LGE2024 Sijui mgogoro huu utafika wapi wa Viongozi wa CCM katika Mtaa wa Nera, baadhi hawamtaki Mwenyekiti aliyemaliza muda wake

LGE2024 Sijui mgogoro huu utafika wapi wa Viongozi wa CCM katika Mtaa wa Nera, baadhi hawamtaki Mwenyekiti aliyemaliza muda wake

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
Imeelezwa kuna uwepo wa mgogoro wa viongozi wa CCM katika Mtaa wa Nera, Kata ya Isamilo, Manispaa ya Nyamagana.

Hayo yanajiri baada ya viongozi kutohitaji uwepo wa jina la Mwenyekiti aliyemliza muda wake (Abubakar Self) kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine kutokana na jitihada zake za kuibua uovu unaendelea kukithiri katika eneo hilo ikiwemo wizi, uvutaji bangi na mirungi na kuwa chanzo kikubwa cha vitendo vya unyanyasaji na ukatili kwa makundi mbalimbali ikiwemo watoto katika eneo hill

Imeelezwa katika kura za maoni Mwenyekiti (Abubakar Seif ) alishinda kwa kura 39 dhidi ya mpinzani wake 38

Sasa baada ya kushinda wakaibuka kundi ambalo lilianza kufanya vurugu na kusema uchaguzi urudiwe lakini Mwenyekiti aliyemaliza muda alikataa kwasababu alikuwa tayari ameshasaini nyaraka za kuidhinishwa.
Mwanza kura.jpg

Baada ya hapo ndipo Katibu wa kata hiyo akahairisha zoezi hilo na kuondoka na kura akaeleza baada ya siku mbili atazirejesha

Sintofahamu ilianzia wapi la sekeseke hili?
Baada ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake (Abubakar Seif) kuzungumza na waandishi wa habari kwa kile kilichotokea ndipo kamati ya maadili ikaamua kukata jina lake sababu kubwa nikwanini kazungumza na waandishi wa habari huku baadhi ya kundi wasilomtaka kushinda kwa mwenyekiti huyo wakafanya sherehe ya kufurahia hilo katika eneo ambalo lakibanda kimoja na kuanza kunywa pombe, uvutaji bangi na mirungi hatimae mmoja wa wanakikundi hicho akarekodi kila kitu na kutuma kwenye mamlaka husika

Hatua iliyofuata ni kukamatwa kwa wale wote walihusika kwenye tukio hilo na kuamuliwa kuvunjwa kwa kile kibanda kilichokuwa kinatumika kufanya hiyo sherehe na bodaboba waliokuwa katika maeneo hayo wametakiwa kuondoka maeneo hayo kwani inaelezwa wao pia wanahusika na na biashara ya uuzaji na usambazaji wa mirungi

Hatua iliyopo katika sinema hii
Imebainika kuna mchezo mchafu unaendelea baina ya zoezi hilo hasa kwa mwenyekiti aliyemaliza muda wake na figisu Zilizopo ni katika kufifisha jitihada za Mwenyekiti huyo katika kuibua maovu yaliyopo na kupingwa na kikundi cha watu hao

sasa katika kutambua mchango wake hatimae maagizo yametolewa ya kwamba Mwenyekiti huyo anahaki zote ndipo akatakiwa kwenda kuchukua fomu na hii leo amefanikisha hilo na anatarajia kuwa miongoni mwa Wenyeviti waliopita katika kura za maoni na kukutana.

Lakini wajuzi wa mambo wameeleza kuwa hilo si eneo moja kwa Mkoa wa Mwanza kwani yapo maeneo mengi yaliyopitia changamoto hiyo ya kukatwa kwa baadhi ya majina ya waliopita kwenye nafasi mbalimbali na wengine kurejeshwa wengine laah!
 
kuna ukabila flani ivi upo ccm hata wakazi wengi wa pwani hawataki wakuja wawe viongozi.
 
Back
Top Bottom