Sijui kwanini waliamua kugawa kwa walimu vishikwambi baada ya sensa wakati kuna mambo mengine mengi yanahitaji matumizi ya vishikwambi?

Kubana matumizi kwa serikali ni muhimu,hapo ndipo msingi wa hoja ulipo pia,lahasha kuna mdau katujuza hapo juu kwamba vishikwambi vilikuwa laki 6,na walimu wapo lak 2.5,je hivyo laki 3.5 vi wapi? Kwanini visitumike kwa zoezi hili?
 
Inawezekana uwezo wako ukawa ni mdogo zaidi yangu,maana kama umeshindwa kuelewa mantiki ya nilichokiandika japo kidogo tu
Hukuandika kwa maana ya kuilaumu serikali kuwapa Walimu hivyo vishikwsmbi badala ya kuwapa computer,bali unaona kuwa ni vyema wasingeliwapa na kuendelea kuvitumia ktk shughuri nyingine.

Na hapo ndipo nmekuona kuwa una uwezo mdogo mno,ulipaswa kukosoa ni kwa nini wamewapa Walimu vishikwambi badala ya computer walizowaahidi.
 
Ni sababu ya ufinyu wa akili yako,? Kwani kuwapa laptop lilikuwa agizo la mtu au sera?,au mkakati wa wizara ? ,then unaweza kututhibitishia Pasi nashaka kwamba Upewaji wa vishikwambi ulikuwa na mantiki ya kimkakati,kimpango na kisera tangu ununuaji wake kwamba vikitumika katika zoezi la sensa watapewa walimu?,abadani wewe ni zumbukuku ashakumu si tusi ahadi ya mtu ata awe Rais wa nchi kama haipo katika ilani na sera ya chama si sehemu ya utekelezaji na haipaswi kuingia katika budget.katika budget ya wizara ya elimu,sayansi na tecnologia mwaka 2021-2022,2022-2023 ,kunasehemu walizungumzia uhitaji wa hivyo vifaa kwa walimu,?
 
Kwani kuna sehemu uliona ama kusikia Walimu wakiomba hivyo vishikwambi?
Kwa nini hukudai serikali inunue vingine kama umeona kuna uhitaji badala ya kuonesha chuki zako kwa Walimu kwa kupewa hivyo vishikwsmbi?
 
mkuu mbona unatumia ngv nyng kuliwazia taifa hili, kwamba kungekua na ulazima wa kuvitumia wangeshindwa kununua? be humble. Acha waalim waenjoy
 
Tablet nying sasa walizogawa hazisomi SIM CARD muda mwingi zinaandika NO SERVICE. Na tatizo hilo halirekebishiki
Tumia wi-fi!!!
Ila Wenzio walilibaini hilo mapema pamoja na matatizo ya kukataa App muhimu so why wamewapa watoto wachezee subway surfers
 
Already expired. Vingi vipo scraper room ya mafundi. Yaani ni vibovu visivyofaa kwa matumizi ya muda mrefu. Wangenunua samsung wasingegawa na iwapo wangegawa basi wangegaiana wabunge na maofisa wa juu.
Usifikiri wanasiasa hawana akili.
 
Bora wamewapa maticha maana wangeviiba vipotee km upepo.
 
Already expired. Vingi vipo scraper room ya mafundi. Yaani ni vibovu visivyofaa kwa matumizi ya muda mrefu. Wangenunua samsung wasingegawa na iwapo wangegawa basi wangegaiana wabunge na maofisa wa juu.
Usifikiri wanasiasa hawana akili.
Asante kwa taarifa,kwani vilikuwa aina gani maana sijawahi kuviona live,
 
Nahitimisha huu uzi kwamba,Serikali ilinunua vishikwambi visivyo na uwezo hivyo visingeweza kudumu na kutumia kwa majukumu Mazito ndio maana wakafanya maamuzi ya kuvigawa,lengo langu lilikuwa ni kuona ni namna gani wangeweza kubana matumizi kwa kutumia rasirimali zilizopo ilikurahisisha kazi na kuboresha mambo.

Hata hivyo kama waligundua hilo tume ya uchaguzi haipaswi kuboresha daftari kwa daftari na peni ya mkono lahasha hata kama wahamishia katika data base wenyewe maana lazima kutajitokeza uhuni mwingi hasa uwepo wa majina feki kuwakirisha watu fake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…