Nina ndugu zangu wasabato, kila nilipowatembelea enzi hizo nikiwa dogo nilikuwa nikiambatana nao kwenda sabato (ukimtembelea msabato ikifika ijumaa jioni atakuacha, ila jumamosi atakukomalia sana mtaenda wote kanisani kwao, hivyo nilienda mara nyingi).
Kilichonikera ni hicho, yaani mara zote, mahala tofauti, wao wanahubiri spana dhidi ya Roman Catholic na kuizungumzia siku ya sabato tu, hawaendi nje ya hapo. Hata upendo sikuwahi kusikia wakiuzungumzia kabisa.
Sikuwahi kusikia wamezungumzia uislam na ijumaa wala walokole, wao ni wao na RC tu! Huwa najiuliza sana hawa watu wana ugomvi gani na RC?!