Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

Tangu uhuru Marais wote kabla ya mama Samia walikuwa wanaume, lakini sijawahi kusikia Rais kaitisha mkutano wa wanaume tu.

Kazi yetu ni kuondoa vikwazo vya elimu, mikopo na fursa nyingine kwa wanawake lakini sio kupandikiza chuki kwa wanawake dhidi ya wanaume ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakihemea kwaajili ya familia zao. Nani hajui kwamba wanaume duniani kote ndio wako majeshini, migodini, wakwezi wa minazi, waendesha malori na matrekta nk ili kuhudumia taifa na familia?

Taifa na dunia itangia kwenye shida nyingine kama tukisisitiza kuwa wanawake wanaonewa na wanaume, baadhi ya majukumu ya mwanamke yalitoka kwa Mungu mwenyewe. Usawa hauwezi kuanzia kwenye kazi za uongozi tu za wanawake waliosoma tu, bali usawa uanzie kwenye majukumu ya mtu wa kawaida kama vile ulinzi, uchimbaji, uvuvi, usafirishaji, ujenzi, usafirishaji, utoaji wa mahari, uchungaji mifugo, uchuuzi, nk kazi ambazo hata asiyekwenda shule anazifanya. Kila kitu kiende kwa usawa na sio sawa.

Tunaopiga kelele za usawa ni wale tu wqchache tuliopata nafasi ya kusoma ambao tunataka kupewa nafasi za kukaa ofisini lakini sio usawa kwenye kuchunga ng'ombe porini, kwenda jeshi, kuchimba migodini, kuvua samaki, kuendesha malori, kutoa mahari, nk.

Tusieneze chuki hizi dhidi ya watoto wetu wakiume na baba zao leo maana tutatengeneza tatizo kesho ambalo hata Mungu atashindwa kuweka mkono wake.
Hii nchi bwana kila rais na maajabu yake.
Awamu iliyopita kulikuwa na kila aina ya utopolo sasa nchi imegeuzwa kuwa nchi ya special groups [emoji1]
 
Hatupingi 50/50 na mama, dada Na wakazamjomba wetu lakini mkakati uanzie chini huku kwenye kuchunga ng'ombe, kuvua samaki, kusoma, kochomelea vyuma, kuchimba madini, kulima, kukwea kwenye minazi, kuendesha bodaboda, kuendesha malori, ufundi magari Na umeme Na nk ndiyo upande wenyewe polepole kuelekea maofisini. Mfuno huu was 50/50 kama utaanzia chini kabisa waliko watanzania wengi utakuwa imara Na utajipandisha wenyewe kwenye ngazi za ofisini kwakuwa maamuzi makubwa na mengi kwenye jamii hufanywa kwenye ngazi ya familia, kaya, mtaa, kitongoji, kijiji,kata, tarafa, na wilaya.

Wasomi wetu hawataki hilo wanakimbilia kule juu kabisa waliko wachache
 
Usawa hauwezi kuanzia kwenye kazi za uongozi tu za wanawake waliosoma tu, bali usawa uanzie kwenye majukumu ya mtu wa kawaida kama vile ulinzi, uchimbaji, uvuvi, usafirishaji, ujenzi, usafirishaji, utoaji wa mahari, uchungaji mifugo, uchuuzi, nk kazi ambazo hata asiyekwenda shule anazifanya. Kila kitu kiende kwa usawa na sio sawa.
 
Back
Top Bottom