Sijui kwanini waliamua kugawa kwa walimu vishikwambi baada ya sensa wakati kuna mambo mengine mengi yanahitaji matumizi ya vishikwambi?

Vilikuwa zaidi ya laki 6, walimu nchi nzima ni laki 2.5 TU!
 
Nimuhimu kwa serikali kubana matumizi,na hii ni sehemu ya kubana matumizi pia
 
Tekinolojia inabadili isee simu cha 2022 ukisema utumie 2024 unaweza kufail maana kuna app hazita kuwa supported kutoka na umri wa simu usika.

Ingawa kwa vile vishikwambi na quality ile inaonekana kabisa serikali ilipigwa vibaya mno sasa hasira zile wakaona bora wawape walimu tu wasivione huko store.
 

Faida zipo hasa kuandaa current notes,saizi wana andaa softcopy na wanaweka kwenye kishikwambi kisha wana updates kila wanapohitaji kufanya hivyo.tofauti na kuandika kwenye daftari.


Pia kutafuta resources mbali mbali za kufundishia,kutunza maendeleo ya watoto katika somo,kungiza matokeo na kutoa report kwa wakati.faida zipo nyingi
 
Daah kwa hiyo tujadili Laptop kweli Tanzania na watu wake ni maskini ila sio kwa level hiyo..
 
Nchi Ina Hela we wasiwasi wako WA nini? Tutanunua vingine pia kumbuka pia nchi ilipewa msaada ivyo vishikwambi na Japan
 
Unaona walimu hawavihitaji ?
Hata kama walivihitaji je uhitaji wao ulikuwa ni muhimu kuliko uhitaji ktk shughuri nyinginezo?
Dah!!
Sikubahatika kuviona,lakini kwa uelewa wangu,kama ni kwa ajili ya masuala ya serikali,systems zinaundwa na wataalam wa TEHAMA wa serikali hivyo kabla ya kuunda systems ni muhimu wazingatie version ya kifaa itakayotumika mfumo huo,sijui zilikuwa ni tablets ama iPAD?
 
Sawa,kuna mdau katudokeza hapo juu kwamba vilikuwa laki 6 na walimu wapo laki 2.5,hivi 3.5 yamkini tuvifanye reserve kwanini visitumike ktk kazi kama hii ya uboreshwaji wa daftari?
 
Kweli mzee ApK za nje ya playstore haziingii hata ufanyeje, pia app nyingi tu zonadunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…