Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Nimecheka mzee Ana vituko sana eti uliona nin kwenye lile tank [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Halaf mama akawa anajua huyu atakuwa mchepuko wa mzee Yaan hawakufikiria analyse ndio mwenye mzigo [emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka
🤣🤣 kuconclude mambo kutammaliza mama aposto
 
9th Portion:


.....Bi Mkubwa ikabidi aniulize kwa upole tu "Tuambie mwanangu, huyu jamaa unashida nae ipi?". Nikaendelea kuwa kimya tu kwa muda. Fikra ndio zikaanza kunituma, huenda kuumwa kwangu yule Kisauti akawa anahusika. Nilikuwa nishamsahau kabisa. Nilipatwa na hasira kuona nateseka kwa kosa lisilokuwa langu. Mshua alivyoona bado nipo kimya, sijamjibu Mama chochote, akanyanyuka na kuanza kuondoka. Bi mkubwa akamuuliza

Bi Mkubwa: "Baba nanii unaenda wapi sasa?

Mshua: "Sasa mtu haongei, nitakaa hapo siku nzima?"

Bi Mkubwa: "Unajua ili ni tatizo kubwa sana, usilifanyie mzaha"

Mshua: "Mzaha anaufanya huyo hapo, katibua watu mjini huko, karudi kutupa sisi shida"

Bi Mkubwa: "Kwahiyo tumuache afe"

Mshua: "Na akiendelea kukaa kimya, atakufa kweli"

Nilivyoona mzozo utaenda kuwa mkubwa, ikabidi niwafungukie issue nzima ilivyokuwa. Baada ya hapo wakaanza kujadiliana nini kifanyike. Bi Mkubwa akashauri wampigie simu Kisauti ili kumuomba msamaha, Kisha waangalie namna gani wanalimaliza lile jambo. Ila Mshua akagoma.

Bi Mkubwa: "Mwanao hali yake sio nzuri huyu, tuwasiliane na mdeni wake, tumlipe yaishe"

Mshua: "Hatuwezi lipa hela ambayo hatujachukua. Huo ni unyonge, na siwezi kuufanya. Dawa ya moto ni moto, kwavile kaanza yeye, acha tuendeleze, ngoja niwasiliane na Mzee Taba, ili tumpeleke kwa mtaalam"

Bi Mkubwa: "Mwanangu haendi kwa mtaalam wala kilingeni, kesho asubuhi naenda nae kanisani kwenye maombi"

Mshua: "Kwa hali ilivyo, lazima twende tu, na ilo halina mjadala"

Ukatokea mvutano mwingine pale, wapi nipelekwe hiyo kesho. Ila Mshua kutokana na commanding force yake, ikaamriwa nipelekwe kwa mtaalam. Kesho yake asubuhi na mapema tukaenda hadi kilingeni. Bi Mkubwa nae hakutaka kubaki nyumbani, alitaka awe na Mimi muda wote ili kujua hatma yangu.

Kufika kwa mganga tukapokelewa vizuri. Kutokana na hali niliyokuwa nayo, nikapewa kipaumbele kuonana na mtaalam. Tulivyoingia ndani, akaanza kuweka vitu vyake sawa, ongea ongea mambo yake pale.

Kuna muda nadhani alipandisha mashetani, maana lafudhi ilibadilika. Yeye ni mtu wa Kanda ya ziwa, ila ghafla akaanza kuongea lafudhi ya kimasai. Kuna mtu mwingine ambae ni msaidizi wake, ndio akawa anasaidia mwongozo wa yaliyokuwa yanaongelewa. Zoezi lilidumu kama nusu saa, then akarudi normal. Bila hata sisi kuongea sana, akaniambia, "Kijana unabahati sana kuendelea kuliona jua mpaka muda huu. Wapinzani wako, dhamira yao ni ya dhati". Mshua akauliza, kwahiyo nini kifanyike?. Yule mtaalam akasema kwasasa kuna kitu inabidi nimfanyie ili kudhibiti maumivu, alaf usiku ndio tutafanya zoezi kamili la kumtoa kwenye hii hali". Mshua akasema sawa, hakuna shida.

Mtaalam akaanza kufanya kazi yake pale. Mle ndani kulikuwa na kinu kikubwa kama vile wanavyotwangiaga wanawake, ila chenyewe kimechakaa sana, yawezekana ni cha muda mrefu, na rangi yake ilikuwa nyeusi tii, na mistari mistari myeupe. Sasa baada ya mtaalam kufanya mambo yake, akataka kupanda juu ya kile kinu, sikujua dhumuni lake lilikuwa ni lipi, maana wote mle tulibaki kuwa watazamaji tu. Wakati yupo juu ya kile kinu, alianguka yeye na kinu chake na kutanguliza uso chini. Alivyofika chini, kimya kikatawala. Urefu alioanguka ulikuwa mdogo sana, hata mtoto mdogo angeweza kusurvive, ila cha ajabu mganga alizimia. Yule msaidizi wake ndio akamkimbilia ghafla na kumnyanyua. Akachovya ule usinga kwenye kibakuli fulani kilikuwa pembeni, alaf akaanza kumpiga nao, huku anaongea maneno ambayo sikuyaelewa. Baada ya muda, mtaalam akaamka, anaongea ila sauti inatoka kwa mbali sana kama kakabwa au ametoka kukabwa.

Muda huo wote, sisi tupo kimya tu. Fahamu zilipomrudia vizuri na kuwa na utimamu wake. Akatwambia kwa upande wake, ili zoezi lipo nje ya uwezo wake, yani limemshinda. Akatuelekeza kwa mtaalam mwingine, aliyekuwa kijiji cha pili ambaye anaweza kutusaidia. Mshua na Bi Mkubwa wakawa wanajadiliana, Mshua anauliza kama twende siku hiyo hiyo, au kesho yake, ila Mama anataka turudi nyumbani. Yule mtaalam akawaambia, kadiri mnavyochelewa, ndivyo mnavyojisogeza kwenye kilio. Muwahisheni huyu, vinginevyo mtamkosa.

Bila kupoteza muda, tukafunga safari mpaka kwenye hicho kijiji. Tukaulizia hadi tukafanikiwa kumfikia yule mganga. Kutokana na miundombinu ya kijijini ilivyo, tulijikuta tunafika pale jua likiwa limeshaanza kupungua nguvu.

Tulipokelewa vizuri na msaidizi, tukakaa foleni kusubiria zamu yetu ifike.

Mida ya saa kumi na mbili kasoro, ndio tukafanikiwa kuonana nae. Hapo Bi Mkubwa nafsi haijamtulia kabisa. Muda wote kama ana mashaka na mganga. Ile hali ya Bi Mkubwa ikawa inamkera yule mtaalam. Akatwambia "Kuna hii dawa, ili zoezi lifanikiwe, inabidi wote watatu muilambe". Akaanza kutaka kumpa Bi Mkubwa, Mama akasita kidogo. Yule mganga akamkata jicho. Ikabidi Bi Mkubwa akubali kuilamba. Cha ajabu baada ya Bi Mkubwa kuilamba, sisi wengine hatukupewa. Bi Mkubwa akahoji kulikoni? Yule mganga akatoa usinga na kumpiga nao kichwani, Bi Mkubwa akasombwa na usingizi. Mimi na Mshua tukajikuta tunatazamana tu bila kusema chochote.

Baada ya salamu, akatwambia "Poleni sana na safari, maana huku tulipo ni mbali sana na mlipotoka". Baada ya kumuelezea dhumuni letu la kuwa pale, nae akafanya standard procedures zao (naziita standard procedure maana kote nilipoenda naona wanafanya hivyo). Baada ya muda kidogo akaanza kutwambia. Akaendelea "Tatizo lililowaleta hapa nimeliona vizuri sana, ila kwa bahati mbaya lipo nje ya uwezo wangu"

Mshua akamuuliza "Unamaanisha nini?". Yule mganga akasema "Aliyemfanyia hivi kijana wako, ni mtu aliyedhamiria sana, na hata huko alipoenda, ni Kwa mtu mwenye uwezo wa juu kuliko wangu. Hapa ninaweza kuliona tatizo, lakini uwezo wa kulitatua ndio sina"

Mshua akawa kama mtu aliyekata tamaa, akamuuliza yule mtaalam "Sasa unatusaidiaje au unatushauri kitu gani?. Yule mganga akamjibu "Kitu ninachoweza kuwasaidia kwasasa ni kuwapa sehemu ya kupumzika usiku wa leo, na kesho patakapokucha, nawashauri mtafute mganga mwingine".

Kusikia vile, hata Mimi nikajihisi kukata tamaa, Kisauti amedhamiria kunipoteza.

Mshua akamuuliza, dhumuni la yeye kumfanyia vile Bi Mkubwa ni lipi?. Mtaalam akamwambia "Huyu hakuwa na utulivu wa nafsi, kadiri muda unavyoenda angeweza kunikwaza, ila msiwe na wasi, ataamka ndani ya muda mchache ujao.

Mshua akaomba tuondoke siku ile ile. Wakasaidiana kumuweka Bi Mkubwa ndani ya gari, na kumlaza siti za nyuma. Mimi na Mshua tukawa mbele, safari ikaanza.

Tukiwa njiani, Bi Mkubwa ndio fahamu zikamrudia, akajiinua na kukaa. Mshua akageuka na kumuuliza anajiskiaje? Bi Mkubwa hakujibu kitu, ila likamtoka fyonyo moja refu. Kiasi kwamba kule mbele tukapatwa na hali ya kutaka kucheka. Kuzuga ikabidi nigeukie nje, maana ningecheka yangezuka mengine. Mshua sababu ya kuendesha, plus ubovu wa barabara hakuweza kugeukia nje,alaf kicheko kikataka kumponyoka. Akazuga kupiga chafya na kujikoholesha. Picha nzima Bi Mkubwa akawa kaisoma. Bi Mkubwa ni dizaini ya wale wa wamama ambao Ukifanya kosa anaweza akakukata jicho kali hata kwa dakika 5 nzima, sasa ndicho kilichotokea kwenye gari. Alimkata jicho Mshua, kiasi kwamba kule mbele Mshua akawa anahisi ile hali. Ila hapo hapo anajizuia kucheka tena, maana heri ya Mimi, yeye angecheka tena ile safari ingekuwa chungu kwake.

Wote tukawa kimya, unasikika mziki tu kwenye radio. "Zima mamiziki yako inaniumiza kichwa Mimi" Bi Mkubwa akawaka ghafla, Mshua wala hakuongea kitu, akazima, safari ikaendelea.

Njiani nzima akawa anasikika Bi Mkubwa tu, anatusema weee, alaf anakaa kimya. Baada ya muda kidogo anatusema tena, Kisha anakaa kimya.

Mshua yeye yupo kimya tu, macho yako mbele muda wote. Kadiri gari inavyonesa nesa kwenye ile barabara mbovu, na Mimi ndivyo ninavyozidi kugugumia maumivu, Mama nae anakunja sura kwa uchungu, kama vile na yeye anaumia. Mshua yupo kimya, hana story na mtu. Ila kila Bi Mkubwa akimsema, yeye ananikata jicho Mimi, kujaribu kunionesha kuwa Mimi ndio chanzo.....
Mshua kama mshua 😂😂😂

Bi Mkubwa
: "Baba nanii unaenda wapi sasa?

Mshua: "Sasa mtu haongei, nitakaa hapo siku nzima?"

Bi Mkubwa: "Unajua ili ni tatizo kubwa sana, usilifanyie mzaha"

Mshua: "Mzaha anaufanya huyo hapo, katibua watu mjini huko, karudi kutupa sisi shida"

Bi Mkubwa: "Kwahiyo tumuache afe"

Mshua: "Na akiendelea kukaa kimya, atakufa kweli"

mganga alivyodondokea kichwa ningekua ni mimi nisingeweza jizuia kucheka 😂
 
Back
Top Bottom