Sijui niseme nini lakini Mungu alikuwa upande wetu jana.

Sijui niseme nini lakini Mungu alikuwa upande wetu jana.

Binti Sayuni03

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
1,075
Reaction score
1,913
Jana usiku niliandika humu kuwa nipo mbezi, napata vyombo. Sasa mchana watu niliokuwa nao walikuwa wamezianzia pombe tokea mchana, hadi kufika jioni walishalewa.

Tukatoka tukaenda G7 LOUNGE ipo kinyerezi nadhani sasa tulikuwa na magari mawili gari moja la mtu binafsi jingine ni la mtu mwingine lakini la ofisini kwao, sasa mimi nilikaa nyuma kwa hapa upande wa dereva huku kwa dereva kulikuwa na kijana mmoja na dereva, lile gari jingine alipanda mama na mumewe, hawa ni wazazi wa kijana mmoja tuliyekuja nae.

Huyu dereva wetu, ambaye mwenye hii gari ya ofisini kwao alikuwa anaendesha kwa spidi sana, wale niliokaa nao nyuma walikuwa wanamwambia aendelee kupaisha wamechoka kuishi hata wakifa basi, hii ni akili ya pombe ilikuwa. Mimi hapo muda huu moyo wangu haukuwa na amani kabisa.

Yaani gari ilikuwa inatembea kama inapaa😢😢 kufikia pale round about ya mbezi kwenye zile njia za kwenda kinyerezi na kwingineko mbele yetu likatokea fuso limeovateki bajaji kwahiyo likawa linakuja upande wetu na liko spidi ya hatari, aisee hapa nilikiona kifo hiki hapa mbele yetu.

Katika kulikwepa gari dereva akapeleka gari mtaroni, hapa pongezi kwake dereva bila hivyo tulikuwa tunaenda kugonga fuso uso kwa uso. Ilikuwa kama movie hii, kwanza pombe zote ziliisha kichwani, sijaamini mpaka dakika hii kama nimeweza kutoka salama pale, aliyeumia ni mmoja shingoni tu, na gari ndiyo imepata hitilafu. Hili ni jambo la kumshukuru Mungu sana sasa hivi sijui ningekuwa nimekufa au nimeumia. Sina la zaidi ya kusema zaidi ya kumshukuru Mungu.

Nimepata funzo kubwa kuhusu hii ajali hakika nitaendelea kumtukuza Mungu. Pombe siyo nzuri kabisa😢🙌

Muwe na jumapili njema wakuu.
 
Jana usiku niliandika humu kuwa nipo mbezi, napata vyombo. Sasa mchana watu niliokuwa nao walikuwa wamezianzia pombe tokea mchana, hadi kufika jioni walishalewa.

Tukatoka tukaenda G7 LOUNGE ipo kinyerezi nadhani sasa tulikuwa na magari mawili gari moja la mtu binafsi jingine ni la mtu mwingine lakini la ofisini kwao, sasa mimi nilikaa nyuma kwa hapa upande wa dereva huku kwa dereva kulikuwa na kijana mmoja na dereva, lile gari jingine alipanda mama na mumewe, hawa ni wazazi wa kijana mmoja tuliyekuja nae.

Huyu dereva wetu, ambaye mwenye hii gari ya ofisini kwao alikuwa anaendesha kwa spidi sana, wale niliokaa nao nyuma walikuwa wanamwambia aendelee kupaisha wamechoka kuishi hata wakifa basi, hii ni akili ya pombe ilikuwa. Mimi hapo muda huu moyo wangu haukuwa na amani kabisa.

Yaani gari ilikuwa inatembea kama inapaa[emoji22][emoji22] kufikia pale round about ya mbezi kwenye zile njia za kwenda kinyerezi na kwingineko mbele yetu likatokea fuso limeovateki bajaji kwahiyo likawa linakuja upande wetu na liko spidi ya hatari, aisee hapa nilikiona kifo hiki hapa mbele yetu.

Katika kulikwepa gari dereva akapeleka gari mtaroni, ilikuwa kama movie hii, kwanza pombe zote ziliisha kichwani, sijaamini mpaka dakika hii kama nimeweza kutoka salama pale, aliyeumia ni mmoja shingoni tu, na gari ndiyo imepata hitilafu. Hili ni jambo la kumshukuru Mungu sana sasa hivi sijui ningekuwa nimekufa au nimeumia. Sina la zaidi ya kusema zaidi ya kumshukuru Mungu.

Nimepata funzo kubwa kuhusu hii ajali hakika nitaendelea kumtukuza Mungu.

Muwe na jumapili njema wakuu.
Usisahau siku ukipata ukatoe sadaka kwa kua amukutendea.
 
Daktari anamtibu mgonjwa ila sifa zote zinaenda kwa Mungu.

Kaa ukijua baraka za Mungu haziji kwako moja kwa moja, kuna watu wameandaliwa ili baraka zako zipite kwao kwanza.

Sijaona mahali umempongeza dereva.

Ni sawa na ajali ikiua msanii pamoja na wenzake, focus itakuwa kwenye mauti ya msanii tuu utadhani wale wengine waliokufa ni mbwa.
 
Dereva tulishampongeza baada ya ajali mkuu.
 
Back
Top Bottom