Nyuki Mdogo
JF-Expert Member
- Oct 31, 2021
- 4,134
- 10,644
Nakuomba inbox madam...Unajizima data aposto ππππ!! Haya nawaita naomba list yao basi ππππ
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakuomba inbox madam...Unajizima data aposto ππππ!! Haya nawaita naomba list yao basi ππππ
@Analyse ... Aposto umekua digidigi [emoji23]20th Portion:
... Nikiwa pale kwenye kiti, Mzee Kesho Yetu alibaki ameniangalia kwa muda mrefu, Kisha akaniambia
Mzee KY: "Sikia bwana mdogo, nakushauri upotee mjini kwa muda. Hivi pale ulishahama?"
Analyse: "Ndio"
Mzee KY: "Vizuri, sasa inabidi usionekene Dar kwa kipindi fulani, ili upishe hali ya hewa itulie."
Analyse: "Natamani kufanya hivyo, ila hela ndio sina. Kule kuhama hama, kumenipotezea hela sana. Hata huku kukutafuta wewe nako kumenirudisha nyuma"
Mzee KY: "Enhee Hapo hapo kwenye kunitafuta, naomba tukiachana leo nisikuone tena hata kwa bahati mbaya. Nisingependa unifatilie tena"
Analyse: "Sasa naondoka vipi na Sina hela?"
Mzee KY: "Unapoanza jambo lolote, lazima uwe umepanga namna ya kulimaliza. Vinginevyo utajikuta unaingia matatizoni kama hivi sasa"
Analyse: " Basi nifanyie mpango hata wa kiasi kadhaa walau kiniwezeshe kupotea"
Mzee KY: " Sina hela kwasasa"
Analyse: " Hela zote ulizopiga Mzee?"
Mzee KY: " Hela zote kiasi gani?. Hivi unajua nyuma yangu kulikuwa na watu wangapi hadi dili likafanikiwa?"
Akaendelea, " Nitakupa ile laki mbili niliyokuahidi wakati ule, nitakuongezea na elfu hamsini. Zaidi ya hapo, sina."
Nikabaki nafikiria tu pale, natokaje salama kwenye huu msala?
Akaendelea, "Tena kitu unachotakiwa kukikwepa sana, ni kuonana na wale wazee wengine. Ni rahisi wao kukuchoma, ili wao wajiweke on safe side".
Analyse: " Sawa nimekuelewa, ila nina ombi moja la mwisho"
Mzee KY: "Ombi gani?"
Analyse: "Unajua wale wazee walinipora ile hirizi niliyopewa na yule mtaalam wako, kama inawezekana unidirect kwake akanipatie nyingine"
Yule Mzee aliniangalia kama vile nimeongea kitu ambacho hakukitarajia kabisa.
Mzee KY: "Ilo haliwezekani kabisa. Alafu nilijua utaongea kitu cha maana, kumbe kujichanganya na wazee akili yako ndio ishavurugika hivyo?"
Analyse: "Sina akiba Mimi, alaf natakiwa kujificha. Najifichaje sasa?"
Mzee KY: " Hayo ilibidi uyawaze kabla hujaamua kuingia kwenye hizi kazi"
Analyse: "Ila nyie ndio mlionishawishi kuingia kwenye hizi kazi"
Mzee KY: "Ila hakuna aliyekulazimisha"
Maneno yake yanazidi kunikata moto, maana bila hela ya maana ni ngumu kutoboa mafichoni.
Analyse: "Basi nisaidie jambo jingine?"
Mzee KY: "Lipi?"
Analyse: "Kwavile wewe unabiashara nyingi genuine mjini, basi nifanyie hata mchakato nifanye kazi kwako"
Akanishangaa tena;
Mzee KY: "Bwana mdogo kumbe hauko smart kama nilivyodhani. Umefikiria kabla hujatoa ilo ombi?"
Analyse: "Nimefikiria, ila sina namna ya kusurvive"
Mzee KY: "Sikia, Mimi na ww kitendo cha kufahamiana kwa njia hii, basi hatuwezi tena changamana nje ya hapa. Na kama tungejuana nje ya hapa, basi hakuna uwezekano ungeweza kunifahamu namna hii. Wakati unajiunga ulijua unachokuja kukifanya, na ukaamua kujiunga, tafuta namna ya kujitoa"
Yaliongelewa mengi, lakini hapakuwa na lolote ambalo lingeweza kumfanya either aniongezee hela au hata anipe ajira. So, tukamalizana kwa yeye kutoa hela kwa wakala, na kunipatia. Hakutaka kabisa kunipa namba yake aliyokuwa anatumia pale. Baada ya kunipa hela akaniambia;
"Kubali hasara, badili simu na hiyo line. Usivitumie tena. Narudia, Simu na line, sio line peke yake"
Tukaagana, nikaamsha.
Nikazunguka, upande wa parking. Nika nakili namba za lile gari lao, kisha nikadandia usafiri wa kurudi Dar. Nikiwa ndani ya coaster, Mzee Kesho Yetu akanitext kwa ile namba yake ya siku zote, "Nimeambiwa umenakili plate namba za hii gari, fikiria mara mbili kabla hujafanya ulichokusudia, maana hakuna kurudi nyuma baada ya hapo".
Nikajifikiria kwa muda, ila nikaamua kumpotezea. Maana hata Mimi mwenyewe sikujua kwanini nimenakili ile namba, ila nilipata hisia inaweza kuja kuwa na msaada mbeleni.
Sababu iliyosababisha nirudi Dar, kwanza sikuwa nimeplan niende wapi, pili sikuwa nimejipanga vizuri namna ya kuondoka.
Nilivyokuwa ndani ya gari, ile simu nikaamua kumuuzia abiria aliyekuwa pembeni yangu. Niliiuza kwa bei ya hasara, ila sikujali. Line nikafuta majina yote, kisha nikaitupa mle mle ndani ya gari.
Nikanyoosha moja kwa moja mpaka gheto. Naanza kutafakari wapi nitaenda. Kesho yake nikanunua simu ndogo ya batani na kusajili line mpya, kisha nikarudi ghetto. Sikuwa napenda kushinda sana nje. Giza likishaanza kuingia, ndio nilikuwa nautumia huo muda kutembea tembea.
Zilipita kama wiki mbili, bila kash kash yoyote au kukutana na mtu yeyote wa kunipa mashaka. Nilivyohisi kama kumetulia, kuna jamaa yangu nikaenda kuonana nae maeneo ya Mikocheni, sasa muda narudi nimefika pale mwenge mataa. Nilisimama karibia robo saa nzima, natafuta timing ya kuvuka barabara, maana gari zilikuwa speed sana.
Zilivyopungua nikawa navuka. Sasa wakati navuka, kuna Mzee nae akawa anavuka kutokea upande opposite na wangu. Ikatokea ile hali ya kugonganisha njia. Yani wewe ukitaka kupita upande wa kulia, wa mbele yako nae anakua kaamua kupita upande huo. Ukisema ushift kushoto, unakuta na yeye karudisha mawazo ya kupita upande huo. Mpaka mnajikuta mnagongana. Icho ndicho Kilichotokea kwa yule Mzee.
Kila nikimkwepa na kwenda kulia, nae anakuja huko, nikirudi kushoto nae huyo kushoto. Binafsi nikikutanaga na situation kama hiyo, huwa nasimama, ili huyo mtu mwingine apite, ila Cha ajabu kwa yule Mzee, nilivyosimama na yeye akasimama. Alafu muda huo huo, kuna gari ipo kibati inakuja upande wetu. NilivyΓ³ona simuelewi yule Mzee, nikaamua liwalo na liwe, kwa nguvu zangu zote nikaamua kumpush ili tuangukie anapotoka yeye. Cha ajabu, nilitumia nguvu nyingi sana, ila nikajikuta napush hewa, hapakuwa na mtu mbele yangu. Nikaangukia upande wa pili, ile gari ikapita speed bila hata kusimama.
Haya yote yalitokea ndani ya muda mchache sana. Cha kushangaza, watu waliokuwa jirani, wao walichukulia kile kitendo kama nimejirusha ili kulikwepa lile gari, kumbe mwenzao niliona vitu tofauti. Na kati yao waliokuwa wanaongea, hakuna aliyezungumzia habari za kumuona mtu mwingine mbele yangu. Waliishia kunipa pole, wengine hongera kuwa siku yangu ya kufa bado nk. Lile tukio lilinifikirisha sana. Kwanini limetokea? Linahusiana na issue tuliyofanya kwa yule mstaafu?. Au ndio ndugu zake wameamua kunifanya kama alivyofanya Kisauti?. Kama ni hivyo, why Mimi niwe napataga adhabu tu, alaf wanaofaidika ni wengine?. Najitoaje kwenye Ili?
Akili ikaanza kuniambia niondoke mjini haraka sana. Ila naenda wapi?. Home nikienda, lazima niulizwe kwanini nimeenda, maana wao wanahisigi nikishazingua ndio huwa naenda. And this time ni sahihi, nishazingua, je niende au nisiende?
Ila hata nikienda, kama jamaa wameniamulia, wanaweza kunidhuru nikiwa kule kule. Nikaanzr upya vurugu za kwenda kwa waganga na Mshua?. Mawazo yakanijia nimpigie Kisauti, dhumuni ikiwa walau anipeleke hata kwa mtaalam wake nikajikinge kwanza. Ila kuna sauti ndani yangu ikawa inanikumbusha maonyo ya mtaalam kuwa nisije kumtafuta tena Kisauti. Ila nitafanyaje?. Namtafuta vipi huyo Kisauti
wakati namba yake sikuwa nayo, niliifuta nilivyouza simu?.
Na kusema niende mpaka kule walipo kabla sijaongea nae itakuwa uongo. What if hasira zao hazijaisha? Na zinaishaje ikiwa hawajapata hela zao?.
Ndani ya wiki nilishaanza kukonda kwa mawazo, maana pia hela Nazo zinaisha tu Kwa matumizi, ila siingizi hata 100.
Wiki mbili tokea lile tukio la pale mwenge litokee, sister akanipigia simu kuwa Mama anaumwa sana, alafu sijawahi hata kuwajulia hali. Ofcourse kichwa changu kisipokuwa na utulivu, huwa kuwatafuta watu inakuwaga issue sana. Na mtu asiponielewa, tutagombana mara kwa mara, ndio maana mahusiano yangu mengi yanavunjikaga kwa mtindo huu. Tokea nibadilishe simu na line, nilivyowapigia ndugu zangu kuwataarifu kuhusu namba yangu mpya, sikuwahi kuwatafuta tena.
Na hapo ulishapita karibia mwezi mzima. Baada sister kunipigia na kunipa ile taarifa, nikajiona nishapata sababu ya kwenda home. Nikaamua kumpigia Mama home, simu alipokea Mshua. Baada ya salamu za hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kunielezea hali ya Mama. Nikamwambia kuna kazi ya watu naiweka sawa, kisha baada ya wiki moja nitaenda kuwaona. Hakunipinga.
Sikuwa na kazi yoyote, ila Mshua namjua hivyo sikutaka maswali mengi. Ningemwambia kesho yake naanza safari, angetaka kujua kwamba Sina mishe huku mjini? Maana haiwezekani taarifa upewe leo, then kesho upo ndani ya bus. Sikuwa nimejiandaa namna ya kudanganya, nilihofia ningebabaika alaf akahisi kuna jambo haliko sawa.
Ile wiki nzima ya kusubiria safari, sikutaka hata kutoka nje na pale nilipokuwa naishi. Muda wote nipo ndani, au chooni. Ndani au dukani. Kiufupi niliishi kama digidigi.
Baada ya wiki, nikafunga safari kwenda home. Punch alizoenda kunipa Mshua, zilikuwa ni mara mia ya alizonipa Mzee wa Kongowe.
Walau Mzee wa Kongowe alikuwa ni mtu baki, maana kuna baadhi ya maneno ukiambiwa na mtu wa karibu sana, yanachoma kuliko hata msumari. Mzee wa Kongowe alinifanya nikaanza kumuangalia Mshua kwa namna ya tofauti. Ila maneno ya Mshua yalinibadili mtazamo wangu kabisa.
Kauli za Mshua Ziliniumiza sana, ila naweza kusema zilinisaidia sana kurudi kwenye mstari. Zilinifanya nikaanza kuyaangalia baadhi ya mambo kwa mitazamo tofauti sana. Au kuwachukulia watu kwa namna ya kipekee pia.
Niliufurahia uhamuzi wa kurudi nyumbani kipindi kile. Maana niliondoka nikiwa mtu wa tofauti ....
πππ umenitoa usingizini mkuu. Unaweza kuwa punda na hujui.Yawezekana zikafanyika, ila siunajua kila mtu na technic yake. Hata kwenye mpira na mziki kuna ambao wapitia kwa wataalam. Japo sisi tunaamini vile ni vipaji π π π π
Chaiii???Chai ya 20 mbona nishaweka mkuu [emoji28][emoji28][emoji28]
Kosa la jamaa lipo....yeye ndo alikua muamuzi wa mwisho km bimkubwa atapeliwe ama Lah...alipozingua kule site mara ya mwisho alitakiwa achague upande(permanently),coz anayo namba ya bimkubwa,alipaswa amsanue,coz alijua kabisa bimkubwa amesha 'lay' trust kwake,so alijua kabisa akiwaachia wale wazee wampige mstaafu msala utamwangukiaImekukataje stimu? Mkubwa.
Unaambia kama una sikio la kufa basi tena ndio hivyo dawa hutoisikia.
Ndiyo huyo mstaafu sasa,
Sioni kosa la jamaa hapo.
Ishu hapa haikuwa ujanja bali dawa za kupumbazwaMstaafu alipewa ishara zote ila hakutaka kuzielewa ujue angekua Mtu mjanja angeshtukia mchezo mapema sana
π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£15th Portion:
.... Masharti ya zile dawa, ni kwamba, ili mambo yaende kama unavyotaka. Ukikutana na muhusika tu, kabla ya yote, sharti la kwanza lazima umpe mkono wenye ile hirizi. Akiupokea tu, anakuwa chini ya himaya yako.
Na endapo atakuwa katika mazingira ya kushindwa kukupa mkono, mfano amebeba vitu mkononi au hajataka kukupa mkono, basi unachotakiwa kufanya ni kumpiga piga begani mara mbili au tatu na ule mkono wenye hirizi ( in a friendly way, sio kumpiga kwa nguvu).
Ukifanikiwa kufanya kimoja kati ya hivyo (kumpa mkono au kumpiga piga bega), unagain access ya akili yake. Unachomwambia, lazima atekeleze. Kutokana na kutokuwa na uhakika na lile jambo kama ni kweli linawezekana, ndio maana nilichagua kwenda kwa Shani, maana kumshika mkono au kumpiga bega isingekuwa big deal.
Sasa nilivyofika kwa shangazi Shani, alivyoniona, kwanza akashangaa maana sikuwa nimempa taarifa kuwa naenda. Akaniuliza "Mwenzetu vipi, kuja kimya kimya bila taarifa, ndio umekuja kufumania?"
Nikamjibu "Tusalimiane kwanza basi mama". Alaf nikamsogelea na kumshika mabega yote mawili. Kwavile pete ilikuwa kidole cha mkono wa kulia, nikampiga piga kwenye bega lake la kushoto mara mbili, Kisha nikamwambia
Analyse: "Nimekumiss kipenzi"
Shani: "Kwenda huko, hakuna cha kunimiss wala nini, ni lile game ndio linakuzuzua, huishi kuja"
Analyse: "Wala sijaja sababu ya ilo game. Alaf afadhali umeliongelea, naomba basi leo niende nalo, hapa kwako halitumiki, mwishowe lijae kutu"
Shani: "Babu eeh, chukua ilo hapo uende nalo, maana unaweweseka kweli. Kila ukija mawazo yapo kwenye ilo dude tu"
Nikajikuta natabasamu tu.
Tukapiga story za hapa na pale huku tunacheck tamthilia pale. Msosi ulivyokuwa tayari nikala, kisha nikamla na yeye. Mida ya saa tano nikaaga niondoke. Nikapewa PS, nikaamsha nayo.
Wakati nipo njiani naelekea ghetto, uso umechanua kwa tabasam, najiuliza How is this possible?. Sema kuna wazo likaniambia, alishachoka kukaa nayo, ndio maana kakupa, wala sio hayo madawa yako.
Usiku wa siku hiyo hiyo, kabla hata sijafika gheto. Mzee Dingi alinipigia simu na kuniambia kuwa kesho inabidi tukutane wote kwa pamoja, lengo ni kuweka mambo sawa, na kukumbushana majukumu ya kila mmoja. Location ya kukutania, ni pale pale kinondoni. Akili ikaanza kuniambia Ili dili ni must win, jamaa hawataki liende mlama hata kidogo.
. . . ***** ****** ****** ******
Asubuhi na mapema, nikajisogeza eneo la kukutania. Tukakumbushiana umuhimu wa kila mmoja kutekeleza jukumu lake, lakini pia Mzee Dingi akatupa mrejesho wa maongezi yake na yule mstaafu, kwamba kila kitu kipo sawa, na hiyo siku ya kuonana nae ni ile ile.
Timu nzima ikawa inanisisitiza nihakikishe nakuwa mtulivu na mwenye kujiamini, maana nafasi yangu (mwenyekiti), ndio nafasi muhimu ya kumfanya mlengwa asiwe na wasi wasi kabisa.
Kikao kilidumu kama dakika 45 tu. Kisha tukatawanyika.
Binafsi kwa upande wangu sikuwa na amani kabisa. Nilikuwa nikiiangalia timu nzima tunaokutanaga, sikuwa na Imani na mgao utakavyokuwa. Nilikuwa nimeshaanza kutawaliwa na mawazo ya kudhurumiwa tu.
Sasa tulivyotawanyika, wazo likanijia nimfatilie Mzee Dingi hadi anapokaa. Nikishapajua kwake, itakuwa rahisi kudeal nao endapo watataka kunidhurumu, maana familia yake walikuwa hawajui ukweli kuhusu mishe zake kwahiyo ingekuwa rahisi kumtaitisha akiwa kwake. Maana alichowaambia nyumbani, ni tofauti na anachofanya.
Nikadhamiria kumfungia tela. Pale kinondoni Mimi na Mzee Dingi tukapanda wote gari za kwenda kariakoo. Tulivyofika, tukaachana. Nikawa kama naondoka, ila nikajibanza nimuangalie. Akapanda gari ya Mbagala, nikachukua pikipiki na kuanza kumfatilia. Alivyofika mivinjeni, akashuka, akapanda tena gari ya kurudi Kkoo. Nikaanza kujiuliza, huyu Mzee kasahau kununua kitu town au?. Alivyofika kkoo, akapanda gari za gongo la mboto, zikampeleka hadi bungoni, pale pia akashuka, akachukua gari za Tabata. Kumbe jamaa anakaa Matumbi pale. Inaonekana ndio mtindo wake kila akitaka kurudi kwake. Siku zote nilikuwa najua amehamia Mbagala, maana kila tukiachana lazima apande gari za kwenda kule.
Kutokea pale Matumbi aliposhukia, kuna kibao kinaonesha Matumbi Street, kipo upande ule ule alioshukia. Akaingia na kibao kilipokuwa kinaelekeza. nilimfatilia mdogo mdogo, akikata kona nipo, akavuka reli nipo. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, ni kama vile machale yalimcheza. Tulikuwa kwenye kichochoro kirefu, ambacho sikutaka kumpa distance kubwa, maana nilihisi akikimaliza naweza nikampoteza, njia ni vichochoro mno. Alivyokimaliza tu kichochoro, anageuka nyuma anakutana uso kwa uso na Mimi.
Alishtuka kinoma, akabana kibegi chake kwapani, nakuanza kukimbia. Sikulaza damu, nikaanza kumkimbiza, baada ya kile kichochoro, kulikuwa na nyumba mbili zimefatana. Akazipita akiwa speed kali, Mimi nilivyoipita ile nyumba ya pili, nasikia kitoto kinaitwa "Baba, baba". Kile kitoto kikaendelea "Mama, njoo umuone Baba kapapita nyumbani anakimbia". Akili ikaniambia kumbe hapa ndipo anapoishi, basi sina haja ya kuendelea kumkimbiza, atarudi tu.
Nilivyoisogelea ile nyumba kwa ukaribu, kale katoto kakanikimbilia "Anko, anko umekuja kwetu". Mama ake nae akatoka nje, tukasalimiana pale, akanikaribisha ndani, ila sikutaka kuingia, nikaomba kistuli nikae nje. Baada ya kama robo saa hivi, namuona Mzee Dingi anakuja kinyoonge. Alivyofika akanikata jicho tu, kisha akaingia ndani bila hata ya kunisemesha. Nikamsubiria atoke huku nikiwa natafakari na kupangilia maneno yangu kichwani.
Alivyotoka tu, nikasimama na kumpa mkono, akashindwa kuukataa japo alikuwa kafura, akaupokea. Alaf akaniambia tutoke nje ya lile eneo, kama vile hataki mtu mwingine aliyepo ndani au karibu na pale atusikie. Nikampiga piga piga begani na kumwambia kwamba asiwe na wasi wasi. Kiukweli, sikuwa na nia yoyote ovu na Mzee Dingi. Nilikuwa najua Mimi na yeye wote tuko sawa, maana mganga wetu ni mmoja. Hata ile kumpa mkono, na kumpiga bega, ni vitu ambavyo vilitokea naturally tu, siku tegemea chochote, na wala sikuwa na wazo lolote. Ila cha ajabu, baada ya kufanya vile, Mzee Dingi ghafla akawa submissive sana kwangu. Ule ukali aliokuwa nao machoni, na sura aliyokuwa kaikunja, vyote vikapotea. Nikabaki najiuliza, how come? Inamaana dawa zangu Mimi ziko strong kuliko zake au ni vipi?
Nakumbuka tulivyotoka nje ya eneo lake, aliniuliza "Unashida gani Apostle, mbona tunafatana mpaka nyumbani?".
Unajua kama nilivyosema hapo awali katika kile kikundi, hakuna aliyekuwa anajua wengine wanakaa wapi, au hata kuyajua majina yao halisi. Ni Mimi tu ndio nilikuwa namfahamu Mzee Dingi kwa jina la mtoto wake, na hii ni kwasababu tulishawahi kuishi nyumba moja. Yani hata ungetokea msala, atakayeshikwa ni ngumu kuwakamatisha wengine.
Nikajaribu kumwambia Mzee Dingi, "Nina matatizo ya kifamilia, nataka nimrudishe wife kijijini, akajifungulie kule, ila sina hata mia"
Mzee Dingi: "Kwahiyo unatakaje?"
Analyse: "Naomba unikopeshe kama 1.5m, utanikata kwenye dili letu likishakamilika"
Mzee Dingi: "Hayo ungeniambia kule kule, sio kufatana mpaka majumbani. Kwanza umepajuaje huku? Au ulinifatilia tokea mjini?"
Analyse: "Ilo la kupajua hapa halina umuhimu mzee, angalia namna ya kunisaidia"
Mzee Dingi: "Sina hiyo hela hapa home"
Analyse: "Kwahiyo unanisaidiaje? "
Mzee Dingi: "Nisubirie hapa nakuja"
Akaingia ndani chapu. Baada ya dakika chache akatoka. Akaita pikipiki, ikatupeleka mpaka maeneo ya Tabata T.I.O.T, kwenye ATM ya NMB, akatoa ile amount alaf akanipa. Kabla hatujaachana, Nikajaribu kumuuliza wahusika wote wa ule mchongo tuko wa ngapi?. Je ni wale wale ninaowaona au kuna wengine?
Hakuwa tayari kunipa details za maana, zaidi ya kusema wapo wengine wawili, ila hakutaka kuniambia uhusika wao kwenye ule mchongo.
Tukaachania pale pale, nikaelekea zangu ghetto.
Nikiwa nimebakiza hatua chache kuifikia nyumba niliyokuwa nakaa, Mzee Dingi akanipigia simu. Nilivyoipokea, hakutaka hata kunipa nafasi ya kuongea, alinitukana sana. Alinipa vitisho vya kila aina..
Namuuliza "Kwani kuna shida gani mzee?"
Mzee Dingi: "Unajifanya una akili nyingi sio? Nimeanza kuliona jua kabla yako, nitakuonesha. Usiponirudishia hiyo hela kama ulivyosema, nakuua"
Analyse: "Kwani si tumekubaliana nitakurudishia baada ya dili la yule mama kutiki?"
Mzee Dingi: "Ms*nge wee, huyo mke uliyemtia mimba umemtoa wapi, unadhani kuwa na mke kazi ndogo? We endelea kucheza na akili yangu, nitakuonesha"
Analyse: "Niwe na mke, nisiwe nae, hela yako utapata mzee, kuwa na amani"
Hakutaka kuendelea kunisikiliza, akakata simu.
Hisia zake zilikuwa sahihi, sikuwa na mpango wa kumrudishia ile hela, hata kama wasingenidhurumu.
Nikaingia zangu gheto.
** ***
Baada kuoga, nikaenda maeneo ya Segerea kula vizuri, kisha nikarudi tena gheto. Wakati natoka, simu niliiacha ndani kwenye chaji. Nilivyorudi, nikakuta missed call moja toka kwa Mshua, wakati naendelea kujiuliza nimpigie au la, simu ikaita tena. Mpigaji akiwa ni yeye tena.
Ile hali ya uoga dhidi yake, iliendelea kuwepo. Bado najiuliza, nitamwambia kitu gani?. Nafsi ilikuwa bado inanisuta, natokea nilivyoongeaga na yule Mzee wa Kongowe, sikuwahi kupokea simu ya Mzee wala kumpigia.
Ile simu iliita mpaka ikakata. Ilivyokata, robo saa baadae mama akawa ananipigia. Nikajiuliza, huyu ni Mama kweli ananipigia, au ni Mzee?. Sikuzote Mama akitaka kuongea na sisi, huwa anatubeep tu, na ikitokea umepokea ukala salio lake, basi hiyo ni kesi. So, akipiga badala ya kupokea, huwa tunakata then tunampigia.
Ila siku hiyo nilishindwa kuikata, maana sikuwa na uhakika na mpigaji. Kuikata, ni confirmation kuwa nipo karibu na simu. Na kama nipo karibu na simu why sijapokea simu ya Mshua?. Ikaita hadi ikakata yenyewe, then mpigaji akapiga tena. Badala ya kuikata, nikaamua kuipokea.
Nikawahi kujitetea "Mama sina salio ndio maana nimepok.....". Kabla hata sijamalizia, nasikia sauti ya Mshua;
Mshua: "Salimia kwanza"
Analyse: "Samahani Mzee, nilijua ni Mama, shikamoo"
Mshua: "Ni mwili mmoja, hakuna shida. Mbona hupokei simu zangu?"
Analyse: "Kila unaponipigia nakuwa mbali na simu, alafu Sina salio"
Mshua: "Kama vocha ya 500 inakushinda, unafanya nini huko mjini?"
Nikabaki kimya tu. Akaniuliza "Unaendeleaje? Kila kitu kipo sawa huko?". Nikamjibu "Ndio". Akawa kimya kwa muda, Kisha akasema "Sawa, kuwa mwangalifu usije kuwa kibaka huko". Akakata simu.
Msongo wa mawazo ukarudi upya. Ila nikaamua kujipa moyo, huku nikiwaza dili tunaloenda kupiga na hela itakayoingia. Nahitaji mtaji wa biashara, siwezi kurudi nyuma now, liwalo na liwe......
π€¦π€¦π€¦π€¦π€¦π€¦
Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Kwenye story ya mwanzo uliishia form four Hadi kipindi cha magu uko songea unalima...story hii umeendelea form six then chuo...umemaliza uko ktaa unapambana ni almost miaka 5 mbona time frame ya matukio haiconnect mkuuWaandishi wa vitabo wapo wengi tu, ila wanachoma hela kwenye utayarishaji na uchapishaji alaf wasomaji, wanunuzi wanaingia mitini. Wasomaji wengi wanataka Bure kama hivi mkuu π π π
wow thanks mommy πKasinge munooo mnywaniiii nimefikaaaa!! Ngoja niisome!
Bantu Lady Tayukwa baby zu Lovelovie mtzmweusi S V Surovikin Lastmost Unforgettable Restless Huster mmash come this way aposto katupia nyengeneee!!!!
Wewe ndio hauconnect matukio vizuri mkuu, unadeal na heading to. Mzizi wa ile story ilikuwa Mimi kudrop form four na kuingia kitaa, ila niliweka matukio menginea ambayo yalishawahi tokea, ili kusindikiza lengo la simulizi. Ila sikumaanisha mpaka moment naiandika nilikuwa form 4, ungesoma kwa makini, kwenye ile story kuna habari za chuo pia.Kwenye story ya mwanzo uliishia form four Hadi kipindi cha magu uko songea unalima...story hii umeendelea form six then chuo...umemaliza uko ktaa unapambana ni almost miaka 5 mbona time frame ya matukio haiconnect mkuu
Punguza lawama apostle kaunganishwa dili lingine na mzee Kesho yetuNilitaka kushangaa eti story iende mpaka mwisho bila excuses!!!!!! Labda sio humu!!! Ila kwakuwa ni ihari yake arudi hata mwakani .
Apostoo umenichota mchangaWewe ndio hauconnect matukio vizuri mkuu, unadeal na heading to. Mzizi wa ile story ilikuwa Mimi kudrop form four na kuingia kitaa, ila niliweka matukio menginea ambayo yalishawahi tokea, ili kusindikiza lengo la simulizi. Ila sikumaanisha mpaka moment naiandika nilikuwa form 4, ungesoma kwa makini, kwenye ile story kuna habari za chuo pia.
Kama ambavyo msingi wa story hii, nilitaka kusimulia mazungumzo yangu na yule Mzee wa Kongowe, lakini story yake pekee ingekuwa fupi, ndio maana nikajumuisha na matukio mengine yaliyowahi kutokea, mfano kina Mzee Dingi.
Nenda kasome tena ile story kule. Maana maswali mnayouliza ni Yale Yale kila siku. Ukienda kwenye ile story utakuta kuna mtu anauliza habari za chuo zimetokea wapi wakati inaonesha nilikimbia shule [emoji28][emoji28][emoji28].
Guys, humu nasimulia past. Ninachoandika now, hakimaanishi ndio current issue kwangu. Ww msomaji yawezekana usijue what next, ila Mimi tayari najua.
Asantee aposto nimefika!!
Wapii Bantu Lady Tayukwa leadermoe Lovelovie Njemba Soro Kigi Makasi kaburungu Unforgettable Kalpana Lastmost Tyrone Kaijage Mbobo mmash Restless Hustler mtzmweusi
Mtendaji wa kijiji tayari katupia