Sijawahi kuona mkutano wa Rais na wahudhuriaji wa jinsia moja tu

Hii nchi bwana kila rais na maajabu yake.
Awamu iliyopita kulikuwa na kila aina ya utopolo sasa nchi imegeuzwa kuwa nchi ya special groups [emoji1]
 
Hatupingi 50/50 na mama, dada Na wakazamjomba wetu lakini mkakati uanzie chini huku kwenye kuchunga ng'ombe, kuvua samaki, kusoma, kochomelea vyuma, kuchimba madini, kulima, kukwea kwenye minazi, kuendesha bodaboda, kuendesha malori, ufundi magari Na umeme Na nk ndiyo upande wenyewe polepole kuelekea maofisini. Mfuno huu was 50/50 kama utaanzia chini kabisa waliko watanzania wengi utakuwa imara Na utajipandisha wenyewe kwenye ngazi za ofisini kwakuwa maamuzi makubwa na mengi kwenye jamii hufanywa kwenye ngazi ya familia, kaya, mtaa, kitongoji, kijiji,kata, tarafa, na wilaya.

Wasomi wetu hawataki hilo wanakimbilia kule juu kabisa waliko wachache
 
Usawa hauwezi kuanzia kwenye kazi za uongozi tu za wanawake waliosoma tu, bali usawa uanzie kwenye majukumu ya mtu wa kawaida kama vile ulinzi, uchimbaji, uvuvi, usafirishaji, ujenzi, usafirishaji, utoaji wa mahari, uchungaji mifugo, uchuuzi, nk kazi ambazo hata asiyekwenda shule anazifanya. Kila kitu kiende kwa usawa na sio sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…