mia"

Mzee Dingi: "Kwahiyo unatakaje?"
Analyse: "Naomba unikopeshe kama 1.5m, utanikata kwenye dili letu likishakamilika"
Mzee Dingi: "Hayo ungeniambia kule kule, sio kufatana mpaka majumbani. Kwanza umepajuaje huku? Au ulinifatilia tokea mjini?"
Analyse: "Ilo la kupajua hapa halina umuhimu mzee, angalia namna ya kunisaidia"
Mzee Dingi: "Sina hiyo hela hapa home"
Analyse: "Kwahiyo unanisaidiaje? "
Mzee Dingi: "Nisubirie hapa nakuja"

Akaingia ndani chapu. Baada ya dakika chache akatoka. Akaita pikipiki, ikatupeleka mpaka maeneo ya Tabata T.I.O.T, kwenye ATM ya NMB, akatoa ile amount alaf akanipa. Kabla hatujaachana, Nikajaribu kumuuliza wahusika wote wa ule mchongo tuko wa ngapi?. Je ni wale wale ninaowaona au kuna wengine?

Hakuwa tayari kunipa details za maana, zaidi ya kusema wapo wengine wawili, ila hakutaka kuniambia uhusika wao kwenye ule mchongo.

Tukaachania pale pale, nikaelekea zangu ghetto.

Nikiwa nimebakiza hatua chache kuifikia nyumba niliyokuwa nakaa, Mzee Dingi akanipigia simu. Nilivyoipokea, hakutaka hata kunipa nafasi ya kuongea, alinitukana sana. Alinipa vitisho vya kila aina..

Namuuliza "Kwani kuna shida gani mzee?"

Mzee Dingi: "Unajifanya una akili nyingi sio? Nimeanza kuliona jua kabla yako, nitakuonesha. Usiponirudishia hiyo hela kama ulivyosema, nakuua"
Analyse: "Kwani si tumekubaliana nitakurudishia baada ya dili la yule mama kutiki?"
Mzee Dingi: "Ms*nge wee, huyo mke uliyemtia mimba umemtoa wapi, unadhani kuwa na mke kazi ndogo? We endelea kucheza na akili yangu, nitakuonesha"
Analyse: "Niwe na mke, nisiwe nae, hela yako utapata mzee, kuwa na amani"

Hakutaka kuendelea kunisikiliza, akakata simu.

Hisia zake zilikuwa sahihi, sikuwa na mpango wa kumrudishia ile hela, hata kama wasingenidhurumu.

Nikaingia zangu gheto.

** ***

Baada kuoga, nikaenda maeneo ya Segerea kula vizuri, kisha nikarudi tena gheto. Wakati natoka, simu niliiacha ndani kwenye chaji. Nilivyorudi, nikakuta missed call moja toka kwa Mshua, wakati naendelea kujiuliza nimpigie au la, simu ikaita tena. Mpigaji akiwa ni yeye tena.

Ile hali ya uoga dhidi yake, iliendelea kuwepo. Bado najiuliza, nitamwambia kitu gani?. Nafsi ilikuwa bado inanisuta, natokea nilivyoongeaga na yule Mzee wa Kongowe, sikuwahi kupokea simu ya Mzee wala kumpigia.

Ile simu iliita mpaka ikakata. Ilivyokata, robo saa baadae mama akawa ananipigia. Nikajiuliza, huyu ni Mama kweli ananipigia, au ni Mzee?. Sikuzote Mama akitaka kuongea na sisi, huwa anatubeep tu, na ikitokea umepokea ukala salio lake, basi hiyo ni kesi. So, akipiga badala ya kupokea, huwa tunakata then tunampigia.

Ila siku hiyo nilishindwa kuikata, maana sikuwa na uhakika na mpigaji. Kuikata, ni confirmation kuwa nipo karibu na simu. Na kama nipo karibu na simu why sijapokea simu ya Mshua?. Ikaita hadi ikakata yenyewe, then mpigaji akapiga tena. Badala ya kuikata, nikaamua kuipokea.

Nikawahi kujitetea "Mama sina salio ndio maana nimepok.....". Kabla hata sijamalizia, nasikia sauti ya Mshua;

Mshua: "Salimia kwanza"
Analyse: "Samahani Mzee, nilijua ni Mama, shikamoo"
Mshua: "Ni mwili mmoja, hakuna shida. Mbona hupokei simu zangu?"
Analyse: "Kila unaponipigia nakuwa mbali na simu, alafu Sina salio"
Mshua: "Kama vocha ya 500 inakushinda, unafanya nini huko mjini?"

Nikabaki kimya tu. Akaniuliza "Unaendeleaje? Kila kitu kipo sawa huko?". Nikamjibu "Ndio". Akawa kimya kwa muda, Kisha akasema "Sawa, kuwa mwangalifu usije kuwa kibaka huko". Akakata simu.

Msongo wa mawazo ukarudi upya. Ila nikaamua kujipa moyo, huku nikiwaza dili tunaloenda kupiga na hela itakayoingia. Nahitaji mtaji wa biashara, siwezi kurudi nyuma now, liwalo na liwe......

🤦🤦🤦🤦🤦🤦

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Aaliyyah na ERoni 15 hii hapa
 
Back
Top Bottom