Sijui kwanini nimeumia hivi

Asante kwa ushauri mzuri mkuu, barikiwa sana🙏🙏
 
Alafu unatoka Songea Mjini mpaka Peramiho mission mbali kinoma, Anyway take it easy but punguza kujali sana
Kwakweli, sema wengine kua na roho mbaya hatuwezi na tuna mioyo midogo.. kuumia ni kitendo cha dakika sifuri.. But thanks Lord comments zenu zimenipa relief
 
Mimi kanuni zangu za kusaidia ni Tatu tu:
1. Nasaidia kilicho ndani ya uwezo wangu na kusaidia Kwa pesa yangu. kama uwezo huo Sina hata uwe na shida ya namna gani na kumwaga machozi, my friend siwezi kukusaidia hata kidogo kwanini nasaidia kilicho ndani ya uwezo wangu? Ni kwasababu najua kabisa unaweza kuchukua au kukopa pesa mahali kwasababu ya shida ya mtu Fulani ambapo baadae najua lazima itakucost aidha Kwa kujuta, roho kuuma, madeni nk....hivyo ushauri wangu ni kuwa ukitaka kumsaidia mtu hakikisha kama ni pesa basi unayo na ni ya kwako si ya baba, rafiki Wala ndugu yeyote yule. Hii itakusaidia kujihisi na amani na mawazo kama " kwanza nimesaidia Kwa pesa yangu hivyo sijuti nitapata nyingine" nk fikra kama hizo ni positive hivyo ni vizuri Kwa afya yako ya akili.

2. Sisaidii kuzidi uwezo wangu. Kila binadamu ana kikomo chake cha kuweza kusaidia, tajiri wa billion moja hawezi kusaidia shida za bilioni kumi, hivyo hivyo Kwa binadamu wengine kwa level mbalmbal za kifedha walizonazo, hivyo kama kanuni yangu ya kwanza imekidhi yaani Nina pesa yangu mwenyewe lakini ninahitajika kutoa kikubwa zaidi ya nilichonacho basi huwa natoa ninachokimudu hicho hicho, watu huvuka vikomo vyao Kwa kutaka sifa, pongezi, kutumia hisia zaidi kuliko akili au kutokuona Hali halisi ilivyo.

3. Ninaposaidia sitegemei chochote kutoka mtu aidha ahsante, nashukuru nk Wala sizitaki kiasi ambacho ninapofanikiwa kusaidia mtu huwa natoweka haraka, binafsi mara nyingi naona aibu sana kupewa ahsante na ndio maana sometimes naona Bora kutumia watu wengine kusaidia Fulani Ili tu nibaki anonymous, hii hunisaidia kutokukaa na chuki, hasira, vinyongo na wivu nk. Kwasababu ukitegemea kupewa ahsante au return yoyote, mwisho usipopewa hiyo ahsante utaanza kujihisi vibaya mfano hasira, chuki, roho sijui kuuma, kujiapiza nk ambayo kimsingi ni negative situation unaivuta hivyo si nzuri kabisa.

USHAURI: Mimi sipendi kusaidiwa Wala kuonewa huruma, hivyo nakusihi na wewe usipende sana kusaidiwasaidiwa Wala kuonewa huruma maana sometimes kusaidiwa kibongobongo huwa ni deni hivyo pambana mwenyewe uhakikishe una msuli wa kuweza kusimama bila kulalamika.
 
Kwakweli, sema wengine kua na roho mbaya hatuwezi na tuna mioyo midogo.. kuumia ni kitendo cha dakika sifuri.. But thanks Lord comments zenu zimenipa relief
Kama una roho nzuri huwezi kubadirisha hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu, hata kama utajifanya una roho mbaya baadae utajihisi hatia tu. Unachoweza kufanya ni kupunguza kujali sana
 
I wish ningekua na roho kama yako mkuu.. But ipo siku naamini nitaweza, Barikiwa sana🙏
 
Pole sana mkuu.

umetenda wema Unataka ubaki hapohapo🤣(jokes)
 
Nakazia,
 
Ganga yajayo tu mkuu, dunia imekua ya ajabu sana.
Jaribu kuwa fair Mkuu haujui Mtu kaumiaje Kihisia halafu Wewe ulichokiandika hapo juu sio poa halafu huyu Member hanaga mambo ya ajabu ajabu yuko humble kwa watu wote humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…