Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

Katika mada mbovu inayotrend muda wote ni hii ya usawa wa jinsia. Unafanya vijana wenye vipaji vyao kama diamond asioe , Zamani nilwalaumu kwa nini hawaoi wakatulia na mke mmoja. Lakini sasa fikiria mwanaume anazalisha mali labda tshs bilioni 5 ndani ya miaka mitano. Muda wote huo mke wake anakuwa nyumbani si ajabu na mahawara zake kijana anapiga shoo usiku wake na mchana ni wake.

Ngoja watofautiane waachane , hapo mwanamke eti sheria inasema alikuwa akimpikia kwa hiyo wamechuma mali pamoja. Dawa ni kuzalisha wanawake tofauti unatoa matunzo huko huko. Halafu mali urithi unaandika ni mama mzazi wako wewe unaehangaika , na taifa halitambui michango yenu inavyozidiana . HONGERA Platinumz una akili sana kwa za urothi ukuandika ni wa watoto wanawake wengine ni wajinga ,anaweza kukutanguliza kaburini abaki anafaidi mali yako kisa alikuhudumia kila kitu.

Ndio maana sikuza karibuni mataifa yaliyoendelea kama Marekani mnaweza kufunga ndoa yenye makubaliano maalum ili mkiachana msigawane mali ambazo mumechuma pamoja. Unaweza ukamjengea nyumba,unampa dola milioni kimi ,na marupurupu mengine almradi msigawane mali sawa ila hakikisha mkiachana haadhiriki.

Hivi zuckerbug wa facebook akigawana sawa na mke wake si hasara kubwa kwa mwanaume? Alijikunja hapati usingizi maabara na darasani halafu mke anakuwa equal share holder kiulaini tu? Hii sheria inastahikli kuangaliwa upya.
Hizo ndo haki sawa wanazozitaka wao sasa. [emoji1][emoji1] Kwamba Cha mwanaume ni cha wote na chao ni chao.

Sema wanashindwaga tu kuwa straight.
 
Sio Mbaya kwa Rais kuzungumza na makundi tofauti hususan ambayo anaona hayapewi fair ground...

Hapa Key word ni Fair na mimi am all for fairness ila sio favourtism..., kila anayefaa na apewe nafasi kulingana na uwezo na sio sababu ya jinsia yake..., yaani haya mambo ya 50 kwa 50 kwahio kama tuna wanawake wanaoweza 70 wale 20 waachwe ili tu namba itimie ? By the way wanufaika ni wengi waliopo mijini wapiga kelele wakati wale wa vijijini wanaendelea kunyanyasika kwenye mambo basic,,

50 kwa 50!! Najiuliza: 1) Endapo ikatokea wagombea nafasi za uwakilishi, hasa zenye viti maalumu, wakapita wengi wanawake, wakaongezewa na wa viti maalum, kwenye hivyo vyombo vya maamuzi itakuwaje? 2) Je, hilo limefikiriwa?
 
Mtoto wa kiume hana wa kumtetea. Kila kitu utasikia ....... mtoto wa kike.
Tunaimba kila biti ya wanaharakati uchwara.
Huko Ufaransa kuna sheria ya kuadhibu mamlaka zinazobagua jinsia ya kiume, kwa kuwa hali imekuwa mbaya.
"To every action, there is equal and opposite reaction ".
 
Kaka wanawake na wanaume unataka wawe sawa?? Haiwwzekani, kama vyoo tu vipo vya ke na me itakua hayo mengine...! Kuna siku ya wanawake na hamna siku ya wanaume..! Let them enjoy priority..!!
Kutenga siku kama hizo ni kuendeleza unyonge na unyanyapaa. Mwanamke sio kiumbe dhaifu wa kuonewa huruma kiasi hicho, mwanamke ana umahiri na udhaifu wake na mwanaume ana umahiri na udhaifu wake, wanapokuwa pamoja ndipo umahiri na udhaifu wao unapoonekana na kuimarishana, kudai kuwa wanawake wanaonewa ni endangered specie sio kweli kabisa.
 
wachaga hawatakagi ujinga ,jack ashawekwa pembeni kitambo
Eti mwanamke kwa kupika jikoni tu ghafla anawapiku wazazi wangu, dada na kaka zangu walionizaa, nilea na kunisomesha kwenye mali zangu.
 
dawa ni kutokiowa tu,,na ingewezekana wanaume wto tungegoma hata mwaka mzima kutongoza na kutowafanya wanawake iwe kitaa na majumbani,,hapa ote walioowa na wasio na wake ote tugome,,,wataona moto..
Hahaha we jamaa unamsimamo, nadhani haijawahi kutokea wanaume kuungana hivi hadi raha
 
Kujaza wanawake kwenye nafasi za kimaamuzi na kwenye ajira kunaenda kudidimiza maendeleo ya kiuchumi ya taifa na dunia kiujumla, maana mwanamke hajaumbwa afanye kazi wala atoe maamuzi dhidi ya wanaume. Ndo maana makazini unakuta wanawake ni kuonyesha mavazi, nywele, kucha na kujipitisha huku na kule wapate upendeleo, matokeo yake output ya kazi haionekani na taasisi zinazidi kulaumiwa kwa kukosa ufanisi...
Hata vitabu vya dini imeandikuwa kuwa mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu, sasa badala wanawake kudai haki yao ya kuzaa kwa uchungu tu wanataka kuzaa kuzaa kwa uchungu pamoja na kula kwa jasho kwa wakati mmoja. Ndiyo maana siku hizi kuna wengi wa wakina mama wanaokula kwa jasho ambao ni wavuta bangi, mashoga, wanalawitiwa, ni changudoa, hawapendi shule, nk kwakuwa baba na mama wote hawako nyumbani wanasaka pesa na kuacha watoto na dada wa kazi wawalee.
 
Mkutano uko mbioni tujiandae, Ndugai aketuombea ruhusa
 
Mkutano uko mbioni tujiandae, Ndugai aketuombea ruhusa
Tunafanya mzaha lakini liko tatizo kubwa jamii inalitengeneza kwa kukazana kudai wanawake ambao ni mama zetu, dada zetu, watoto wetu, na shangazi zetu wanaonewa na baba zao, watoto wao, wajomba zao, kaka zao na babu zao wenyewe kiasi kwamba watungiwe sheria binafsi wasiguswe, na wapewe mikopo, uongozi, elimu, nafasi Na upendeleo kwenye kila nyanja.

Sheria Na kanuni hizi ndizo zilizochangia kuibuka kwa ushoga, kusagana, ndoa kuvunjika, watu kutokuoa, kushuka kwa idadi ya watu Na kuzuka kwa watoto wengi wa nje ya ndoa. Tatizo hili ni kubwa sana nchi zilizoendelea kiasi cha wasichana wao kuja Afrika kutafuta wanaume wa kuzaa nao, ukifuga rasta tu jiandae kupata mke wa kizungu Na kwenda ulaya Na marekani.
 
Mwanamke lazima atadeka kama akipewa nafasi upendeleo ya kulalamika. Wewe utafanya nini kama mwanaume uko bize mchana kutwa unaendesha daladala kutafuta ugali wa familia huku nyumbani mwanamke wake anatumia mwanya huohuo kuingiza wanaume chumbani kwake kwa kisingizio kuwa mumewe hana nguvu za kiume, au anamwaga chakula, au anaiba hela kupeleka kwenye vikoba vya siri, au anapeleka nyumbani kwao, au anamwagamwaga chakula, au anahonga wanaume wengine, au anataka vijora vya ngoma?
Inasikitisha
 
50 kwa 50!! Najiuliza: 1) Endapo ikatokea wagombea nafasi za uwakilishi, hasa zenye viti maalumu, wakapita wengi wanawake, wakaongezewa na wa viti maalum, kwenye hivyo vyombo vya maamuzi itakuwaje? 2) Je, hilo limefikiriwa?
Tumeshafanya tathimini hao wa viti maalum wanarudisha nini kwa wanawake wenzao? ninachoona mimi ni mikogo, mikorogo, na wigi za bei dhidi ya wanawake wenzao.
 
Ukweli maza anapandikiza chuki sn
Uongozi bila maono ni kichekesho. Anatafuta watu wa kuhutubia kwa lazima. Anadhania hayo ndio matatizo ya wawanawake! Hivi amejiuliza hao wanawake anadhania wanaonewa ni Asilimia ngapi na wako wapi? Kama ni kweli wanawake wanapnewa Nchii Ingalikalika? Ameshafanya Utafiti kujua ni wanandoa wangapi wameachana kufuatia hayo Maonevu? Au anatafuta kura za Wajumbe na baadaye wanawake ili ashinde uchaguzi?
 
Tangu uhuru Marais wote kabla ya mama Samia walikuwa wanaume, lakini sijawahi kusikia Rais kaitisha mkutano wa wanaume tu.

Kazi yetu ni kuondoa vikwazo vya elimu, mikopo na fursa nyingine kwa wanawake lakini sio kupandikiza chuki kwa wanawake dhidi ya wanaume ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakihemea kwaajili ya familia zao. Nani hajui kwamba wanaume duniani kote ndio wako majeshini, migodini, wakwezi wa minazi, waendesha malori na matrekta nk ili kuhudumia taifa na familia?

Taifa na dunia itangia kwenye shida nyingine kama tukisisitiza kuwa wanawake wanaonewa na wanaume, baadhi ya majukumu ya mwanamke yalitoka kwa Mungu mwenyewe. Usawa hauwezi kuanzia kwenye kazi za uongozi tu za wanawake waliosoma tu, bali usawa uanzie kwenye majukumu ya mtu wa kawaida kama vile ulinzi, uchimbaji, uvuvi, usafirishaji, ujenzi, usafirishaji, utoaji wa mahari, uchungaji mifugo, uchuuzi, nk kazi ambazo hata asiyekwenda shule anazifanya. Kila kitu kiende kwa usawa na sio sawa.

Tunaopiga kelele za usawa ni wale tu wqchache tuliopata nafasi ya kusoma ambao tunataka kupewa nafasi za kukaa ofisini lakini sio usawa kwenye kuchunga ng'ombe porini, kwenda jeshi, kuchimba migodini, kuvua samaki, kuendesha malori, kutoa mahari, nk.

Tusieneze chuki hizi dhidi ya watoto wetu wakiume na baba zao leo maana tutatengeneza tatizo kesho ambalo hata Mungu atashindwa kuweka mkono wake.
Umesema la maana sana. Hawa wasomi ndio wanataka upendeleo kwenye vyeo kwa kisingizio cha usawa. Mungu alipanga majukumu ya mwanamke na mwanamume ndio maana mwanamke hata akiwa na uwezo kiasi gani hajisikii kama sawa kumuhudumia mwanamume bila kumdhalilisha kuhusu nafasi yake aliyopewa na mungu. Ndio maana wanaume wanawaepuka hao wenye uwezo kwani mwisho wanaweza kuambiwa na wao wabebe mimba 😂.
Ukweli tuwape nafasi wanawake kufuatana na uwezo wa kila mtu na tusiwabague au kuwanyanyasa.
 
Kelele na madai haya ya wanawake wachache ni mwiba mkali kwa wanawake wa kawaida kwenye jamii. Baba hawapeleki mahitaji na wanakataa kuoa kuyakwepa manyanyaso kutoka kwa wanawake wanaosubiri jikoni waletewe cha kupika. Kupika sio kazi wanaume wanakula magengeni siku hizi ambako hata wauza supu ni wanaume wenzao.

Kuna tatizo kubwa linakuja kama dhana itakuwa wanawake wanaonewa na wanaume wakati ni kinyume chake. Mwanaume anauza madafu, anakoroga zege, anachimba madini na kuwapelekea wanawake nyumbani. Je, waache kufanya hivyo ili wao wakae nyumbani kufagia na kufua ili wanawake waende kutafuta madini na samaki?
Uongozi bila maono ni kichekesho. Anatafuta watu wa kuhutubia kwa lazima. Anadhania hayo ndio matatizo ya wawanawake! Hivi amejiuliza hao wanawake anadhania wanaonewa ni Asilimia ngapi na wako wapi? Kama ni kweli wanawake wanapnewa Nchii Ingalikalika? Ameshafanya Utafiti kujua ni wanandoa wangapi wameachana kufuatia hayo Maonevu? Au anatafuta kura za Wajumbe na baadaye wanawake ili ashinde uchaguzi?
Aache kuongea vitu vyepesi vyepesi. Unapoongea Juu ya Wanawake kama Raisi wa Nchi unatakiwa uongee vitu vya kufikirisha. Aache kuongea lawama za wanawake dhidi ya wanaume wanapokuwa vyumbani. Kama wanawake wanaonewa yeye kafikaje hapo wakati kote alikopitia kulikuwa na wanaume? Wanaume wanamuonea vipi wakati wametimiza mpaka wajibu wa kumfanya azae? Kwani yeye anatakaje hasa? Kwani kuna wanaume huwa wanawateka wwanawake na kulazimisha mahusiano? Unajua hizi kauli za wanawake wanaonewa mara nyingi ni wamama waliofikia Menopause tu? Vinginevyo mbona mabinti wako busy kuwagombania wanaume hao hao?
 
Uongozi bila maono ni kichekesho. Anatafuta watu wa kuhutubia kwa lazima. Anadhania hayo ndio matatizo ya wawanawake! Hivi amejiuliza hao wanawake anadhania wanaonewa ni Asilimia ngapi na wako wapi? Kama ni kweli wanawake wanapnewa Nchii Ingalikalika? Ameshafanya Utafiti kujua ni wanandoa wangapi wameachana kufuatia hayo Maonevu? Au anatafuta kura za Wajumbe na baadaye wanawake ili ashinde uchaguzi?
Miaka 5 itaisha ana-promote na wanawake
 
Aache kuongea vitu vyepesi vyepesi. Unapoongea Juu ya Wanawake kama Raisi wa Nchi unatakiwa uongee vitu vya kufikirisha. Aache kuongea lawama za wanawake dhidi ya wanaume wanapokuwa vyumbani. Kama wanawake wanaonewa yeye kafikaje hapo wakati kote alikopitia kulikuwa na wanaume? Wanaume wanamuonea vipi wakati wametimiza mpaka wajibu wa kumfanya azae? Kwani yeye anatakaje hasa? Kwani kuna wanaume huwa wanawateka wwanawake na kulazimisha mahusiano? Unajua hizi kauli za wanawake wanaonewa mara nyingi ni wamama waliofikia Menopause tu? Vinginevyo mbona mabinti wako busy kuwagombania wanaume hao hao?
Huku kwenye halmashauri eti kuna mikopo ya vijana na mikopo ya wanawake. Yaani kwenye mikopo ya vijana wanawake wamo na kwenye mikopo ya wanawake wanawake wamo pia tena. Iko siku jambo kubwa litatokea. Chakusikitisha maspika wote wa bunge walikuwa ni wanaume wakati upuuzi kama huu ikipitishwa bungeni. Wabunge wanaume wamekaa kimya wakati treni linaelekea kwenda kukiponda kichwa cha mtoto wa kiume.

Siku moja nilisikitika sana pale mwanamke alipopewa mali zote za mume wake aliyefariki na kuwanyima wazazi na ndugu zake mume amabo walikuwa wakimtegemea mtoto na ndugu yao aliyefariki. Yule mwanamke akazitumia mali zile kuwatunzia wazazi wake na kuwasomesha wadogo zake shule za hela huku wazazi na ndugu wa mwanamume wakipiga miayo kwa njaa baada ya kifo cha ndugu yao. Huu ni upuuzi mkubwa kwa wazazi na ndugu za wanaume.
 
Back
Top Bottom