Sijawahi yaelewa kabisa madirisha ya aluminium, yamekaa kifakefake sana

Yaani tupo kama kondoo kufuata bila kufikiri. Bibi mmoja huko Iringa alikataa nyumba ya bati na kubaki nyumba ya nyasi kisa baridi kali kwenye nyumba ya bati. Lazima tuangalie na mazingira.
 
Wewe unafikiri watu hawapendi vigae? Unajua bei ya vigae kulinganisha na bati? Unajua maandalizi ya kuweka vigae? Kwanini mnashindwa kuelewa simple facts?
1. Madirisha ya aluminium ni cheap kulinganisha na ya mbao. Pia Yana muonekano mzuri.
2.Bati ni cheap kulinganisha na vigae
 
Yapo madirisha ya aluminum yanayofunguka kama ya mbao ni uamuzi wako tu. Unajua aluminum ni cheap kuliko mbao
 
Hayo unayoita madirisha ya mbao yapoje?
Yanakuwa kama ya Aluminium, lakini ni mbao na kioo na yote yanafunguka kwa nje au kwa ndani. Madirisha mengine mazuri ni yale ya vioo vya luvers.
 
Aluminium uzuri wake inategemea na eneo, mfano msimu wa baridi Aluminium ni nzuri sana, kipindi cha joto kama nyumba yako ni fupi na Ceiling yako sio ya Gypsum utakoma na joto.
Kwangu naona ni best kuliko mengine kwa vile kipindi cha mvua ya upepo madirisha mengine hayafai.
Pia Aluminiam inaongeza mwanga ndani lakini pia ni Sound proof ukifunga hata kelele za nje unazisikia kwa mbali.
 
Yaani hizi picha mbili zitakuambia na kuunga mkono hoja ya mleta uzi...haya madirisha ya aluminium hakuna kitu...dirisha ni la mbao tu tatizo letu kuigana...aluminium upande ile high end designing ndo nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…