Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Aise nimecheka kinoma story nzuri
ila na mimi nikikumbuka nilimpeleka mzazi feki kutoka kwenye bar ya mbege duh jamaa alikuwa ananukia pombe hatari, ofisini naulizwa ndio baba yako nikasema ndio mwalimu alisizi kama 5 min hivi akituangalia tu ndio maongezi yakaendelea tukamaliza nikampa 10k yake moto.
Ila ujana bn tena wa shule, nimemiss zile hustle sana
[emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Mzee wa kichagga ananikumbusha February 2002 nikiwa f.6 nilipewa SPA siku tunarudi na wazazi mi nlienda na maza, kuna dent alimkodi jamaa pale Arusha mjini kama ndio kaka yake, kufika shule jamaa alintembezea kipondo cha maana, sasa baada ya maonyo ya wazazi na walimu tukaruhusiwa kuwasindikiza wazazi stendi, kufika njiani jamaa si wakazikunja!? Mi na maza tunashangaa kuuliza dent anasema yule jamaa hata sio ndugu yake kamkodi tu. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] hatar sn

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
5th Portion:

.... Akili yangu faster ikaniambia, hapa nitakuwa nimeleta mchepuko wa Mshua home, ndio maana Mama kazimia alipouona. Nikajisemea, nishaharibu hapa, tena siku ya kwanza tu kuja.

Nikamkimbilia Mama pale chini. Yule bi mkubwa akawa anakuja taratibu, Mshua nae akawa ametoka ndani. Tukawa tunampa huduma ya kwanza, huku Mshua ananiuliza "Imekuwaje akawa hivi?. Nikamjibu kuwa sielewi, na kiukweli sikuwa naelewa. Baada ya kumpepea pepea huku Mshua akimnawisha kwa maji ya baridi kichwani, Mama fahamu zikawa zinarudi taratibu.

Kipindi hayo yanaendelea, Mshua alikuwa anaongea na yule bi mkubwa niliyekuja kuja nae. Maongezi yao yalikuwa ya kawaida tu, lakini kila nikijaribu kumsoma Mshua kuona kama ana wasiwasi, ila namuona yuko neutral tu. Mama nae fahamu zilivyorudi kabisa, akapewa na maji akanywa. Alivyoona Mshua na yule bi mkubwa wanaongea kama watu wanaofahamiana, nikaona na yeye kazidi kupata ahueni. Ikabidi viletwe viti hapo hapo nje, ili bi mkubwa aendelee kupata hewa safi. Mshua akatoa utambulisho pale, nikaona Mama kumbukumbu juu ya yule bi mkubwa zikawa zimemrudia, kumbe na yeye alikuwa anamfahamu.

Baada ya chakula cha pamoja, yule bi mkubwa akaomba kuondoka maana anaratiba zingine. Mzee akamsindikiza. Huku nyuma nilivyobaki na Mama, nikajaribu kumuuliza alikutwa na nini mpaka kuzimia? Akanijibu "Acha tu, cha muhimu niko sawa sasa". Jitihada zangu za kumbembeleza aniambie, zikagonga mwamba, ikabidi nisalimu Amri.

***** ****** ******** ******* *******

Maisha yaliendelea vizuri pale nyumbani, likizo ilivyo karibia kuisha, nikaondoka.

Siku zikaenda, hatimae masomo yakafikia tamati. Nilipofanikisha kumaliza chuo, kabla ya graduation, Mzee akawa ameniita home. Siku niliyofika, hatukuongea mambo mengi, ila baada ya siku 3 ndio akaniweka kikao. Tukaongea mengi sana kuhusu maisha. Mwisho wa siku akaniambia "Ukirudi tena mjini, kuna mtu nataka ukaonane nae". Nikamuuliza ni nani? Akajibu "usijali, nitakupa namba yake, na namna ya kumpata. Anaweza kukusaidia maisha yako baada ya chuo". Nikamuitikia sawa. Lakini kimoyo moyo sometime nilikuwa namind, maana kama kunipa namba yake ya simu na hizo taarifa zake, angeweza kunipa hata kwa njia ya simu nikiwa Dar.

Nilivyotaka kurudi Dar, alinipa ile namba ya huyo mtu, Kisha akaniambia mengine nitayapata nikishaongea nae, maana anatarajia simu yangu. Nikarudi zangu mjini.

Baada ya kama siku tatu tokea nifike mjini, nikampigia yule mtu. Akanitambua vizuri, Kisha baada ya mazungumzo machache, akasema atanitafuta, akitulia. Nilikaa wiki nzima, hakunicheki. Mshua kuna siku akaniuliza kama nilimtafuta yule mtu, nikamjibu "Ndio, ila alisema atanitafuta akitulia, ila amekuwa kimya". Mzee akaniambia mtafute tena.

Nikampigia tena, hakupokea. Kesho yake nikampigia tena, alivyopokea akaniuliza "Nani mwenzangu?", Ikabidi nijitambulishe upya, alivyonikumbuka, akasema alibanwa na shughuli alafu pia namba yangu hakuwa ameisave, ndio maana alishindwa kunitafuta. Nikamjibu aina shida Mzee. Akaniuliza "Siku gani unakuwa na muda?", Nikamjibu "Kila siku". Akacheka kidogo, alafu akasema atanipigia mwishoni mwa wiki, ili ikiwezekana tuonane.

Ilivyofika mwisho wa wiki, nikasahau makubaliano na yule Mzee, nikajikuta nimemualika mpenzi wangu gheto. Wakati tupo pale, Mzee akapiga simu. Ugomvi wangu mkubwa na huyu binti ilikuwaga simu, alikuwa hataki kabisa tutumie simu tukiwa pamoja, labda mpaka aondoke. Kwahiyo akijaga, simu tunaziweka silent, alaf zinakaa juu ya meza. Yule Mzee alipiga mara 3, zote sikuweza kuzisikia. Nilikuja kuziona zile missed calls jioni sana. Nilipojaribu kumpigia hakupokea. Nikatulia. Baada ya wiki, Mshua akanipigia simu kuuliza kama niliongea na yule mtu, ikabidi nimuelezee hali halisi ilivyo. Baada ya kunisikiliza mpaka mwisho, akaniambia "Tukimaliza kuongea na simu, jaribu kumtafuta tena". Ikabidi nimuulize Mshua, yule Mzee ni nani haswa? Na kwanini natakiwa kumcheki?

Mshua: "Huyo ni mtu wa huku kijijini kwetu, ni kama ndugu yetu. Anafahamiana na watu wengi huko mjini, anaweza kukusaidia"

Analyse: "Ila hapokei simu, alaf ni kama vile hataki huu ukaribu unaojaribu kuuweka"

Mshua: "Ila ni mtu anayeweza kukusaidia, ngoja nikuelekeze kwake, ili umfate kule"

Mshua akanielekeza, lakini sikuwa comfortable kabisa kwenda. Mtu kama simu hapokei, ukienda kwake siutaishia getini?. Nikaamua kumpigia simu siku hiyo hiyo, ili kama kesho nitaenda, basi awe anautarajia ujio wangu. Nilivyopiga, simu ikaita kidogo, alaf ikakatwa. Akanitumia msg "Nipo kwenye kikao, nitakupigia nikitoka. Nani mwenzangu?"

Ile msg ilinifanya nijisikie vibaya na huu undugu wa kufosi. Mzee kila siku ananiuliza Mimi nani?. Sikuijibu ile msg, nikajisemea, kama akinipigia baada ya hicho kikao, sawa. Asisipopiga, simtafuti tena. Yule Mzee hakupiga. Nikampotezea.

Nikaendelea na harakati zingine za utafutaji. Siku, wiki, miezi ikapita. Mshua hakuwahi niuliza tena kuhusu yule Mzee, na hata ilipokuwa tukiongea, hakuingizia ilo swala. Baada ya miaka kama miwili au mitatu kasoro, nikawa nimedhamiria swala la kwenda kumtambulisha mwanamke nyumbani, ili mambo yakienda sawa, siku zijazo nioe.

Na wazo ilo lilitokana na msukumo niliokuwa nao ndani yangu, maana nilikuwa nishaanza kuingiwa na uvivu usio wa kawaida. Kupika, kufua, usafi nk. Yani kiufupi kazi zote za ndani kwangu zilikuwa mzigo. Tatizo pekee nililokuwa nalo, mwanamke ambae nilikuwa nae kwenye hayo mahusiano kwa wakati huo, kila nikimwambia issue ya kumtambulisha nyumbani, anasita sita. Kwamba tusubirie kidogo, mara tuzae kwanza ajifunze malezi. Binafsi sikuwa na mpango wa kuzaa nae bila kuwa tumeoana, maana kama tukishindwana, sitaki nitakae kuja kumuoa nimpe lundo la watoto wasio wake. Baada ya kujadiliana nae kwa kina, mwisho wa siku tukawa tumekubaliana kuanza hizo process.

Nilivyofikisha hiyo taarifa nyumbani, kila mtu aliipokea neutral, hakuna aliyekuwa na shauku au furaha nayo. Mama akaniambia niendelee kujipanga kwanza kimaisha.

Analyse: "Ila Mama, maisha ndio haya haya, hakuna jipya, mambo mengine yatakaa sawa mbeleni"
Mama: "Ni sawa mwangu, pia nakuombea sana heri, ila huoni kama ungesubiria kidogo?"
Analyse: "Nisubirie nini tena Mama? Hutaki kuitwa mkwe?"
Mama: "Nataka sana mwanangu, tena kati ya wanangu ambao natamani kushuhudia harusi yao ni wewe mwanangu"
Analyse: "Basi niruhusuni nimlete mumfahamu Mama"
Mama: "Kusema ukweli naogopa mwanangu. Naogopa sana sijui utaniletea mwanamke wa aina gani, maana kuna muda akili zako unazijua mwenyewe. Hata ile siku niliyopatwa na mshtuko, akili yangu iliniambia yule mwanamke uliyeongozana nae ndio umekuja kumtambulisha"

Nilichoka. Nikajikuta nimekaa kimya kwa muda, nisijue cha kusema. Kumbe ile ndio sababu ya Mama kupata mshtuko?. Yani familia zingine wakisikia watoto wao wanataka kuoa inakuwa furaha, kwa upande wangu naleta wasi wasi? Vijana wenzangu wakiongozana na wamama, wakawasaidia mizigo, wanaonekana vijana wa heshima, Mimi Mama yangu kuniona nimeongozana na mmama, kapatwa hadi namshtuko? [emoji1751][emoji1751][emoji1751][emoji1751]....

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu. Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Familia nzima Washakuona una uraibu wa mishangazi[emoji38]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
21st Portion:

...Nyumbani nilipokelewa vizuri tu, tena kwavile safari walijua nimekuja kuwaangalia sababu ya ugonjwa wa Mama, hivyo Mshua hakuwa mkaksi kwangu. Hali ya Mama ni kweli haikuwa nzuri, alikuwa haishi kulalamika maumivu na vichomi vya mara kwa mara. Mwanzoni walivyompeleka hospitali, alipewa tu dawa ambazo walidhani zingeweza kulitatua tatizo lake. Ila alitumia mpaka zikaisha, ila tatizo likaendela.

Nilivyofika ikabidi nishauri turudi tena hospital kwa uangalizi zaidi. Na kweli tulivyoenda tena, wale madaktari baada ya vipimo vyao, wakasema Mama anasumbuliwa na appendix na kwa stage iliyofikia, inatakiwa afanyiwe upasuaji haraka sana. Binafsi nikishasikia habari za upasuaji, huwa naichukulia kama habari nzito hata kama ni upasuaji mdogo. Ikabidi tushauriane kama familia nini kifatie, maana Kwa mazingira ya hospital ya pale kijijini, haikunipa amani kabisa kuwaruhusu wamfanyie upasuaji Mama. Mshua akabisha bisha sana pale, Mama nae asivyopenda kusafiri, akawa anasisitiza tufanyie pale pale. Kwavile watoto tuko wengi kuliko wazazi wetu, mawazo yetu ndio yakapita, kuwa upasuaji usifanyikie pale kijijini.

Baada mjadala huo kuisha, ukaibuka mjadala wa hospital gani aende. Nikashauri twende Bugando Mwanza, kwanza ni karibu lakini pia pale Mama atakuwa chini ya uangalizi mzuri wa Dada. Mshua akashauri twende Dar, kule huduma ni nzuri na kuhusu sehemu ya kufikia atafikia kwangu.

Analyse: "Kule Mama hawezi kuwa comfortable tofauti na kwa Dada"

Mshua: "Kwanini asiwe comfortable?"

Analyse: "Sasa unadhani Mimi na wewe tutaweza kumpa uangalizi mzuri kuliko Dada?"

Mshua: "Kwani mpaka tumuangalie Mimi na wewe?"

Analyse: "Sasa nani mwingine atamuangalia?"

Mshua: "Mkeo"

Analyse: "Mke yupi Mzee?. Sina mke mjini Mimi"

Mshua: "Huna mke, au huwa anakuja na kuondoka?"

Mama: "Nyie mkishaanza kubishana hapo, mpaka apatikane mshindi Mimi ntakuwa nishajifia hapa"

Ikabidi mazungumzo na Mshua yakome kwa muda. Tukaadhimia Mama aende Bugando. Tulisafiri nae mpaka kule, Mshua yeye alibaki. Kufika Bugando tukawaelezea tuliyoambiwa hospital kule kijijini, tukawapa na makaratasi ya vipimo vyao walivyofanya. Wakayasoma, kisha wakashauri afanyiwe vipimo upya, baada ya hapo ndio taratibu zingine zifatie.

Majibu ya vipimo vyao pale Bugando yaliporudi. Mama akaonekana hana tatizo appendix, isipokuwa kwenye mifupa ya nyonga uloto ndio umepungua (sababu ya umri), hivyo mifupa inasagana na kumletea maumivu. Akapewa dawa na ushauri wa baadhi ya vyakula anavyotakiwa azingatie, Kisha tukaruhusiwa. Hakufanyiwa upasuaji. Tukaendelea kukaa Mwanza, tukishangaa Jiji kidogo. Mshua akawa anataka turudi;

Mshua: "Ameshapewa dawa, fanya mpango arudi sasa"

Analyse: "Ngoja walau tufanye utalii kidogo kwa wiki hii kisha tunarudi"

Mshua: "Umenisikia vizuri nilichokwambia?. Nimesema fanya mpango Mama arudi, wewe hata ukiendelea kukaa mwaka, Sina tatizo"

Sister: "Lakini Baba, ungemuacha hata siku chache, huko anawahi kufanya nini?"

Mshua: "Hivi nyie sijui hata kama mnanielewa. Yani mnanipangia juu ya mtu ambae mmezaliwa mkanikuta nae?. Nimesema namuhitaji mke wangu"

Tulianza tunajadiliana kawaida tu, ila Mshua akaenda anabadilika mdogo mdogo. Kesho yake tukarudi nyumbani. Home Sweet Home.

Mshua: "Kwahiyo hawa madaktari wa hapa kijijini walikuwa wanataka kufanyia mazoezi mwili wako?"

Mama: "Yameshapita hayo, makosa hutokea"

Mshua: "Ni kwavile huo upasuaji haukufanyika tu, ila nadhani wangeomba uhamisho. Lakini hata hivyo lazima niwafate tukaambizane ukweli"

Analyse: "Hata ukiwafata itabadili nini, acha tu yapite"

Mshua: "Ili limepita, lakini maradhi hayaishi kuja, nataka siku nyingine wakiiona hii sura, wakumbuke notsi zote walizosoma hadi wakahitimu"

Nikamkubalia tu, then nikaingia jikoni kutaka kusaidia kupika maana hatukula njiani. Mshua akaniambia nijipikie mwenyewe tu, maana chakula cha Mama ameshakipika. Nilijua asingeniruhusu kula kile chakula, ila nikamjaribu tu;

Analyse: "Lakini wote tumetoka safari"

Mshua akacheka kwanza, "Yani ninunue mahitaji yote humu ndani, pia nikupikie. Huyu ni mke wangu"

Analyse: "Na Mimi ni mwanao"

Mshua: "Nani kakwambia?. Una uhakika gani wewe ni mwanangu?. Ukiachana na sisi kufanana maana hata Mimi na Mama yako tunafanana, una ushahidi gani mwingine?. Huyu ni mke wangu, ukitaka cheti Cha ndoa kipo, wasimamizi wapo. Wewe unachochote cha kuthibitisha wewe ni mwanangu?.

Mama yeye anacheka tu, wala hachangii chochote. Mshua najua alikuwa katika mood ya utani, lakini kwenye mood ile ile ya utani, nilikuwa na uhakika kile chakula siwezi kula, otherwise mood yake ingechange. Maana nakumbuka kipindi niko O level, Mshua alikuwa na kawaida ya kutupikia. Tukitoka shule tunakuta chakula tayari. Ilitokeaga nikasingiziwa mimba, Mshua alimaindigi kwamba anatupikia chakula (Mimi na mdogo wangu), tukishiba tunaenda kusumbua watoto wa watu. Alisema hatokaa atupikie tena maana tushakuwa vidume. Japa lile soo, baada ya mtoto kuzaliwa iligundulika sihusiki, ila Mshua aliendelea kunimaindi, yeye msimamo wake siku zote ilikuwa mwanamke hawezi kukusingizia mimba kama hujalala nae.

Nikaingia zangu jikoni kupika.

***** ****** *****

Siku zilisogea sana, nilikaa takriban mwezi na nusu. Mpaka jioni moja Mshua aliniomba tuongee mida ya usiku shughuli za nyumbani zikiwa zimepoa.

Siku hiyo hiyo, baada ya kula chakula cha usiku, tukaenda kukaa nje kwenye bustani. Tukiwa pale nje akaniuliza "Vipi unashida gani safari hii?"

Nilikaa kimya kwa muda, nilikuwa najaribu kutafakari, nianzie wapi kumuomba msamaha? Au nifunguaje haya mazungumzo?

Alivyoona nipo kimya sana, akabaki ananiangalia tu bila kusema chochote. Kisha akanyanyua simu yake, na kuniuliza:

Mshua: "Najua unatatizo, vipi niende ndani, alaf tuongee kwa njia ya simu?

Nikatabasam tu.

Analyse: "Nilionana na yule Mzee"

Mshua: "Aliniambia kuwa ulienda shambani kwake"

Analyse: "Kwanini hukuwa niambia yeye ni nani, au mipango uliyokuwa nayo juu yangu?"

Mshua: "Unadhani hiyo ingeweza kubadili kitu?"

Analyse: "Sio kubadili kitu tu, bali ingebadili maisha yangu yote"

Mshua: "Kwani sasa hivi huwezi kubadili hayo maisha yako?"

Analyse: "Sio kiwepesi kama ambavyo ingekuwa mwanzo"

Mshua: "Unapenda kufanya mambo kiwepesi au kwa njia ulizochagua wewe?

Analyse: "Hakuna anayependa kupita njia ngumu, ni matokeo tu ya machaguo yetu ndio yanaweza kutupitisha huko"

Akakaa kimya kwa muda. Alaf kabla hajaongea chochote, nikaona niutumie ule ukimya kumuomba msamaha.

Analyse: "Najua nimeku disappoint sana, nimefanya maamuzi mengi ambayo yameuvunja sana moyo wako na wangu. Ila...."

Kabla sijamalizia, akanikatisha.

Mshua: "Mimi ndio mwenye makosa hapa. Kama kuna anayetakiwa kuomba msamaha kwa kuivunja mioyo yetu, basi ni Mimi"

Akaendelea:

"Unajua katika maisha yangu, sikuwahi kabisa kufikiria kujiunga na jeshi. Ndoto na mipango yangu mingi ilikuwa sehemu nyingine kabisa. Mimi kujiunga na jeshi, ilikuwa ni ndoto ya Babu yako, yeye ndiye aliyenipush sana kuingia kule, japo nilikataa kwa nguvu zangu zote.

Kama ilivyokuwa kwako, nilivyomalizaga kidato cha nne, sikutaka kuendelea zaidi, nilitaka kuwa mfanyabiashara, ila Babu yako alitaka niendelee zaidi, ila kwa kupitia jeshini. Palitokea sintofahamu nyingi kati yetu, hadi ikapelekea Mimi kuondoka nyumbani na baadhi ya mifugo yake

Siku niliyorudi nyumbani, japo nilirudi na zaidi ya nilichoondoka nacho, ila Babu yako hakutaka kunipokea. Ilibidi wazee wa Kijiji wahusike katika kutupatanisha. Pamoja na adhabu ya bakora nilizopogwa mbele yao, Babu yako aliweka sharti la Mimi kujiunga na jeshi, hapo ndio ataweza kunisamehe kabisa na kunichukulia tena kama mwanae.

Sikuwa na jinsi, ilibidi nikubali, japo kutoka moyoni nilijenga chuki na yeye, kwa kunilazimisha kitu nisichotaka. Nilivyoingia jeshini, baada ya muda nikachaguliwa kwenda kozi Urusi. Hapo kidogo ndio nikaanza kulipenda jeshi. Kabla sijaondoka nchini, Babu yako akataka niache nimeoa kabisa. Hapo ukatokea ugomvi mwingine, maana sikuwa tayari kwa jambo lile kwa muda ule.

Nikaambiwa kama sipo tayari kuoa, basi inabidi niache nimechumbia. Pia nikakataa. Wakati najiandaa na safari, Babu yako akaniambia atamchumbia mwanamke kwa niaba yangu. Nikamwambia sitomtambua. Nikaondoka tukiwa hakuna maelewano mazuri.

Nilivyohitimu na kurudi Tz, nilikuwa sitaki kwenda kusalimia nyumbani, maana ningekabidhiwa mke ambae sio chaguo langu. Nilikuja kupata matatizo ya kiafya jeshini, kwa mara nyingine tena Babu yako akaingilia kati kinyume na matakwa yangu, nikajikuta rasmi nimetoka jeshini. Nilivyorudi nyumbani, mwanamke niliyechaguliwa na Babu yako, ndio akapewa jukumu la kuniuguza kwa ukaribu. Kitendo cha kuwa nae karibu kwa muda mwingi, kikajenga mazoea kati yetu. Nikajikuta naanza kumkubali."

Kufikia hapo nikaanza kujiuliza maswali, huyu mwanamke anayezungumziwa hapa ndio Mama yetu au? Ikabidi nimuulize,

Analyse: "Huyo mwanamke aliyekutafutia Babu, ndio Mama?"

Mshua: "Ndio. Kwani vipi?"

Analyse: (nikacheka kidogo) "Kumbe ulitafutiwa mke na Babu?"

Mshua: (akanikata jicho) "Acha dharau kijana, kuna baadhi ya mambo yako nje ya upeo ,huwezi kuelewa sawa?"

Nikawa, mpole, Kisha nikawa najizuia kucheka. Mwisho wa siku tukajikuta wote tunacheka [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

Akaendelea na story:

"Kabla afya yangu haijatengamaa vizuri, ile biashara aliyopanga kunipa Babu yako, ikapata ajali ya moto. Nikajikuta sina kazi, Sina kiwanda. Hapo ndio hasira juu ya Babu yako zikazidi. Nikaamua kuondoka pale kijijini, na kwenda mbali nao kuanzisha maisha yangu mengine, kivyangu, bila wao. Mwaka 82 nikaamua kumuoa rasmi Mama yenu, kipindi ana ujauzito wa dada yenu.

Majukumu yalipozidi kuongezeka, ikabidi nisogee sehemu za mbali zaidi ili kutafuta kipato. Niliamini umri niliokuwa nao, ndio wakati sahihi wa kupambana. Hakuna sehemu katika hii nchi ambayo sijafika. Nimenusulika kufa mara kadhaa huko migodini, nilishawahi kufukiwa hadi na kifusi. Huu mguu niliomia kipindi nipo jeshini, katika harakati za utafutaji, umeshavunjika tena mara kadhaa. Lakini pamoja na yote hayo, sikufikiria ku-make peace na Babu yako.

Sikuwahi kuwasiliana nae wala kurudi tena pale kwake. Kwa muda mrefu nilikuwa nikimchukia kwa maamuzi aliyoyafanya juu yangu, maana ni kama yaliniharibia maisha. Nilitamani sana angesimama upande wangu, au kusimamia yale niliyojipangia, na sio kunilazimisha kuwa vile anavyoona yeye inafaa.

Ila Mwenyezi Mungu ana njia nyingi sana za kutuonesha mambo ambayo sio rahisi kuelezeka. Hata uwe na moyo mgumu kiasi gani, akiamua kukufikishia ujumbe wake, basi jua atakufikishia tu, hata kwa namna ambayo hukuitarajia

Baada ya miaka mingi kupita, chuki na hasira juu ya Babu yako zikiendelea kuwepo. Alikuwa akinitafuta na kunitumia barua kupitia kwa wafanyabiashara waliokuwa wanatembea vijiji kwa vijiji, ila sikuwahi kumuandikia chochote. Ujumbe wangu nilikuwa naurudisha kwa mdomo tu, japo wahusika waliufikisha.

Mwenyezi Mungu akaamua kunionesha jambo. Mimi nilizaliwa kabla ya Uhuru wa nchi hii, ila macho yangu yangu yaliendelea kuwa gizani kwa muda mrefu.

Ile siku ambayo wewe uliyozaliwa, ndio siku ambayo macho yangu yalianza kuona. Ujio wako, ulifanya hasira zote nilizokuwa nazo juu ya Babu yako kufutika. Pengine usingezaliwa, ningeendelea kuwa kipofu, japo macho yangu hayakuwa na tatizo. Ningeendelea kuamini nipo sahihi"

Sikuelewa anamaanisha nini, ikabidi niendelee kumsikiliza. Hapo ndio akanifunulia kurasa za kitabu ambacho sikuwahi kukisoma kabla. Kurasa ambazo zilikipa thamani kubwa sana kile kitabu. Kurasa zilizofanya niyatazame baadhi ya mambo, kwa mtazamo tofauti kabisa....
Mzee wako ni comedian ni vile hajui tu [emoji23]
 
6th Portion:

.... I was a bit disappointed. Tukaongea story zingine mbili tatu, alafu tukaagana. Niliendelea kulifikiria lile swala, mwisho wa siku nikadhamiria nijipange Kisha niende mpaka kijijini, walau nipate kuongea nao ana kwa ana, maana dhamira yangu ilikuwa thabiti. Tofauti na wao walivyohisi, Mimi sikuwa napanga kuoa shangazi, kuna binti nilikuwa nae kwenye mahusiano ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa serious.

Wiki moja baadae, sister angu akawa ameniita niende kumtembelea Mwanza, lakini pia aweze kuniunganisha na mchongo fulani. Nilivyoenda akafanikisha kuniunganisha na ilo deal, japo halikuwa na muda mrefu, maana nilikaa kule takriban mwezi mmoja.

Kumbe ukiachana na huo mchongo, sister alikuwa na mission nyingine. Nyumbani, wazazi walimpa jukumu la kumfahamu mwanamke wangu, Kisha awape taarifa. Sister nae alichokosea, badala walau aniulize, akawa anapitia simu yangu kimya Kimya. Simu yangu haikuwa na password, fingerprint wala patterns, so ilikuwa rahisi kuaccess information.

Katika mapenzi kuna muda wapenzi huwa wanachatig ujinga ili kusogeza siku. Sasa kuna chatting fulani nilikuwa nachat na shangazi, kiutani utani nilimwambiaga "Yani wewe ningefanikiwa kukuoa, ningekuwa na raha sana", ilikuwa ni chatting za kupoteza muda tu, ila sister akaichukulia serious. Na kwenye gallery alikuta picha zake kadhaa, akajirushia Kisha akakausha, maana hakuwa na namna ya kuniambia, kwasababu info amezipata kwa njia isiyo halali.

Siku zikaenda, na ule mchongo ukafika tamati, nikarudi Dar. Sasa kuna siku yule shangazi alitaka nimpost kwenye status, baada ya kuvutana sana, nikaona isiwe case, nikawahide watu wote muhimu, Kisha nikampost nakuweka caption ya kawaida tu. Sasa kumbe sister alikuwa ameinstall Whatsapp mbili kwenye simu yake, na Mimi sikugundua. Akaiona ile status. Nashangaa kuona amereply "Mdogo wangu ndio maana hata uleje haunenepi, mzigo wote huo kweli?"

Ikabidi nijaribu kumkataa:

Analyse: "Huyo ni Mama wa rafiki yangu"
Sister: "Kwenda huko, niliona picha zenu kwenye simu yako, nikahisi ni yaliyopita, kumbe ndiyo yaliyopo?
Analyse: "Haipo hivyo dad... "
Sister: "Huyo ndio mwanamke unataka kumpeleka nyumbani bila aibu? Hivi akili zako zipoje lakini?"

Ikabidi nikaushie msg zake, akaamua kunipigia simu, alinisema sana siku hiyo, hadi nikahisi kizungu zungu. Nikaanza kujihisi sasa hapa nilipofikia pashakuwa pabaya, wanaonizunguka wote hawana utulivu wala amani, inabidi niachane na haya mambo sasa.

Hata lile wazo la kumpeleka yule binti home, ikabidi nilisimamishe kwa muda. Maana mazingira hayakuwa supportive tena, na Kwa jinsi ninavyomjua Mshua, panaweza pakatokea ngumi nikienda, alaf sikutaka tufikie huko.

Huyu manzi, kipindi namwambia nataka nikamtambulishe nyumbani, alikuwa anasita sita, mara aseme nivute subira kidogo, muda bado. Alivyosikia nimesitisha kumpeleka nyumbani, ukawa ugomvi sasa, maana akawa ana push sana nimpeleke, hadi nikawa najiuliza, hiyo subira aliyokuwa anasema niivute, imekatika au?.

Fast forward kidogo. Niliendelea kufanya mishe zangu za kuunga unga mjini, huku nikipata nafasi, nazungusha bahasha maofisini. Pale gheto nilipokuwa nimepanga, kuna Mzee fulan smart, amechomekea muda wote, ni mtu mzima, ila hana mvi hata moja, panki lake muda mwingi limepakwa super black, nae alikuwa amepanga pale. Sema tofauti yetu, Mimi nilikuwa nimepanga chumba kimoja, yeye alichukuwa vyumba viwili na sebule, maana alikuwa na familia.

Mzee sikuwa na mazoea nae sana, hata jina lake halisi nilikuwa silifahamu, nilizoea kusikia mkewe anamuita baba fulani (jina kapuni), au vijana wengi pale mtaani walipenda kumuita Mzee Dingi (na Mimi humu nitapenda kutumia ilo ilo jina la Mzee Dingi). Huyu Mzee kwa mtazamo wa nje, alikuwa na muonekano fulani wa kimamlaka, yani ukimuona tu kwa mara ya kwanza, unahisi atakuwa mtu mzito au yupo kitengo nyeti somewhere. So, kutokana na mambo yangu kuwa magumu, nikapata wazo la kuongea nae, pengine anaweza akaniunganishia mchongo wowote hapa mjini. Siku ya siku nikamkabili, ilikuwa siku ya jumapili, maana huwa anashindaga home tu.

Nilivyomuelezea shida yangu, kabla ya yote akaniuliza kwanini nimemfata yeye?. Nikamjibu nimejaribu tu, maana siwezi jua nani anaweza nisaidia, maana mjini Sina connection ya maana. Mzee Dingi akaniuliza elimu yangu na taaluma niliyonayo. Nikajielezea vizuri pale. Tukaongea mambo mengi, mwishowe akaniambia, kesho nivae vizuri, Kisha nimpigie simu anielekeze nitakapomkuta. Tukabadilishana namba za simu, nikarudi ghetto kwangu.

Kesho yake nikajiandaa vizuri, Kisha nikampigia simu anipe direction. Akanielekeza niende mpaka city center, maeneo ya Samora, kuna bustan fulani ipo opposite na NBC, nimsubirie pale. Nikabeba copy za vyeti vyangu kwenye bahasha, nikaanza safari ya kuelekea town. Nilivyofika, nikamjulisha, akaniambia nimsubirie atakuja. Nikatulia.

Nilikaa sana pale, karibia masaa mawili, Mzee hajatokea, wala hajanicheki. Sema sifa kubwa ya jobless ni uvumilivu, nikaendelea kuvumilia. Baada ya muda, pembeni yangu alikuja akakaa jamaa, ambae alionekana kama Yuko stressed hivi. Kila muda anapiga simu, na ukimuangalia vizuri kama anataka kulia. Sasa katika kupoteza time maana nilikuwa bored, nikajikuta namuuliza kilichomsibu. Jamaa ndio kunipa story kuwa huwa anafanya biashara ya mkaa, analeta na kuuza kwa jumla, kisha anarudi mkoani. Hii ilikuwa ni trip yake ya kwanza tokea aanze biashara kwa upande wa Dar, mzigo wote umekamatwa na maliasili maana pia alikuwa amebeba vitu ambavyo hakuwa na vibali navyo, So upo kituo cha polisi. Haelewi afanye nini, na wale waliomshika, wanataka mpunga mrefu ili aachiwe. Ndani ya muda ule mfupi, alijikuta tu ananiamini, tukawa tunaongea kama watu ambao tumefahamiana kwa muda mrefu.

Binafsi sikuwa na cha kumsaidia, nikabaki nampa pole na kumtia moyo tu. Ghafla Mzee Dingi akawa amefika, nikanyanyuka kumsalimia, alafu nikawa nasubiria anioneshe direction tunayoenda, ila yeye akawa amemakinika sana na yule jamaa niliyekuwa naongea nae. Akaniuliza "Huyu mwenzako ana Nini?". Nikashangaa kwann amemuita mwenzangu, ila sikujali sana, nikampa briefly tu.

Baada ya kuisikia story ya jamaa, pale pale Mzee Dingi akasema anafahamiana na mwanasheria ambae alishamsaidiaga rafiki yake kwenye mzozo na maliasili. Akamwambia yule jamaa aongozane na sisi wakati yeye anampigia simu mwanasheria. Kilichonishangaza, wakati tunaondoka, ile simu aliyopiga, ikaita kwa Mzee mwingine ambae alikuwa eneo lile lile anakunywa kahawa, sema kakaa benchi jingine. Yule jamaa wa mkaa hakuusoma mchezo, sijui ni stress au vipi.

Mzee Dingi aliongea huku simu kaiweka loudspeaker wote watatu tunasikia, mwisho wa siku mwanasheria akasema yupo maaneo ya stesheni,kuna mgahawa anapata chai, so tumfate pale. Tukaongozana Mimi, Mzee Dingi na jamaa wa mkaa. Stesheni kuna mgahawa upo unaface stand direct, ndio tukaingia hapo. Tukamkuta huyo mwanasheria, nilivyoiangalia ile sura, ni Mzee ambae tokea nilivyofika kwenye bustan pale Samora, nilimkuta, muda wote alikuwa anasoma gazeti, story kidogo huku anakunywa kahawa. Yani kiufupi hakuwa na haraka yoyote. Ila tulivyomkuta hapo kwenye mgahawa, akatwambia tuongee tunachotaka kuongea, hana zaidi ya dakika 15, anawahi mahakamani.

Kuna kengele Fulani ikalia kichwani mwangu. Zilipigwa sound za kutosha pale, sound nyingi sana. Mpaka ikafikia hatua, yule jamaa wa mkaa akahitajika kutoa laki 5 ili issue yake iwe solved siku ile ile. Jamaa wa mkaa akawa anajaribu kubargain yule mwanasheria feki akanyanyua briefcase yake akatishia kuondoka, Mzee Dingi akawahi kumtuliza kuwa amsaidie jamaa issue yake, jamaa nae kwa kuhofia kupoteza mtu wa kumsaidia, akakubali kutoa hiyo 500k. Pale pale akili ikaniambia, kuna mtu anatapeliwa muda sio mrefu.

Kati ya wote pale, yule jamaa wa mkaa, alionekana kuniamini Mimi kuliko wengine. Hata ile 500k waliyokubaliana atoe, akanitupia Mimi jicho fulani kama vile kuomba ushauri au kuuliza atoe au asitoe?. Kwa mazingira yalivyokuwa, nikajikuta nampa ishara atoe hela, asiwe na wasi wasi, ila nafsi ilikuwa inanisuta sana.

Wote wanne, tukatoka nje ya ule mgahawa, tukapanda gari ya yule mwanasheria, mpaka ATM, jamaa wa mkaa akatoa hela. Kisha tukarudi mpaka karibu na jengo la mamlaka ya bandari, kufika pale, yule mwanasheria na jamaa wa mkaa wakashuka na kuingia ndani, Nia ni kwenda kuandikishiana hela walizipeana, then ndio waende polisi. Baada ya dakika kama 15, yule mwanasheria akarudi peke yake, akazama kwenye gari haraka, Mzee Dingi akang'oa.

Akili yangu ikawa wazi, kuwa Mzee Dingi ni tapeli tu, yeye na mwenzie. Ikabidi nivunje ukimya ndani ya gari, kwamba kilichafanyika haikuwa haki. Hakuna aliyenijibu, Mzee Dingi akapaki gari kituo cha mnazi mmoja pale, then Mzee Dingi akawa ananiambia "Bahasha wanazunguka nazo vijana wanaotafuta kazi, wewe umeshapata kazi tayari, tafuta briefcase au begi la kubeba mkononi, kesho usije tena kazini na hiyo Bahasha". Nikamwangalia yule Mzee, hana hata chembe ya huruma au kujutia. Yule mwanasheria feki, akaniuliza "Kwani bwana mdogo unachotaka hasa ni nini?". Nikamjibu " Tumrudishie jamaa hela zake". Mzee Dingi akadakia "Sikia apostle, Ungetaka kumsaidia, ungemsaidia kipindi tupo pale mgahawani, acha kutia huruma wakati hela unaitaka"

Nikajikuta hasira zinazidi, hasa alivyoniita apostle, maana ilikuwa ni kama kebehi fulani hivi. Yule mwanasheria feki kwenye ile 500k, yeye akachukua 200k, Mzee Dingi akapewa 200k, alafu akachukua 100k na kunikabidhi Mimi,kisha akanipa na namba ya simu kwenye kikaratasi. Akaniambia "Hiyo ndio namba ya yule jamaa, hiyo 100k ndio mgao wako, mtafute umrudishie walau nusu hasara"

Nikabaki nimetoa macho tu.....

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu. Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
Unaingizwa kwny utapeli mkuu[emoji38]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Baada mjadala huo kuisha, ukaibuka mjadala wa hospital gani aende. Nikashauri twende Bugando Mwanza, kwanza ni karibu lakini pia pale Mama atakuwa chini ya uangalizi mzuri wa Dada. Mshua akashauri twende Dar, kule huduma ni nzuri na kuhusu sehemu ya kufikia atafikia kwangu.

Analyse: "Kule Mama hawezi kuwa comfortable tofauti na kwa Dada"

Mshua: "Kwanini asiwe comfortable?"

Analyse: "Sasa unadhani Mimi na wewe tutaweza kumpa uangalizi mzuri kuliko Dada?"

Mshua: "Kwani mpaka tumuangalie Mimi na wewe?"

Analyse: "Sasa nani mwingine atamuangalia?"

Mshua: "Mkeo"

Analyse: "Mke yupi Mzee?. Sina mke mjini Mimi"

Mshua: "Huna mke, au huwa anakuja na kuondoka?"

Mama: "Nyie mkishaanza kubishana hapo, mpaka apatikane mshindi Mimi ntakuwa nishajifia hapa"
 
Ila all in all Analyse una akili nyingi sana na ni mwandishi mzuri

Pili, una uwezo mkubwa wa kuhimili hisia maana masimango ya watu humu na bado unajibu kwa utulivu, no panic
Kuna some comments nilikuwa nikisoma mwenyewe nakasirika

Tatu, kupitia story hii walau nimepanua uelewa wangu wa namna ya kumuomba Mungu, kama mtu anafikia extent ya kwenda kwa mganga kupikwa, hizo ishu za kutapeliwa hutoboi bila msaada Mungu
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom