Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

Muhimu uwaandalie watoto wako wasijewakakuona pia ulizingua.

Maisha yanapokuwa magumu sana ninkawaida kwa binadamu kudhani kuna mtu amechangia magumu yake.
shukran kwa maoni yako mkuu
 
Tofautisha mapungufu na uhalifu au dhambi.

Kushindwa kumhudumia na kumtunza mtoto ni uhalifu, dhambi, ni kosa hata kisheria.
Hayo sio mapungufu unayotaka kusema.

Kama huwezi kuhudumia au kutunza Watoto usizae. Full stop.
Heshima inaenda kama utatimiza wajibu kama mzazi na sio uzae kama panya utelekeze Watoto alafu utake heshima ya Uzazi.
Hata panya analea Watoto wake.
Big brow✊
 
mkuu heshima ipo kwa wazazi wangu na nawapenda nilichokizungumzia juu ni hisia zangu za kutokujivunia wao.
Minafikiri, nijambo jema na lenye kheri iliyojaa baraka na kujivunia ikiwa unawaona wazazi wako, niliwahi kumsikia mzee mmoja alisema...... hata masikini huzaa
 
Mzee naona watu mkiambiwa kuwajali wazazi wenu mnatoa mapovu 😁Basi yaishe pelekeni kwa michepuko!

NI kweli kwamba mzazi asiyetimiza majukumu yake anafanya uhalifu! Lakini siungi mkono kulipa kisasi kisa mzazi wako hakukujali.
kuna mzazi kalipwa kisasi mkuu mbona uzi wangu hauna lengo baya, Uzi wangu umelenga kueleza jinsi gani sijivunii kuwa na aina ya wazazi nilio nao ila ndo washakua no, way zaidi ya kupambana... Unamaana ya kwamba mtu akizaliwa kilema aufurahie? nop sio kweli ila anaweza tu kuridhia kishingo upande kwa kuwa hana jinsi.
 
Cha msingi pambana, ukipata hela, trust me. Utawakumbuka tu na utawasaidia iko hivo yaani.
Muda unaongea. Ww pambana. Huna haja ya kuwakumbuka wazee kwa kuandika machungu yako unayoyaona.
hata sasa nawakumbuka na ninawapenda pia mkuu.
 
kuna mzazi kalipwa kisasi mkuu mbona uzi wangu hauna lengo baya, Uzi wangu umelenga kueleza jinsi gani sijivunii kuwa na aina ya wazazi nilio nao ila ndo washakua no, way zaidi ya kupambana... Unamaana ya kwamba mtu akizaliwa kilema aufurahie? nop sio kweli ila anaweza tu kuridhia kishingo upande kwa kuwa hana jinsi.
Kwanza kwa kitendo cha wazazi wako kukuzaa na kukusomesha hadi darasa la 12, unapaswa kuwashukuru sana. Sio jambo jema na niukosefu wa hekima kuwasema wazazi wako vibaya kijana.
 
Kwanza kwa kitendo cha wazazi wako kukuzaa na kukusomesha hadi darasa la 12, unapaswa kuwashukuru sana. Sio jambo jema na niukosefu wa hekima kuwasema wazazi wako vibaya kijana.
nashukuru elimu ya bure lasivyo ningeishia la 8, Unaongea juujuu kwa kuwa hujui ni vitu gani nimepitia... Hukuwepo wakati nalia barabarani kama chizi hapa dar sijala kutwa na nobody alie-care, simu zao sikuziona kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa nawaomba wakati huo simu zangu kwao zilikuwa kero, japo wanitumie hela ya kula, Nimetembea sana na mguu hii Dar kwenda kibaruani na kurudi kwa ndugu zao walionitelekeza kwao... Nimechoteshwa maji usiku silali ili tu nipate chakula..... Simu zao zimeanza kuita baada ya kusikia mimi Nimepata kakazi ka uhakika.... Oi mkuu acha tu usi-comment hujui unachoandika
 
Umesema hivyo umenikumbusha mbali sana. Baba yangu mkubwa aliwahi kukopa ela bank na kumficha mkewe, wanakuja kufukuzwa nyumbani yule mama na watoto hawajui waende wapi na huyo mzee hajawahi kutoa hata mia ya kiberiti. Wanashanhaa deni kubwa hivyo alifanyia nini wakati watoto amewatelekeza hawahudumii kwa chochote:

Watoto wake wakubwa tu wameshalalamika hadi walichoka wanasema baba yao kukopa kote hata ada za wanae hajui. Anaehangaika ni mama yao tu. Amemnyanyasa sana mkewe hadi leo hii nnavyokwambia ana maisha hayo. Na hajali. Ndo maana mi huwa nawaangalia sana wanaume wanavyojitapa wakati ni wabinafsi. Sometimes wazazi mnazingua hadi basi af wanakwambia mzazi hakosei
 
sawa mkuu, hekima sina kwa sababu nimezaliwa na kulelewa na wasio na hekima
Yaani wewe maisha yako yatakua ni fumbo hadi mwisho wa dahari ...aisee ..uwe unasoma hata bible/quoran walau kujua wako ni nani hapa duniani! Hadi nasismka kusoma unavyoandika hapa...baba hana nyumba ni sawa, ubadhani babako anapenda kuishi kwa mamake? Unadhqni mamako anapenda kumwwita eti single mom?? Kwamba waloolewa wote wamefanikiwa yaani wewe utaishi na hii laana hadi kabiurini...TUBU😏
 
ahsante sana mkuu
Ila mdogo wangu pambana. Kama tayari una pa kujishikiza endelea kupambana sana huku ukimwomba Mungu. Wazazi wetu ndo hawahawa... wanatukera sana ila ndo wa kwetu hakuna namna. Ili kuepusha kuwakosea adabu jitahidi kukaa tu kimya na kwenye ishu ya vizinga wasaidie pale unapoweza. Ila Kama ni juu ya uwezo wake waambie straight huna uwezo. Mwanzoni wanaweza kutokukuelewa ila baadae wataelewa. Wazazi huwa wanajifanya hawajali ila deep down wanatupenda na kutuwaza sana.

Umefanya vyema kutemea hii nyongo huku JF maana kuna vijana wengine wameshawahi kuwatemea nyongo wazazi na kufikia pabaya. Kiimani na kwa desturi zetu mzazi hakosei. Kwa kabila letu mtu mzima akijamba anagombezwa mtoto aliyeko hapo na haitakiwi kubisha. Inatakiwa uombe msamaha kwa kujamba 😄😄. Piga kazi huku ukihakikisha unaenda sawa na wazazi wako. Cha muhimu kasoro za wazazi tusije tukazirithi. Turithi mazuri yao tu.
 
Yaani wewe maisha yako yatakua ni fumbo hadi mwisho wa dahari ...aisee ..uwe unasoma hata bible/quoran walau kujua wako ni nani hapa duniani! Hadi nasismka kusoma unavyoandika hapa...baba hana nyumba ni sawa, ubadhani babako anapenda kuishi kwa mamake? Unadhqni mamako anapenda kumwwita eti single mom?? Kwamba waloolewa wote wamefanikiwa yaani wewe utaishi na hii laana hadi kabiurini...TUBU😏
sawa mkuu nimekuelewa tuseme me ndo nina makosa kuongea ukweli.
 
Yaani wewe maisha yako yatakua ni fumbo hadi mwisho wa dahari ...aisee ..uwe unasoma hata bible/quoran walau kujua wako ni nani hapa duniani! Hadi nasismka kusoma unavyoandika hapa...baba hana nyumba ni sawa, ubadhani babako anapenda kuishi kwa mamake? Unadhqni mamako anapenda kumwwita eti single mom?? Kwamba waloolewa wote wamefanikiwa yaani wewe utaishi na hii laana hadi kabiurini...TUBU😏
Wazazi wangapi wa kitanzania wanaowaambia watoto wao wa kike wavumilie ndoa zenye manyanyaso hadi mabinti wao wanapata vilema na wengine vifo kisa kusisitizwa na wazazi kuvumilia upuuzi? Nimekupa tu mfano mdogo kukuonyesha kwamba baadhi ya wazazi wanakosea sana. Mabadiliko yanahitajika.
 
Back
Top Bottom