Sijivunii wazazi wangu

Naelewa unayopitia ila pambana tu na saidia pale unapoweza kusaidia ishi wewe ili kesho yako iwe bora kuliko jana na leo yako..
 
Muhimu uwaandalie watoto wako wasijewakakuona pia ulizingua.

Maisha yanapokuwa magumu sana ninkawaida kwa binadamu kudhani kuna mtu amechangia magumu yake.
 

Ni ujinga kuamini kuwa ukimsaidia Mama na Baba ati unafanikiwa,
Pia ni ujinga kuamini kuwa ATI Mama au Baba wakikuombea unafanikiwa.
Hizo ni Akili za kizamani Sana.
Hakuna mambo kama hayo.

Kama mzazi au MTU yeyote anakuchanganya mfungie Vioo. Achana naye
 
ulipo kuna single mother wangapi? Nani atawalea hao watoto?
Unachopaswa kufahamu ni kuwa hata mtoto kuzaliwa ni kwa neema yake Bwana...haijalishi mtoto amekaa miezi 9 katika tumbo la kahaba au mwanamke yeyote yule,,unapokuja duniani play part yako kama mtoto,,Mwenyezi Mungu alijua fika duniani kuna wazazi watadhalaurika na watoto wao,,,that's why akatoa AMRI na siyo OMBI ya kwamba "waheshimu baba na mama yako uishi miaka mingi na yenye kheri duniani".
 
Yaaan maisha ambay wazaz wankuwa hawapo pAmoja/ kuishi n mzaz wa Kambo
Ni moja kati ya mAish mAbaya saana #sitaki kukumbuka yaliyopita
Ila omba san mungu yaskupitie
 
Jitahidi sasa uwe mfano bora Kwa wanao
 
Labda tujiulize heshima maana yake nini?
Heshima ni sawa na neno RESPECT, (treat someone or something with kindness and care) hiyo ndiyo heshima tunayopaswa kuwapa wazazi wetu. Mapungufu yao hayabadili ukweli kuwa ni wazazi wako.

Tofautisha mapungufu na uhalifu au dhambi.

Kushindwa kumhudumia na kumtunza mtoto ni uhalifu, dhambi, ni kosa hata kisheria.
Hayo sio mapungufu unayotaka kusema.

Kama huwezi kuhudumia au kutunza Watoto usizae. Full stop.
Heshima inaenda kama utatimiza wajibu kama mzazi na sio uzae kama panya utelekeze Watoto alafu utake heshima ya Uzazi.
Hata panya analea Watoto wake.
 
Mzee naona watu mkiambiwa kuwajali wazazi wenu mnatoa mapovu 😁Basi yaishe pelekeni kwa michepuko!

NI kweli kwamba mzazi asiyetimiza majukumu yake anafanya uhalifu! Lakini siungi mkono kulipa kisasi kisa mzazi wako hakukujali.
 
Mzee naona watu mkiambiwa kuwajali wazazi wenu mnatoa mapovu 😁Basi yaishe pelekeni kwa michepuko!

NI kweli kwamba mzazi asiyetimiza majukumu yake anafanya uhalifu! Lakini siungi mkono kulipa kisasi kisa mzazi wako hakukujali.

Hakuna anayezungumzia mambo ya visasi hapa,
Mtoa mada ameeleza kero anayoipata Kutoka Kwa Wazazi wake wapumbavu.
Sio kosa kueleza kero hizo,
Mzazi ili aheshimiwe lazima ajiheshimu.
Heshima haiendi Kwa MTU burebure Kwa kigezo cha Ubaba au umama au umungu. Kama MTU hajiheshimu hawezi kuheshimiwa.

Kumjali MTU au kumpenda MTU ni ishu ya Hiyari sio Amri wala Sheria.
Hakuna sheria ya hivyo.
MTU kumjali mzazi inatokana na mahusiano yaliyojengeka tangu mwanzo.

Hizo hadithi za hisopo kuwa sijui mzazi akikuombea baraka au Laana ni hadithi za kitoto na zakijinga Sana ambazo huambiwa na kuaminiwa na watu WAJINGA.
 
Cha msingi pambana, ukipata hela, trust me. Utawakumbuka tu na utawasaidia iko hivo yaani.
Muda unaongea. Ww pambana. Huna haja ya kuwakumbuka wazee kwa kuandika machungu yako unayoyaona.
 
Robert Heriel ,kitendo cha kuwaita wazazi wa (ko, ke) wapumbavu kinakuweka kundi gani?

Wacha sisi tunaoiamini biblia tuonekane wajinga NARUDIA waheshimu wazazi wako!

kuna kisa kimoja NUHU alilewa mpaka akavua nguo, mwanae mmoja alimtazama akacheka akaenda kuwaambia wenzake! Wakachukua nguo wakamvalisha, walitembea kinyumenyume ili wasione utupu wa baba yao! Ingekuwa wewe Robert Heriel ungesema mzee wako ni mlevi kavua nguo
 
Shukuru mungu kwa yote!! Shukuru mungu tena kwa yote though yanauma lakin shukuru tu kaka..#usiwalaumu wazaz kutokuwa na viwanja, connection au wew kuzaliwa wao wakatengana, mungu anakusudi wew kupitia hayo yote vumilia na ushukuru.
 
Pole sanaa mkuu ila kumbuka siku zote kitanda hakizai haramu acha kulaumu shukuru Mungu kwa uhai ulionao ...ni kweli wengi wetu tunapitia nyakati ngumu lakin still we believe ipo cku tutafanikiwa ikiwa ni kuendelea kumwomba Mungu atufungulie njia ....changamoto unazopitia ni njia ya kukufanya uwe imara bila kukata tamaa ipo cku utatoboa believe that ,everythng is possible ,ila kuhusu kuwasaidia wazazi ni jambo zuri nakusihi endelea kuwasaidia kama unacho kama haujapata na huna kitu Mwenyezi Mungu anaona...sikuzote hatufanikiw kwa sababu tunalaumu sanaa amini hili maana mwenyezi Mungu anaona yote unayopitia...PRAY HARD
 
Mkuu uhalisia ulivyo wewe na hizo pesa zako unazopata kwenye kuuza mapazia nyote ni mali ya baba yako, namaanisha wewe na mapazia yako ni miliki ya baba yako so muheshimu tu na umpe pale utakapojaaliwa maana hilo litakuzidishia baraka.
🤣🤣🤣🤣umenikumbusha Uzi mmoja kule inteligence wa " sisi ni mifugo ya Mungu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…