Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Alianza Mzee wa kichaga (Baba fake), akaja Mzee baba A.K.A mzee michongo na sasa kuna Mzee wa tatu na hatujajua anakuja na visa gani.

Anyway usisahau kuni-tag portion inayofuatia mkuu.
 
Alianza Mzee wa kichaga (Baba fake), akaja Mzee baba A.K.A mzee michongo na sasa kuna Mzee wa tatu na hatujajua anakuja na visa gani.

Anyway usisahau kuni-tag portion inayofuatia mkuu.
Sawa mkuu usijali
 
11th Portion:

... Kabla sijamfata nje, nikahakikisha kwanza kama milango Iko wazi au kama kaacha kamfungia Bi Mkubwa kwa nje. Nilivyokuta Iko wazi, ndio nikamfata.

Tofauti na matarajio yangu, kule nje Mshua alikuwa mpole sana kuliko kawaida yake. Na alikuwa anaongea kama mtu ambae mawazo yake yapo mbali sana.

Mshua: "Hivi unajua Mimi na yako ndoa yetu inamuda gani?
Analyse: "Nahisi kama thelathin naaa hivi"
Mshua: "Unahisi sio?". Sasa sikiliza, nilianza mahusiano na Mama yako mwaka 75, ila nilikuja kufunga nae ndoa mwaka 82. Katika kipindi icho chote tulikuwa na furaha sana. Na hata baada ya kufunga ndoa furaha na upendo viliongezeka pia. Katika kipindi chote icho, ugomvi serious ambao ulishawahi kutokea kati yetu, ilikuwa ni mara moja, mengine ni ya kawaida tu"

Nikabaki namwangalia tu, bila kumkatisha. Akaendelea "Ila tokea umezaliwa wewe, ugomvi kati yetu imekuwa kitu cha Kawaida sana. Kwanza sasa hivi Mimi sio priority tena kwa mke wangu, hasa wewe ukiwepo hapa nyumbani"

Nikajikuta nataka kucheka, yani Mshua na umri ule bado analia wivu?. Akaniwahi "Cheka uone nini kitafatia". Nikajibana, ila yeye ndio akajikuta anacheka [emoji28][emoji28].

Akaniambia sikia "Nakukumbusha kuwa wewe sio last born, na Safari hii ukiondoka hapa usirudi tena bila mke. Yani wewe yeyote tu njoo nae Mimi kama baba nitampokea". Nikabaki nimeshangaa, Mzee Vipi?

Akaendelea "Ili kulegeza bond ya wewe na Mama yako, inabidi na wewe uoe, swala la utamuoa nani, utajua mwenyewe"

"Pia kitu kingine cha muhimu, unamkumbuka yule Mzee niliyekupaga namba yake?". Nikamjibu ndio, "Ukifika mjini, safari hii fanya juu chini uonane nae". Nikamjibu hakuna shida nitafanya hivyo.

Tukaongea mambo mengine tofauti tofauti ya kiutafutaji. Wakati tunahitimisha, ili turudi ndani maana Bi Mkubwa alituita tukale, Mshua akanisisitiza tena "Ukijiona unataka kurudi huku bila mke, basi uishie center, nitakufata tuongelee huko huko, na hakuna kumwambia Mama yako kuwa unakuja. Ila ukijitoa akili ukaja mpaka huku kijijini bila mke, basi jua lazima nikuozeshe binti yeyote wa hapa kijijini, swala la kumpenda, utampenda mbele ya safari ukishamzoea. Na ni lazima uondoke nae". Kumbe Bi Mkubwa alikuwa kasimama dirishani, haya maongezi ya mwisho mwisho akayasikia, nae akatoka nje "Kumbe ndio maana mmekuja kujificha, hayo ndio maongezi yenyewe?. Kama wewe ulitafutiwa mke, hizo ni enzi zenu, sio zama hizi. Mwanangu hachaguliwi mke, mwanangu oa ukiwa tayari, na ukiwa na mwanamke utakayemtaka, wala hakuna presha."

Hii kauli ya Bi Mkubwa nikawa sijaielewa, anamaanisha Mshua alitafutiwa mke?. Sikutaka inipite, ikabidi niulize. "Kumbe Baba alitafutiwa mke?". Mama akataka kujibu, ila Mshua akamuwahi na kunijibu "Achana nae, hajui anachokiongea huyo.

Mama (akacheka kidogo): "Kwamba sijui ninachokiongea?. Kumbe wanao hawajui story yako? (Akacheka tena)"

Analyse: "Story gani hiyo?. Baba siumetoka kuniambia umejuana na Mama tokea miaka ya 70, ukamuoa miaka ya 80?. Kuna story tofauti na hiyo?". Mama akawa anacheka tu.

Mshua: "Kwani mtu akituma mshenga, hapo anakuwa katafutiwa mke?. Huyu mama ako haelewi mambo yanavyoenda". Akamalizia kwa kicheko.

Ila kila Bi Mkubwa alipokuwa anataka kuongea, Mshua anamcrash as if anazuia asiongee. Nikajaribu kum-probe Bi Mkubwa walau anipe hiyo story ila akaishia kucheka.

Mama: "Atakuambia mwenyewe huyo, ila Cha msingi oa mwanamke utakayemtaka wala asikulazimishe"

Mshua: "Si alikuja na yule rafiki yangu, nusura ufe kwa kihoro hapa ukijua ndio mka mwana [emoji28][emoji28][emoji28]"

Bi Mkubwa akamkata jicho bila kusema kitu, alaf akanigeukia Mimi, "Sema na wewe usije kutuletea kizaa zaa kama cha yule wa kipindi kile"

Nikaishia kutabasam tu, Kisha tukaingia ndani kula.

******** ****** ******* ***** *******

Baada ya siku mbili nikaondoka pale nyumbani. Kufika town, ramani zote hazisomeki. Nikamcheki yule Mzee, baada ya kunitambua tukaongea mawili matatu. Akaulizia kuhusu afya yangu, then tukaweka appointment nikaonanae mwishoni mwa wiki. Akanielekeza maeno ya Kongowe, kuna sehemu unapanda milimani, Mlamleni kwa mbele mbele huko. Sikuwa nimewahi kufika maeneo yale, ila nikasema itabidi niende.

Ilivyofika siku tuliyokubaliana. Wakati nipo njiani, akanipigia simu. Baada ya salamu akaniuliza,

Mzee: "Vipi umeshaanza safari ya kuja huku?"
Analyse: "Ndio Mzee"
Mzee: "Ukifika Kongowe mwisho, subiria hapo, kuna kijana wangu yupo njiani nae anakuja huku. Yupo na gari, mtakuja wote"
Analyse: "Sawa Mzee"

Nikafika mpaka pale, nikasubiria. Muda kidogo napigiwa simu, baada ya kuongea nae ndio nikajua ni huyo kijana ninayetakiwa kwenda nae. Nikasogea hadi alipopaki gari, then safari ikaanza. Njiani no story, hadi tunafika.

Kufika, ni eneo fulani kubwa, pia lina uzio. Ila kwa ndani sehemu kubwa Iko wazi, kuna mabanda mengi ya mifugo na nyumba moja ya kuishi watu, ambayo imejitenga kiasi chake.

Tukapokelewa na mlinzi. Baada ya muda kidogo, yule Mzee ndio akaja. Tokea nimeanza kuwasiliana nae, kwa mara ya kwanza hiyo ndio siku tulikuwa tunaonana. Nilishtuka kumuona, japo hiyo siku ndio ilikuwa tunakutana ana kwa ana, ila sura yake haikuwa ngeni kwangu, ni mtu ambae sura yake iko very popular. Alishawahi kuhudumu nyazfa kadhaa kwenye serikali, awamu za nyuma kabla ya Ngosha.

Ni mtu ambae najua tunatokea nae mkoa mmoja, ila sikuwahi jua kama anafahamiana na Mshua. Na hata Mshua siku zote anavyoniambiaga nikaonane nae, hakuwahi niambia huyo mtu ni nani haswa.

Yule Mzee kaniambia nimsubirie amalizie kuangalia mifugo yake na kuweka mambo sawa, kisha tutaongea. Na kweli baada ya kama dakika 45, akaniambia tuongozane kuelekea kwenye ile nyumba iliyojitenga. Lakini kabla hatujaifikia, akabadili mawazo, akamuagiza mmoja wa vijana waliokuwepo pale atuletee vitu, then tukaenda kukaa chini ya mti.

Wakati tunaweka viti vizuri ili tukae, akaniambia

Mzee: "Mbona kama umeshangaa kuniona Mimi, ulitarajia kukutana na nani?
Analyse: "Hapana sio hivyo Mzee, ni vile sikutarajia kukutana na sura ninayoifahamu"
Mzee: "Haya niambie ushawahi kuiona wapi hii sura unayosema unaifahamu?"

Sikujibu kitu, nikaishia kutabasam tu kama namna ya kuzuga.

Mzee: "Inaonekana uko busy sana"
Analyse: "Hapana Mzee"
Mzee: "Kwanini hukunitafuta kipindi chote icho, mpaka ile juzi ulivyo nipigia?."

Nikakosa utetezi.

Akaendelea

Mzee: "Kipindi kile tunawasiliana kwa mara ya kwanza, ndio nilikuwa kwenye mchakato wa kustaaf. Kwasasa nimstaafu, nakujaga kupoteza muda na mifugo huku"
Analyse: "Ni jambo zuri, ukisema ukae tu, mwili utashambuliwa sana na maradhi"
Mzee: "Ni kweli, maana umri huu hakuna tena kash kash"

Tuliongea vitu kadhaa, ambavyo ni kama tulikuwa tunajenga msingi wa dhumuni lililofanya tuwe pale. Baada ya hizo story za hapa na pale kuisha, tukaenda kwenye dhumuni sasa. Maongezi ambayo mpaka leo natamani nisingeyasikia au kuyajua. Ni maongezi ambayo kila nikiyafikiria, huwa naishia kujifyonya mwenyewe.

Maongezi ambayo yalifanyika kwa masaa machache ila yamekuwa yakiniumiza kwa muda mrefu.

Kiufupi, ni maongezi ambayo yananifanya najilaumu kila iitwayo leo......
'Cheka uone nini kitafatia' [emoji23]
 
Back
Top Bottom