Sijawahi kuona Mkutano Mkuu CCM( NEC) uliofeli kama huu

Sijawahi kuona Mkutano Mkuu CCM( NEC) uliofeli kama huu

Mikutano yote huwa iko vile, sema faida uliyoipata wewe huu Mkutano uliuona Mubashara

Ungeuona Mkutano ambao Lowassa alisimama akamwuliza Kikwete amweleze kwanini alimpakazia Richmond sijui ungesemaje!
Mikutano yoote abcd huwa zinatufikia
 
CCM kwa sasa imetoka kwenye utaratibu wa kuheshimu kura, kiasi kwamba kwao kura ni jambo la fashion tu. Kiongozi pamoja na kundi lake kwa sasa wanapanga Kiwango cha kura wazitakazo. Tabia hii ya kutoheshimu kura ni lazima itazua uasi.
Yeah ni hatari sana. Kutoheshinu Ballot Box na Mapenzi ya wananchi haina tofauti na Mapinduzi
 
Hakuna haja ya kuongea sana.

Ktk historia ya siasa za CCM kuna jambo limezuka na jambo hilo sio la kawaida.

Ccm imebaki inaendesha mikutano ya ndani yenye vitisho vikali mno.

Cha ajabu zaidi ni pale wanapotishana wao kwao na kutukanana wazi wazi.

Mkutano ulijaa matusi, kejeli, hasira, mipasho na vitisho dhidi ya mtu na mtu, mtu na kikundi au kundi dhidi ya kundi kutokana na ufuasi ndani ya chama.

Huu ni mkutano wa kwanza uliofeli kupindukia.

Ni mkutano ulio acha simanzi, hasira na majonzi kwa wanachama na kuacha aibu na fedheha kwa watanzania.

Sitaki kurudia yaliyosemwa na kuandikwa hapo Tar 7- 8 2022 Jijini Dodoma.

Ule mkusanyiko umeonesha kiwango kidogo cha Uaminifu, uadilifu na ubora.

Siku nyingine mkipanga mikutani basi hakikisheni mnamalizana tofauti zenu na sio lazima kuziweka wazi hadi watoto wadogo wanawacheka.

" labda mambo yaharibike saana"

Wikendi njema.
Hata mimi kada nimefadhaishwa na hali ya mkutano ule kukosa dira.
Kitendo cha kuwaweka mbele watu wasio na akili kama Yusufu Makamba kimenikera kwa kweli.
 
Acha ramli chonganishi,mkutano wa CCm umemalizika kwa kishindo na ushindi kwa kila eneo,umemalizika kwa umoja na mshikamano,umemalizika kwa kila mmoja kuelewa kazi iliyopo mbele yake,. Ni uchaguzi unaokwenda kukijenga chama mashinani,Ni uchaguzi ulioleta matumaini kwa watanzania,Ni uchaguzi uluowasha Taa ya Matumaini na ushindi katika kulijenga Taifa letu,Ni uchaguzi uliokipatia chama ushindi mkubwa Sana kwa kuwa kila mmoja ametambua kuwa chama ni kikubwa kuliko mtu binafsi. Ni uchaguzi uluowasha Wana CCM wakiwa wamoja na wenye mshikamano
Umepost thread saa 4 usiku, now ni saa SITA na nusu replies ni 4 tu.

Hujastuka tu kujua kuwa huna impact yoyote?
 
Hata mimi kada nimefadhaishwa na hali ya mkutano ule kukosa dira.
Kitendo cha kuwaweka mbele watu wasio na akili kama Yusufu Makamba kimenikera kwa kweli.
Kuwa kada wa chama hicho ni sawa na kusimama hadharani ukajipiga kifuani mara kadhaa na kukiri huna......!!!!!
 
Hayajatokea KWA Bahati mbaya!

ULE ni mpango kazi wa kuua Chama KWA kuleta taharuki KWA wenye nchi kukosa imani na chama Baada ya kuonyesha kuwa wanauana wao KWA wao tena wanaua Mwenyekiti aliepo madarakani!(rafer kauli ya kusema "kama wazee tulisema hapana")

KWA kauli hizo ni dhahiri wenye nchi watasema mmepoteza mvuto inahitajika nembo mpya!

Ile move jk anaijua VIZURI mno!sidhani kama Mzee Makamba anaielewa kama jk anavoielewa!!

Self analysis!

Ngoja tuone!

Kuna wana ccm wanalalamika kuwa idadi ya wa NEC Tanganyika Kuwa sawa Zanzibar sio sahihi hasa kuangalia idadi ya watu na uwakilishi kwa uwiano
 
Kuna wana ccm wanalalamika kuwa idadi ya wa NEC Tanganyika Kuwa sawa Zanzibar sio sahihi hasa kuangalia idadi ya watu na uwakilishi kwa uwiano
Tanzania kila kitu kinafanyika kutokana na mapenzi ya Rais aliyeko madarakani. Akiamua wazanzibara 40 vs watanganyika 20 hakuna atakayekohoa.
 
Acha ramli chonganishi,mkutano wa CCm umemalizika kwa kishindo na ushindi kwa kila eneo,umemalizika kwa umoja na mshikamano,umemalizika kwa kila mmoja kuelewa kazi iliyopo mbele yake,. Ni uchaguzi unaokwenda kukijenga chama mashinani,Ni uchaguzi ulioleta matumaini kwa watanzania,Ni uchaguzi uluowasha Taa ya Matumaini na ushindi katika kulijenga Taifa letu,Ni uchaguzi uliokipatia chama ushindi mkubwa Sana kwa kuwa kila mmoja ametambua kuwa chama ni kikubwa kuliko mtu binafsi. Ni uchaguzi uluowasha Wana CCM wakiwa wamoja na wenye mshikamano
Sasa kulikuwa na sababu gani ya Kikwete na Makamba kuongea yale maneno....!!? Naamini Maza bado naamini kuwa kuna watu ndani ya CCM wanamtesa Maza na 2025....!!
 
Back
Top Bottom