#COVID19 Siku 60 zijazo Tanzania inaweza kuwa zaidi ya India kwenye suala la COVID-19

Kuna hatari kubwa sana mbele yetu. Hatua za lazima za tahadhari inapaswa zichukuliwe. Suala la kusema tuchukue tahadhari wakati mambo yanafanyika kimazoea yatatuletea vifo vya covid hadi tushangae
Kama unampenda kufa anza kufa wewe
 
Unapaswa kunijibu ina maana Tanzania ilikuwa na tahadhari zaidi ya USA, Brazil, Italia n.k

Jibu hilo swali acha kurukaruka
Mwanzoni tulikuwa nazo kuliko hao
 
Tanzania nchi ya mzaha mzaha kwenye kila kitu. Watanzania wengi ni watu wasiojali, yani hawajali chochote kiwe hatari au faida.

Watanzania hao hao kwenye kualalamika wanaongoza baada ya kupata madhara tayari ila ni wazito sana kufanya maamuzi...
Hizo siku 60 zijazo nitakukumbusha ili unipe takiwimu corona imeua watu wangapi katika familia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania nchi ya mzaha mzaha kwenye kila kitu. Watanzania wengi ni watu wasiojali, yani hawajali chochote kiwe hatari au faida.

Watanzania hao hao kwenye kualalamika wanaongoza baada ya kupata madhara tayari ila ni wazito sana kufanya maamuzi..
Hivi unawazaje kuandika mambo kama haya kuwatabiria Watanzania wenzako hata wanadamu wenzako mabaya. Watu kama nyie mnaitwa PSYCHOPATHS au WATU WENYE ROHO MBAYA. Hatufi tuna kinga nzito kutokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu aliyotuumba nayo. Tunaamini katika UKUU wa Meenyezi Mungu
 
Wanaokufa hawaamini huo ukuu?
 
Maisha yanaenda kasi sana, makundi haya uliyotaja ndio yalikuwa yanamuandama Hayati kuhusu tahadhari pamoja na juhudi alizofanya, lakini leo wako kimya kama hamna tena tatizo la upumuaji!
 
Mwakajana tulifanikiwa kwakuwa kila mtu aliwajibika ipasavyo, lakini ustaarabu ulivurugwa baadaye tulipoambiwa na watu walewale tena viongozi wataalamu wa afya wabobezi "...HAKUNA UGONJWA" leo hii mwananchi kuambiwa na watu walewale kuna ugonjwa wanaona kama wanachezeshwa twist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…