Siku 350 bila punyeto wala picha za ngono

Habari wakuu,

Kwa ufupi, nimekuwa nikifanya punyeto kuanzia 2003 mpaka February 2019. Iliniathiri sana kisaikojia na imenivurugia malengo yangu kwa kiwango kikubwa, wengi wanaofanya wanajua fedheha na madhara yake.

Nilijaribu kuacha miaka yote hii lakini nilikuwa nafanikiwa kwa muda mfupi tu; ndivyo wanavyofanya wengi walio katika tatizo hili.

Nikaamua kufanya maamuzi magumu ya kuacha, bila kujali nimeshindwa mara ngapi. Nimekuwa nikijisemea kauli hii "kitu chochote ambacho ukikiacha haufi kinawezekana kuacha" safari ilikuwa ngumu sana hasa siku100 za kwanza, nilishawishika sana katika nafsi yangu kuingia katika tovuti za ngono, lakini nilikaza nafsi na kusonga mbele.

Hivi nashukuru Mungu nimefikisha Siku 350 bila punyeto wala kuangalia picha za ngono, ninafuraha na akili yangu ipo huru zaidi kupambana na maisha. Ujasiri umeongezeka, na mwelekeo na malengo pia, pia ufanisi katika mapenzi upo vizuri bila kusahau mahusiano mazuri na marafiki pamoja na jamii kwa ujumla.

Namalizia kwa kusema kuacha punyeto na picha za ngono inawezekana, sio kwa dawa bali kwa uamuzi wa kweli kutoka moyoni na kujitoa muhanga kutimiza uamuzi wako. Mateso mwanzoni lazima, lakini baada ya muda mwili utazoea maisha mengine, na utakuwa huru hatimaye.

Anything without which you can't die is possible to let it go (chochote ambacho hakikufanyi uishi kinawezekana kuacha)

It is possible to break addiction, but not easy.

Mungu awabariki

Sent using Jamii Forums mobile app

UPDATES

Idadi ya Siku bila picha za ngono wala punyeto mpaka sasa =389 days(mwaka 1 na siku 24)

Naendelea kupambana,japo sasa hivi mapambano ni mepesi sana,yaani ni sawa na timu yako inaongoza kwa goli 6-0,halafu dakika za 75,unacheza kwa ku relax,halafu timu yenyewe unayocheza Nayo ni Liverpool na moto wake ule umeikalisha sita,sema nini pambano hili mwanzoni huwa ni gumu sana unaweza kata tamaa ( never give up) never lose hope,mm nimeweza wewe unashindwaje? Mm ni binadamu kama wewe,Mungu awabariki
Mungu atukuzwe kwa hilo
 
Hiki chama ukishachukua kadi ndio ntoleee iyo mazima

Hauachi, unapunguza tu ushiriki.
 
Uongo ,inategemea mtu na mtu wapo wengi tu walio saliti chama na wanatoboa miaka kibao cha msingi nia na mikakati imara.
 
Back
Top Bottom