Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Umesahau! Nakushauri urudi nyuma step moja. Unaongelea hasara wakati wa Kikwete wakati kipindi cha ubinafsishaji tuliuza Nchi? Hasara gani hiyo wakati wa Kikwete inayoweza kuzidi ile ya kuuza Nchi? Makosa aliyofanya Kikwete, kama yapo, yote kwa asilimia 100 yalichangiwa na hali ya nchi alivyoikuta wakati anaingia madarakani. Still, aliweza kufanya kile alichoweza, pamoja na hali hiyo tete aliyoikuta wakati anaingia madarakani. Hicho kizingiti alichokikuta ni cha kihistoria katika nchi yetu, na sidhani kama atakuja kutokea Rais mwingine huko mbele ya safari, ambaye atakuja kuchukua nchi ikiwa kwenye hali tete kama aliyoikuta Kikwete!
 
Kamanda, mwaka huu twende tukaadhimishe dubai! Kila kitu jui yangu, ila sharti uje umevaa dera!
 
Haya maneno yetu huwa yanadumu hata tukiwa tumeenda zetu
 
Njoo uanzimishe
 
Kwakweli Jakaya Mrisho Kikwete aliliyumbisha Sana hili Taifa nakumbuka ndio enzi hizo kila nilipokuwa naingia Kwaro na mtu nisiemjua unashangaa naambiwa kijana unanijua kuwa Mimi Ni Nan? Dah yani ulikuwa Ni uongozi wa kupigana biti mwanzo mwisho... Mtu anafanya kila analojisikia katika jamii harfu anasema wewe Ni peleke unapojua..
Ndo hikihiki kipindi ambacho wanafunzi kupigwa Mimba ilikuwa kawaida Yan ndo kipind hichohicho Cha Kikwete ambapo ulikuwa unaweza kuingia guest na mwanafunzi akiwa amevaa sare za shule..

Daaah huu ulikuwa uongozi wa ajabu Sana sitaki hata uje kujirudia vizazi vyote..
 
Utanialika namie karamuni nije kunwa yokozuna,
 
JF jamani!
 
JF Raha Sana iko Kama maktaba ya Ardhi, kumbukumbu hazipotei
 
Natarajia siku moja mtoa post aje akane kauli yake kwani yaliyopo ni heri JK, uchumi ni tete, ajira ni balaa,wasiojulikana usiseme, demokrasia mmmhh chichemi. Ukiangalia maisha ya Mtanzania wa leo na yule wa JK kiuchumi ni tofauti sana, kwani tumebugi kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…