Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tangu uhuru Marais wote kabla ya mama Samia walikuwa wanaume, lakini sijawahi kusikia Rais kaitisha mkutano wa wanaume tu.

Kazi yetu ni kuondoa vikwazo vya elimu, mikopo na fursa nyingine kwa wanawake lakini sio kupandikiza chuki kwa wanawake dhidi ya wanaume ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakihemea kwaajili ya familia zao. Nani hajui kwamba wanaume duniani kote ndio wako majeshini, migodini, wakwezi wa minazi, waendesha malori na matrekta nk ili kuhudumia taifa na familia?

Taifa na dunia itangia kwenye shida nyingine kama tukisisitiza kuwa wanawake wanaonewa na wanaume, baadhi ya majukumu ya mwanamke yalitoka kwa Mungu mwenyewe. Usawa hauwezi kuanzia kwenye kazi za uongozi tu za wanawake waliosoma tu, bali usawa uanzie kwenye majukumu ya mtu wa kawaida kama vile ulinzi, uchimbaji, uvuvi, usafirishaji, ujenzi, usafirishaji, utoaji wa mahari, uchungaji mifugo, uchuuzi, nk kazi ambazo hata asiyekwenda shule anazifanya. Kila kitu kiende kwa usawa na sio sawa.

Tunaopiga kelele za usawa ni wale tu wqchache tuliopata nafasi ya kusoma ambao tunataka kupewa nafasi za kukaa ofisini lakini sio usawa kwenye kuchunga ng'ombe porini, kwenda jeshi, kuchimba migodini, kuvua samaki, kuendesha malori, kutoa mahari, nk.

Tusieneze chuki hizi dhidi ya watoto wetu wakiume na baba zao leo maana tutatengeneza tatizo kesho ambalo hata Mungu atashindwa kuweka mkono wake.
 
Oooh yes well said my friend!

Na hii imewaponza sana wanawake wengi kwenye familia zao na kuondoka nature inavyotaka na maadiko matakatifu.

Kama ni usawa basi iwe ni kwenye maeneo yoote mengine ni aibu hata kuyasema hapa😆😆😆😆
Kelele na madai haya ya wanawake wachache ni mwiba mkali kwa wanawake wa kawaida kwenye jamii. Baba hawapeleki mahitaji na wanakataa kuoa kuyakwepa manyanyaso kutoka kwa wanawake wanaosubiri jikoni waletewe cha kupika. Kupika sio kazi wanaume wanakula magengeni siku hizi ambako hata wauza supu ni wanaume wenzao.

Kuna tatizo kubwa linakuja kama dhana itakuwa wanawake wanaonewa na wanaume wakati ni kinyume chake. Mwanaume anauza madafu, anakoroga zege, anachimba madini na kuwapelekea wanawake nyumbani. Je, waache kufanya hivyo ili wao wakae nyumbani kufagia na kufua ili wanawake waende kutafuta madini na samaki?
 
Katika kipindi cha "Mahusiano katika familia" kilichorushwa leo na Radio One, mtaalamu wa saikolojia amedai wanaofikisha malalamiko kwake zaidi ya 99% ni wanawake. Na hata kwenye ofisi za Ustawi wa Jamii walalamikaji wengi ni wanawake. Kundi kubwa la hao ni wanawake wa kawaida tu.

Hoja hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuwezeshwa atimize majukumu yake ya kimaumbile na ulezi wa watoto na si kuwapa upendeleo kwenye nafasi za uongozi.

Hivyo basi juhudi zinazochukuliwa na viongozi wanawake zinajenga chuki na utengano katika jamii kwa kivuli cha "mwanamke anaonewa".
 
Sijaona kosa la Rais kuongea na wanawake, kwani wanawake ni ktk kundi miongoni mwa makundi ya jamii yetu yanayohitaji msaada wetu wa hali na mali. Kama aliweza kuongea na wazee wa Dar, kisha akaahidi kuongea na vijana huko Mwanza, akasema ataongea na wafanya biashara, ataongea na wapinzani, sasa ajabu iko wapi akiongea na wanawake?
 
Una chuki binafsi.

Aidha, umepitwa na wakati kwa maana habari ya wanaume kuwa juu ya wanawake ni ya kale sana; kama hatuko sawa asilimia kubwa ya wanaume wanaonewa na wanawake.
 
Katika kipindi cha "Mahusiano katika familia" kilichorushwa leo na Radio One, mtaalamu wa saikolojia amedai wanaofikisha malalamiko kwake zaidi ya 99% ni wanawake. Na hata kwenye ofisi za Ustawi wa Jamii walalamikaji wengi ni wanawake. Kundi kubwa la hao ni wanawake wa kawaida tu.

Hoja hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuwezeshwa atimize majukumu yake ya kimaumbile na ulezi wa watoto na si kuwapa upendeleo kwenye nafasi za uongozi.

Hivyo basi juhudi zinazochukuliwa na viongozi wanawake zinajenga chuki na utengano katika jamii kwa kivuli cha "mwanamke anaonewa".
Mwanamke lazima atadeka kama akipewa nafasi upendeleo ya kulalamika. Wewe utafanya nini kama mwanaume uko bize mchana kutwa unaendesha daladala kutafuta ugali wa familia huku nyumbani mwanamke wake anatumia mwanya huohuo kuingiza wanaume chumbani kwake kwa kisingizio kuwa mumewe hana nguvu za kiume, au anamwaga chakula, au anaiba hela kupeleka kwenye vikoba vya siri, au anapeleka nyumbani kwao, au anamwagamwaga chakula, au anahonga wanaume wengine, au anataka vijora vya ngoma?
 
Sijaona kosa la Rais kuongea na wanawake, kwani wanawake ni ktk kundi miongoni mwa makundi ya jamii yetu yanayohitaji msaada wetu wa hali na mali. Kama aliweza kuongea na wazee wa Dar, kisha akaahidi kuongea na vijana huko Mwanza, akasema ataongea na wafanya biashara, ataongea na wapinzani, sasa ajabu iko wapi akiongea na wanawake??
Jamii yetu tuendelee kuigawanya kwenye makundi ya watoto, vijana na wazee baaasi. Hata wanaume wana matatizo yao pia kama vile ajali za bodabada, ukosefu wa nguvu za kiume, ukosefu wa mahari, kuumia migodini, kuanguka kwenye minazi, kuadhiriwa na mavumbi ya randa nk. Hata wao wana shida, mbona hawaitwi kusikilizwa au hata kutiwa moyo?
 
Kasome kuhusu AFFIRMATIVE ACTION
 
dawa ni kutokiowa tu,,na ingewezekana wanaume wto tungegoma hata mwaka mzima kutongoza na kutowafanya wanawake iwe kitaa na majumbani,,hapa ote walioowa na wasio na wake ote tugome,,,wataona moto..
 
Back
Top Bottom