Sijawahi kuona brick-and-mortar store yoyote hapa Dar, lakini watu wana Gucci

Sijawahi kuona brick-and-mortar store yoyote hapa Dar, lakini watu wana Gucci

Kitu gani ni halisi au cha kiwango bora hasa kwenye hizi nchi maskini? Wakati mwingine hata kama unapesa yako na unataka kitu kizuri kukipata chenye ubora inakuwa shida. Ndio maana wengine wanaamua kuelekea kwenye mitumba tu angalau huko watapata vitu vya ukweli japo vimetumika.

Bidhaa nyingi, achilia mbali mavazi, zinazotengenezwa kulenga soko la nchi zetu zina viwango duni sana.

Sawa, but the bootlegging is so brazen it makes you wonder about a lot of other things as well...
 
Miafrika Ndivyo Tulivyo

famba hizo maneno nchi wang kacheza makaratee🙄
 
Na hapo ndio hoja yako inapokuwa na mantiki kwamba vyombo au mamlaka husika hazifanyi kazi zao ipasavyo.

Imagine huko kwenye vyakula, vinywaji, na madawa....hakuna Coca-Cola na Pepsi feki kweli?

Hakuna Viagra feki huko mitaani ambazo huuzwa kwenye hayo maduka ya dawa baridi?

Lord have mercy!!
 
Watu wa kuungaunga utawajua tu!
Watu na hadhi zao wala hawana muda wa eti kushangaa fake products!
Asante JF kutufichia uhalisi wetu! Fake tuko wengi sana humu!
 
Imagine huko kwenye vyakula, vinywaji, na madawa....hakuna Coca-Cola na Pepsi feki kweli?

Hakuna Viagra feki huko mitaani ambazo huuzwa kwenye hayo maduka ya dawa baridi?

Lord have mercy!!

Mkubwa tunazunguka tu lakini maisha yetu huku kwetu ni siri ya Mungu tu. Kama unaambiwa familia nyingi wanaishi chini ya USD 1. Hizo bidhaa halali zenye ubora wangapi watazimudu?

Pamoja na hayo mamlaka husika hazitakiwi kushindwa kutimiza wajibu wao, madhara ni makubwa mno.

Wewe umeenda mbali sana. Kuna magari unayakuta barabarani hadi unajiuliza TBS wanakagua viwango vya vitu gani?

Mfano mwingine twende kwenye simu na vifaa vya elekronik kama vile kompyuta na televisheni. Unafikiri hizo zinazokuja huku ndio zinaenda huko nchi za wenzetu? Licha ya watu kumudu bei, sheria zao zinabana sana kuwalinda watumiaji wa bidhaa na kuweka ushindani sawa wa kibiashara pia.
 
Muhimu kupendeza......hiyo original achia wenye stress za maisha ya show-off
 
Mkuu, dunia imebadirika sana na uwepo wa technology+media ndo kabisa umerahisisha mambo. kuhusu bidhaa hizo original, kuna wenye pesa(mawe) wanaziagiza states kwenyewe. mwishoni mwa mwaka jana, nilicheki kampuni ya Ford wanazindua gari ya ford everist-titanium 5.7L na nilivyokuja bongo january this year, nikakutana na jamaa anasukuma uswazi the same car. kwa mswahili, only quantity and satisfaction matters kuliko ubora@Nyani Ngabu
 
Usiyemjua humjui tu.

Mimi si mtu wa kuvaa lifulana lina maandishi ya Gucci kifuani.

Siyo zangu kabisa.

Hivyo pole yako ipeleke kwingine maana kwangu umenoa.
Sikutaja nembo...nimejumuisha.
Na hiyo ndio hali halisi, iwe design au brand yoyote unayovaa zimeshafyatuliwa na wachina unless unavaa lubega hapo wachina bado.
 
Kilicho feki ni watu kuiga bidhaa za wengine na kuziuza kwa kutumia jina lao.

Wewe siyo Gucci kwa nini utengeneze kofia ya Gucci halafu uiuze kibandani?

Kwa nini usitumie jina jingine utumie jina lao?

Hapo ndipo ufeki ulipo.
Tunatekeleza Sera ya ujenzi wa viwanda, we kana imekuuma sana katakata ndimu za kutosha, tia pili pili mbuzi debe zima kisha tafuna usiku na mchana.
Nakuhakikishia hayo maumivu yatakutoka tu.
 
Pale unapotoka ulaya uje uswazi ili utambe na nguo yako yenye nembo maarufu alafu unakuta muokota chupa ameivaa then copyright....mbwembwe zote zitakuisha na kuishia JF kulia

Pole mkuu Mchina si mtu mzuri hata kidogo.
sana mamaeeee
 
Kilicho feki ni watu kuiga bidhaa za wengine na kuziuza kwa kutumia jina lao.

Wewe siyo Gucci kwa nini utengeneze kofia ya Gucci halafu uiuze kibandani?

Kwa nini usitumie jina jingine utumie jina lao?

Hapo ndipo ufeki ulipo.
mjini hapa bila kuwa mjanja utapata wapi pesa
 
Inauma sana unanunua nguo kwa dollar 100 afu unakuta inauzwa kariakoo kwa 10000


Ubaya wake ni kuwa yanapauka siku moja tu
Hiyo mitumba wanayokimbilia ndio nguo za dollar 100 na kuendelea

Ila na sisi Watanzania tusitume nguo hadi ichanike
 
Nasubiri Bugati fake toka China.

e275a3ec8064b685eabbb7be6e112df1.jpg
8d5468b03350441a14eea461ed6f0a48.jpg
 
Back
Top Bottom